Isaya 27 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 27 (Swahili) Isaiah 27 (English)

Katika siku hiyo Bwana, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini. Isaya 27:1

In that day Yahweh with his hard and great and strong sword will punish leviathan the swift serpent, and leviathan the crooked serpent; and he will kill the monster that is in the sea.

Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni. Isaya 27:2

In that day: A vineyard of wine, sing you to it.

Mimi, Bwana, nalilinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda. Isaya 27:3

I Yahweh am its keeper; I will water it every moment: lest any hurt it, I will keep it night and day.

Hasira sinayo ndani yangu; Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja. Isaya 27:4

Wrath is not in me: would that the briers and thorns were against me in battle! I would march on them, I would burn them together.

Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami. Isaya 27:5

Or else let him take hold of my strength, that he may make peace with me; [yes], let him make peace with me.

Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda. Isaya 27:6

In days to come shall Jacob take root; Israel shall blossom and bud; and they shall fill the surface of the world with fruit.

Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye? Isaya 27:7

Has he struck them as he struck those who struck them? or are they slain according to the slaughter of those who were slain by them?

Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki. Isaya 27:8

In measure, when you send them away, you do contend with them; he has removed [them] with his rough blast in the day of the east wind.

Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena. Isaya 27:9

Therefore by this shall the iniquity of Jacob be forgiven, and this is all the fruit of taking away his sin: that he makes all the stones of the altar as chalk stones that are beaten in sunder, [so that] the Asherim and the sun-images shall rise no more.

Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake. Isaya 27:10

For the fortified city is solitary, a habitation deserted and forsaken, like the wilderness: there shall the calf feed, and there shall he lie down, and consume the branches of it.

Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe. Isaya 27:11

When the boughs of it are withered, they shall be broken off; the women shall come, and set them on fire; for it is a people of no understanding: therefore he who made them will not have compassion on them, and he who formed them will show them no favor.

Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana atayapiga-piga matunda yake toka gharika ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli. Isaya 27:12

It shall happen in that day, that Yahweh will beat off [his fruit] from the flood of the River to the brook of Egypt; and you shall be gathered one by one, you children of Israel.

Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu. Isaya 27:13

It shall happen in that day, that a great trumpet shall be blown; and they shall come who were ready to perish in the land of Assyria, and those who were outcasts in the land of Egypt; and they shall worship Yahweh in the holy mountain at Jerusalem.