Isaya 31 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 31 (Swahili) Isaiah 31 (English)

Ole wao watelemkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Bwana! Isaya 31:1

Woe to those who go down to Egypt for help, and rely on horses, and trust in chariots because they are many, and in horsemen because they are very strong, but they don't look to the Holy One of Israel, neither seek Yahweh!

Lakini yeye naye ana akili, naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno yake; bali ataondoka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu. Isaya 31:2

Yet he also is wise, and will bring evil, and will not call back his words, but will arise against the house of the evil-doers, and against the help of those who work iniquity.

Basi Wamisri ni wanadamu wala si Mungu, na farasi zao ni nyama wala si roho; na Bwana atakaponyosha mkono wake, yeye asaidiaye atajikwaa, na yeye asaidiwaye ataanguka, nao wote pamoja watakoma. Isaya 31:3

Now the Egyptians are men, and not God; and their horses flesh, and not spirit: and when Yahweh shall stretch out his hand, both he who helps shall stumble, and he who is helped shall fall, and they all shall be consumed together.

Maana Bwana aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwana-simba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo Bwana wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake. Isaya 31:4

For thus says Yahweh to me, As the lion and the young lion growling over his prey, if a multitude of shepherds are called forth against him, will not be dismayed at their voice, nor abase himself for the noise of them: so will Yahweh of Hosts come down to fight on Mount Zion, and on the hill of it.

Kama ndege warukao, Bwana wa majeshi ataulinda Yerusalemu; ataulinda na kuuokoa, atapita juu yake na kuuhifadhi. Isaya 31:5

As birds hovering, so will Yahweh of Hosts protect Jerusalem; he will protect and deliver [it], he will pass over and preserve [it].

Mwelekeeni yeye mliyemwasi sana, enyi wana wa Israeli. Isaya 31:6

Turn you to him from whom you have deeply revolted, children of Israel.

Maana katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, ambazo mikono yenu imezifanya, zikawa dhambi kwenu. Isaya 31:7

For in that day they shall cast away every man his idols of silver, and his idols of gold, which your own hands have made to you for a sin.

Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamla; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi. Isaya 31:8

The Assyrian shall fall by the sword, not of man; and the sword, not of men, shall devour him; and he shall flee from the sword, and his young men shall become subject to forced labor.

Na mwamba wake utatoweka kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera hofu kuu, asema Bwana, ambaye moto wake u katika Sayuni, na tanuru yake katika Yerusalemu. Isaya 31:9

His rock shall pass away by reason of terror, and his princes shall be dismayed at the ensign, says Yahweh, whose fire is in Zion, and his furnace in Jerusalem.