Isaya 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 19 (Swahili) Isaiah 19 (English)

Ufunuo juu ya Misri. Tazama, Bwana amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake. Isaya 19:1

The burden of Egypt. Behold, Yahweh rides on a swift cloud, and comes to Egypt: and the idols of Egypt shall tremble at his presence; and the heart of Egypt shall melt in the midst of it.

Nami nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme. Isaya 19:2

I will stir up the Egyptians against the Egyptians: and they shall fight everyone against his brother, and everyone against his neighbor; city against city, [and] kingdom against kingdom.

Na roho ya Misri itamwagika kabisa katikati yake, nami nitayabatilisha mashauri yake, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli, na kwa wachawi. Isaya 19:3

The spirit of Egypt shall fail in the midst of it; and I will destroy the counsel of it: and they shall seek to the idols, and to the charmers, and to those who have familiar spirits, and to the wizards.

Nami nitawatoa hao Wamisri na kuwatia katika mikono ya bwana mgumu; na mfalme mkali atawatawala; asema Bwana, Bwana wa majeshi. Isaya 19:4

I will give over the Egyptians into the hand of a cruel lord; and a fierce king shall rule over them, says the Lord, Yahweh of Hosts.

Na maji ya baharini yatapunguka, na huo mto utakauka na kuwa pakavu. Isaya 19:5

The waters shall fail from the sea, and the river shall be wasted and become dry.

Na vijito vya mto vitatoa uvundo, na mifereji ya Misri itakuwa haina maji mengi, itakauka; manyasi na mianzi itanyauka. Isaya 19:6

The rivers shall become foul; the streams of Egypt shall be diminished and dried up; the reeds and flags shall wither away.

Vitu vimeavyo karibu na Nile, katika ukingo wa Nile, na vyote vilivyopandwa karibu na Nile vitakauka na kuondolewa na kutoweka. Isaya 19:7

The meadows by the Nile, by the brink of the Nile, and all the sown fields of the Nile, shall become dry, be driven away, and be no more.

Na wavuvi wataugua, na wote wavuao kwa ndoana watahuzunika, nao watandao jarife juu ya maji watazimia. Isaya 19:8

The fishermen shall lament, and all those who cast angle into the Nile shall mourn, and those who spread nets on the waters shall languish.

Tena wao wafanyao kazi ya kuchana kitani watafadhaika, na hao pia wafumao bafta. Isaya 19:9

Moreover those who work in combed flax, and those who weave white cloth, shall be confounded.

Na nguzo za nchi zitavunjika vipande vipande, wote wafanyao kazi ya mshahara watahuzunika nafsini mwao. Isaya 19:10

The pillars [of Egypt] shall be broken in pieces; all those who work for hire [shall be] grieved in soul.

Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, shauri lao limepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani? Isaya 19:11

The princes of Zoan are utterly foolish; the counsel of the wisest counselors of Pharaoh is become brutish: how do you say to Pharaoh, I am the son of the wise, the son of ancient kings?

Wako wapi, basi, watu wako wenye hekima? Na wakuambie sasa; na wajue mambo aliyokusudia Bwana wa majeshi juu ya Misri. Isaya 19:12

Where then are your wise men? and let them tell you now; and let them know what Yahweh of Hosts has purposed concerning Egypt.

Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu, wakuu wa Nofu wamedanganyika; na hao walio mawe ya pembeni ya kabila zake wameikosesha Misri. Isaya 19:13

The princes of Zoan are become fools, the princes of Memphis are deceived; they have caused Egypt to go astray, who are the corner-stone of her tribes.

Yeye Bwana ametia roho ya ushupavu katika moyo wa Misri, nao wameikosesha Misri katika matendo yake yote, kama mlevi aendavyo huko na huko akitapika. Isaya 19:14

Yahweh has mixed a spirit of perverseness in the midst of her; and they have caused Egypt to go astray in every work of it, as a drunken man staggers in his vomit.

Wala haitakuwako kazi yo yote katika Misri iwezayo kufanywa, ya kichwa au ya mkia, ya tawi au ya nyasi. Isaya 19:15

Neither shall there be for Egypt any work, which head or tail, palm-branch or rush, may do.

Katika siku hiyo Misri itakuwa kama wanawake; itatetemeka na kuogopa kwa sababu ya kutikiswa kwa mkono wa Bwana wa majeshi, autikisao juu yake. Isaya 19:16

In that day shall the Egyptians be like women; and they shall tremble and fear because of the shaking of the hand of Yahweh of Hosts, which he shakes over them.

Na nchi ya Yuda itakuwa sababu ya utisho kwa Misri; kila mtu atakayeambiwa habari zake ataingiwa na woga, kwa sababu ya kusudi la Bwana wa majeshi, analolikusudia juu yake. Isaya 19:17

The land of Judah shall become a terror to Egypt; everyone to whom mention is made of it shall be afraid, because of the purpose of Yahweh of Hosts, which he purposes against it.

Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia Bwana wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa uharibifu. Isaya 19:18

In that day there shall be five cities in the land of Egypt that speak the language of Canaan, and swear to Yahweh of hosts; one shall be called The city of destruction.

Katika siku hiyo itakuwako madhabahu katika nchi ya Misri kwa Bwana, na nguzo mpakani mwake kwa Bwana. Isaya 19:19

In that day shall there be an altar to Yahweh in the midst of the land of Egypt, and a pillar at the border of it to Yahweh.

Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa Bwana wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia Bwana kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa. Isaya 19:20

It shall be for a sign and for a witness to Yahweh of Hosts in the land of Egypt; for they shall cry to Yahweh because of oppressors, and he will send them a savior, and a defender, and he will deliver them.

Na Bwana atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua Bwana katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea Bwana nadhiri, na kuzitekeleza. Isaya 19:21

Yahweh shall be known to Egypt, and the Egyptians shall know Yahweh in that day; yes, they shall worship with sacrifice and offering, and shall vow a vow to Yahweh, and shall perform it.

Naye Bwana atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa Bwana, atakubali maombi yao na kuwaponya. Isaya 19:22

Yahweh will strike Egypt, smiting and healing; and they shall return to Yahweh, and he will be entreated of them, and will heal them.

Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri. Isaya 19:23

In that day shall there be a highway out of Egypt to Assyria, and the Assyrian shall come into Egypt, and the Egyptian into Assyria; and the Egyptians shall worship with the Assyrians.

Katika siku hiyo Israeli atakuwa wa tatu pamoja na Misri na Ashuru, watakuwa baraka kati ya dunia; Isaya 19:24

In that day shall Israel be the third with Egypt and with Assyria, a blessing in the midst of the earth;

kwa kuwa Bwana wa majeshi amewabariki, akisema, Wabarikiwe watu wangu Misri; na wewe Ashuru, kazi ya mikono yangu; na wewe Israeli, urithi wangu. Isaya 19:25

because Yahweh of Hosts has blessed them, saying, Blessed be Egypt my people, and Assyria the work of my hands, and Israel my inheritance.