Isaya 48 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 48 (Swahili) Isaiah 48 (English)

Sikieni haya, enyi watu wa nyumba ya Yakobo, mnaoitwa kwa jina la Israeli, mliotoka katika maji ya Yuda; mnaoapa kwa jina la Bwana, na kumtaja Mungu wa Israeli, lakini si kwa kweli, wala si kwa haki. Isaya 48:1

Hear you this, house of Jacob, who are called by the name of Israel, and are come forth out of the waters of Judah; who swear by the name of Yahweh, and make mention of the God of Israel, but not in truth, nor in righteousness

Maana hujiita wenyeji wa mji mtakatifu, hujitegemeza juu ya Mungu wa Israeli; Bwana wa majeshi ni jina lake. Isaya 48:2

(for they call themselves of the holy city, and stay themselves on the God of Israel; Yahweh of Hosts is his name):

Mimi nimehubiri mambo ya kale tangu zamani; naam, yalitoka katika kinywa changu, nikayadhihirisha; naliyatenda kwa ghafula, yakatokea. Isaya 48:3

I have declared the former things from of old; yes, they went forth out of my mouth, and I shown them: suddenly I did them, and they happened.

Kwa sababu nalijua ya kuwa wewe u mkaidi, na shingo yako ni shingo ya chuma, na kipaji cha uso wako ni shaba; Isaya 48:4

Because I knew that you are obstinate, and your neck is an iron sinew, and your brow brass;

basi nimekuonyesha tangu zamani; kabla hayajatukia nalikuonyesha; usije ukasema, Sanamu yangu imetenda haya; sanamu yangu ya kuchonga, na sanamu yangu ya kuyeyusha, imeyaamuru. Isaya 48:5

therefore I have declared it to you from of old; before it came to pass I shown it you; lest you should say, My idol has done them, and my engraved image, and my molten image, has commanded them.

Umesikia haya; tazama haya yote; nanyi, je! Hamtayahubiri? Nimekuonyesha mambo mapya tangu wakati huu, naam, mambo yaliyofichwa, usiyoyajua. Isaya 48:6

You have heard it; see all this; and you, will you not declare it? I have shown you new things from this time, even hidden things, which you have not known.

Yameumbwa sasa, wala si tokea zamani; na kabla ya siku hii ya leo hukusikia habari yake; usije ukasema, Tazama, naliyajua. Isaya 48:7

They are created now, and not from of old; and before this day you didn't hear them; lest you should say, Behold, I knew them.

Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nalijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako; Isaya 48:8

Yes, you didn't hear; yes, you didn't know; yes, from of old your ear was not opened: for I knew that you did deal very treacherously, and was called a transgressor from the womb.

kwa ajili ya jina langu nitaahirisha hasira yangu, na kwa ajili yako nitajizuia, ili nisifiwe, wala nisikukatilie mbali. Isaya 48:9

For my name's sake will I defer my anger, and for my praise will I refrain for you, that I not cut you off.

Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuru ya mateso. Isaya 48:10

Behold, I have refined you, but not as silver; I have chosen you in the furnace of affliction.

Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu. Isaya 48:11

For my own sake, for my own sake, will I do it; for how should [my name] be profaned? and my glory I will not give to another.

Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia. Isaya 48:12

Listen to me, O Jacob, and Israel my called: I am he; I am the first, I also am the last.

Naam, mkono wangu umeuweka msingi wa dunia, na mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu; niziitapo husimama pamoja. Isaya 48:13

Yes, my hand has laid the foundation of the earth, and my right hand has spread out the heavens: when I call to them, they stand up together.

Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? Bwana amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo. Isaya 48:14

Assemble yourselves, all you, and hear; who among them has declared these things? He whom Yahweh loves shall perform his pleasure on Babylon, and his arm [shall be on] the Chaldeans.

Mimi, naam, mimi, nimenena; naam, nimemwita; nimemleta, naye ataifanikisha njia yake. Isaya 48:15

I, even I, have spoken; yes, I have called him; I have brought him, and he shall make his way prosperous.

Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake. Isaya 48:16

Come you near to me, hear you this; from the beginning I have not spoken in secret; from the time that it was, there am I: and now the Lord Yahweh has sent me, and his Spirit.

Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Isaya 48:17

Thus says Yahweh, your Redeemer, the Holy One of Israel: I am Yahweh your God, who teaches you to profit, who leads you by the way that you should go.

Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari; Isaya 48:18

Oh that you had listened to my commandments! then had your peace been as a river, and your righteousness as the waves of the sea:

Tena wazao wako wangalikuwa kama mchanga, na hao waliotoka katika tumbo lako kama chembe zake; jina lake lisingalikatika, wala kufutwa mbele zangu. Isaya 48:19

your seed also had been as the sand, and the offspring of your loins like the grains of it: his name would not be cut off nor destroyed from before me.

Haya, tokeni katika Babeli, Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo; Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya, Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni, Bwana amemkomboa mtumishi wake, Yakobo. Isaya 48:20

Go you forth from Babylon, flee you from the Chaldeans; with a voice of singing declare you, tell this, utter it even to the end of the earth: say you, Yahweh has redeemed his servant Jacob.

Wala hawakuona kiu alipowaongoza jangwani; Alitoa maji katika mwamba kwa ajili yao; Pia akaupasua mwamba, maji yakatoka kwa nguvu. Isaya 48:21

They didn't thirst when he led them through the deserts; he caused the waters to flow out of the rock for them; he split the rock also, and the waters gushed out.

Hapana amani kwa wabaya, asema Bwana. Isaya 48:22

There is no peace, says Yahweh, to the wicked.