Isaya 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 12 (Swahili) Isaiah 12 (English)

Na katika siku hiyo utasema, Ee Bwana, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo. Isaya 12:1

In that day you will say, "I will give thanks to you, Yahweh; for though you were angry with me, your anger has turned away and you comfort me.

Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Isaya 12:2

Behold, God is my salvation. I will trust, and will not be afraid; for Yah, Yahweh, is my strength and song; and he has become my salvation."

Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. Isaya 12:3

Therefore with joy you shall draw water out of the wells of salvation.

Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litajeni jina lake kuwa limetukuka. Isaya 12:4

In that day you will say, "Give thanks to Yahweh! Call on his name. Declare his doings among the peoples. Proclaim that his name is exalted!

Mwimbieni Bwana; kwa kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya katika dunia yote. Isaya 12:5

Sing to Yahweh, for he has done excellent things! Let this be known in all the earth!

Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako. Isaya 12:6

Cry aloud and shout, you inhabitant of Zion; for great in the midst of you is the Holy One of Israel!"