Isaya 50 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 50 (Swahili) Isaiah 50 (English)

Bwana asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo naliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu. Isaya 50:1

Thus says Yahweh, Where is the bill of your mother's divorce, with which I have put her away? or which of my creditors is it to whom I have sold you? Behold, for your iniquities were you sold, and for your transgressions was your mother put away.

Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu. Isaya 50:2

Why, when I came, was there no man? when I called, was there none to answer? Is my hand shortened at all, that it can't redeem? or have I no power to deliver? Behold, at my rebuke I dry up the sea, I make the rivers a wilderness: their fish stink, because there is no water, and die for thirst.

Mimi nazivika mbingu weusi, nami nafanya nguo ya magunia kuwa kifuniko chao. Isaya 50:3

I clothe the heavens with blackness, and I make sackcloth their covering.

Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao. Isaya 50:4

The Lord Yahweh has given me the tongue of those who are taught, that I may know how to sustain with words him who is weary: he wakens morning by morning, he wakens my ear to hear as those who are taught.

Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma. Isaya 50:5

The Lord Yahweh has opened my ear, and I was not rebellious, neither turned away backward.

Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate. Isaya 50:6

I gave my back to the strikers, and my cheeks to those who plucked off the hair; I didn't hide my face from shame and spitting.

Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya. Isaya 50:7

For the Lord Yahweh will help me; therefore I have not been confounded: therefore have I set my face like a flint, and I know that I shall not be disappointed.

Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni nani atakayeshindana nami? Na tusimame pamoja; ni nani aliye hasimu yangu? Na anikaribie basi. Isaya 50:8

He is near who justifies me; who will bring charges against me? Let us stand up together: who is my adversary? Let him come near to me.

Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia; ni nani atakayenihukumu kuwa mkosa? Tazama hao wote watachakaa kama vazi; nondo atawala. Isaya 50:9

Behold, the Lord Yahweh will help me; who is he who shall condemn me? Behold, all they shall wax old as a garment, the moth shall eat them up.

Ni nani miongoni mwenu amchaye Bwana, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la Bwana, na kumtegemea Mungu wake. Isaya 50:10

Who is among you who fears Yahweh, who obeys the voice of his servant? He who walks in darkness, and has no light, let him trust in the name of Yahweh, and rely on his God.

Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni. Isaya 50:11

Behold, all you who kindle a fire, who gird yourselves about with firebrands; walk you in the flame of your fire, and among the brands that you have kindled. This shall you have of my hand; you shall lie down in sorrow.