Isaya 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 17 (Swahili) Isaiah 17 (English)

Ufunuo juu ya Dameski. Tazama, Dameski umeondolewa usiwe mji, nao utakuwa chungu ya magofu. Isaya 17:1

The burden of Damascus. Behold, Damascus is taken away from being a city, and it shall be a ruinous heap.

Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu. Isaya 17:2

The cities of Aroer are forsaken; they shall be for flocks, which shall lie down, and none shall make them afraid.

Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema Bwana wa majeshi. Isaya 17:3

The fortress shall cease from Ephraim, and the kingdom from Damascus, and the remnant of Syria; they shall be as the glory of the children of Israel, says Yahweh of Hosts.

Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua-pungua, na kunona kwa mwili wake kutakonda. Isaya 17:4

It shall happen in that day, that the glory of Jacob shall be made thin, and the fatness of his flesh shall wax lean.

Tena itakuwa kama hapo avunaye ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai. Isaya 17:5

It shall be as when the harvester gathers the standing grain, and his arm reaps the ears; yes, it shall be as when one gleans ears in the valley of Rephaim.

Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema Bwana, Mungu wa Israeli. Isaya 17:6

Yet there shall be left therein gleanings, as the shaking of an olive tree, two or three berries in the top of the uppermost bough, four or five in the outmost branches of a fruitful tree, says Yahweh, the God of Israel.

Katika siku hiyo mwanadamu atamwangalia Muumba wake, na macho yake yatamtazama Mtakatifu wa Israeli. Isaya 17:7

In that day shall men look to their Maker, and their eyes shall have respect to the Holy One of Israel.

Wala hataziangalia madhabahu, kazi ya mikono yake; wala hatavitazama vilivyofanyika kwa vidole vyake, maashera na sanamu za jua. Isaya 17:8

They shall not look to the altars, the work of their hands; neither shall they have respect to that which their fingers have made, either the Asherim, or the sun-images.

Katika siku hiyo miji yake yenye maboma itakuwa kama mahali palipoachwa ndani ya mwitu, na juu ya kilele cha mlima, palipoachwa mbele ya wana wa Israeli; napo patakuwa ganjo. Isaya 17:9

In that day shall their strong cities be as the forsaken places in the wood and on the mountain top, which were forsaken from before the children of Israel; and it shall be a desolation.

Maana umemsahau Mungu wa wokovu wako, wala hukuukumbuka mwamba wa ngome yako; kwa sababu hiyo ulipanda mashamba yapendezayo, na kutia ndani yake mizabibu migeni. Isaya 17:10

For you have forgotten the God of your salvation, and have not been mindful of the rock of your strength; therefore you plant pleasant plants, and set it with strange slips.

Katika siku ile ulipopanda, ulifanya kitalu, na wakati wa asubuhi ulizimeesha mbegu zako, lakini mavuno yatatoweka siku ya huzuni, na ya sikitiko la moyo lifishalo. Isaya 17:11

In the day of your planting you hedge it in, and in the morning you make your seed to blossom; but the harvest flees away in the day of grief and of desperate sorrow.

Aha! Uvumi wa watu wengi! Wanavuma kama uvumi wa bahari; Aha! Ngurumo ya mataifa! Wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Isaya 17:12

Ah, the uproar of many peoples, who roar like the roaring of the seas; and the rushing of nations, that rush like the rushing of mighty waters!

Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani. Isaya 17:13

The nations shall rush like the rushing of many waters: but he shall rebuke them, and they shall flee far off, and shall be chased as the chaff of the mountains before the wind, and like the whirling dust before the storm.

Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu; Na kabla ya mapambazuko hawako; Hilo ndilo fungu lao watutekao, Na ajali yao wanaotunyang'anya mali zetu. Isaya 17:14

At evening, behold, terror; [and] before the morning they are no more. This is the portion of those who despoil us, and the lot of those who rob us.