Isaya 25 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 25 (Swahili) Isaiah 25 (English)

Ee Bwana, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli. Isaya 25:1

Yahweh, you are my God; I will exalt you, I will praise your name; for you have done wonderful things, [even] counsels of old, in faithfulness [and] truth.

Kwa sababu umefanya mji kuwa ni chungu; Mji wenye boma kuwa ni magofu; Jumba la wageni kuwa si mji; Hautajengwa tena milele. Isaya 25:2

For you have made of a city a heap, of a fortified city a ruin, a palace of strangers to be no city; it shall never be built.

Kwa hiyo watu walio hodari watakutukuza, Mji wa mataifa watishao utakuogopa. Isaya 25:3

Therefore shall a strong people glorify you; a city of awesome nations shall fear you.

Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Kivuli wakati wa hari; Wakati uvumapo upepo wa watu watishao, Kama dhoruba ipigayo ukuta. Isaya 25:4

For you have been a stronghold to the poor, a stronghold to the needy in his distress, a refuge from the storm, a shade from the heat, when the blast of the awesome ones is as a storm against the wall.

Kama vile hari katika mahali pakavu Utaushusha mshindo wa wageni; Kama ilivyo hari kwa kivuli cha wingu, Wimbo wa hao watishao utashushwa. Isaya 25:5

As the heat in a dry place will you bring down the noise of strangers; as the heat by the shade of a cloud, the song of the awesome ones shall be brought low.

Na katika mlima huu Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana. Isaya 25:6

In this mountain will Yahweh of Hosts make to all peoples a feast of fat things, a feast of wines on the lees, of fat things full of marrow, of wines on the lees well refined.

Naye katika mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote. Isaya 25:7

He will destroy in this mountain the surface of the covering that covers all peoples, and the veil that is spread over all nations.

Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo. Isaya 25:8

He has swallowed up death forever; and the Lord Yahweh will wipe away tears from off all faces; and the reproach of his people will he take away from off all the earth: for Yahweh has spoken it.

Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake. Isaya 25:9

It shall be said in that day, Behold, this is our God; we have waited for him, and he will save us: this is Yahweh; we have waited for him, we will be glad and rejoice in his salvation.

Kwa maana mkono wa Bwana utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji ya jaa. Isaya 25:10

For in this mountain will the hand of Yahweh rest; and Moab shall be trodden down in his place, even as straw is trodden down in the water of the dung-hill.

Naye atanyosha mikono yake katikati yake, kama vile aogeleaye anyoshavyo mikono yake ili aogelee, naye atashusha kiburi chake, pamoja na hila za mikono yake. Isaya 25:11

He shall spread forth his hands in the midst of it, as he who swims spreads forth [his hands] to swim; but [Yahweh] will lay low his pride together with the craft of his hands.

Na boma la ngome ya kuta zako ameliinamisha, na kulilaza chini, na kulitupa chini hata mavumbini. Isaya 25:12

The high fortress of your walls has he brought down, laid low, and brought to the ground, even to the dust.