Isaya 51 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 51 (Swahili) Isaiah 51 (English)

Nisikilizeni, ninyi mnaoifuatia haki; ninyi mnaomtafuta Bwana; uangalieni mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa, na tundu la shimo ambalo mlitolewa kwa kuchimbuliwa. Isaya 51:1

Listen to me, you who follow after righteousness, you who seek Yahweh: look to the rock whence you were hewn, and to the hold of the pit whence you were dug.

Mwangalieni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nalimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi. Isaya 51:2

Look to Abraham your father, and to Sarah who bore you; for when he was but one I called him, and I blessed him, and made him many.

Maana Bwana ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama bustani ya Edeni, na nyika yake kama bustani ya Bwana; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba. Isaya 51:3

For Yahweh has comforted Zion; he has comforted all her waste places, and has made her wilderness like Eden, and her desert like the garden of Yahweh; joy and gladness shall be found therein, thanksgiving, and the voice of melody.

Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu; nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka kwangu, nami nitaistarehesha hukumu yangu iwe nuru ya mataifa. Isaya 51:4

Attend to me, my people; and give ear to me, my nation: for a law shall go forth from me, and I will establish my justice for a light of the peoples.

Haki yangu i karibu, wokovu wangu umekuwa wazi, na mikono yangu itawahukumu kabila za watu; visiwa vitaningoja, navyo vitautumainia mkono wangu. Isaya 51:5

My righteousness is near, my salvation is gone forth, and my arms shall judge the peoples; the isles shall wait for me, and on my arm shall they trust.

Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na haki yangu haitatanguka. Isaya 51:6

Lift up your eyes to the heavens, and look on the earth beneath; for the heavens shall vanish away like smoke, and the earth shall wax old like a garment; and those who dwell therein shall die in like manner: but my salvation shall be forever, and my righteousness shall not be abolished.

Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu; msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwa sababu ya dhihaka zao. Isaya 51:7

Listen to me, you who know righteousness, the people in whose heart is my law; don't you fear the reproach of men, neither be you dismayed at their insults.

Maana nondo itawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi vyote. Isaya 51:8

For the moth shall eat them up like a garment, and the worm shall eat them like wool; but my righteousness shall be forever, and my salvation to all generations.

Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani. Isaya 51:9

Awake, awake, put on strength, arm of Yahweh; awake, as in the days of old, the generations of ancient times. Isn't it you who did cut Rahab in pieces, who pierced the monster?

Si wewe uliyemkata-kata Rahabu? Uliyemchoma yule joka? Si wewe uliyeikausha bahari, Na maji ya vilindi vikuu; Uliyevifanya vilindi kuwa njia, Ili wapite watu waliokombolewa? Isaya 51:10

Isn't it you who dried up the sea, the waters of the great deep; who made the depths of the sea a way for the redeemed to pass over?

Nao waliokombolewa na Bwana watarejea, Watafika Sayuni, wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; Watapata shangwe na furaha; Huzuni na kuugua zitakimbia. Isaya 51:11

The ransomed of Yahweh shall return, and come with singing to Zion; and everlasting joy shall be on their heads: they shall obtain gladness and joy; [and] sorrow and sighing shall flee away.

Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani? Isaya 51:12

I, even I, am he who comforts you: who are you, that you are afraid of man who shall die, and of the son of man who shall be made as grass;

Ukamsahau Bwana, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo afanyapo tayari kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye? Isaya 51:13

and have forgotten Yahweh your Maker, who stretched forth the heavens, and laid the foundations of the earth; and fear continually all the day because of the fury of the oppressor, when he makes ready to destroy? and where is the fury of the oppressor?

Yeye aliyehamishwa na kufungwa atafunguliwa kwa haraka; wala hatakufa na kushuka shimoni, wala chakula chake hakitapunguka. Isaya 51:14

The captive exile shall speedily be freed; and he shall not die [and go down] into the pit, neither shall his bread fail.

Maana mimi ni Bwana, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma. Isaya 51:15

For I am Yahweh your God, who stirs up the sea, so that the waves of it roar: Yahweh of Hosts is his name.

Bwana wa majeshi ndilo jina lake. Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu, ili nizipande mbingu, na kuiweka misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, Ninyi ni watu wangu. Isaya 51:16

I have put my words in your mouth, and have covered you in the shadow of my hand, that I may plant the heavens, and lay the foundations of the earth, and tell Zion, You are my people.

Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea, mkononi mwa Bwana, Kikombe cha hasira yake; Bakuli la kikombe cha kulevya-levya Umelinywea na kulimaliza. Isaya 51:17

Awake, awake, stand up, Jerusalem, that have drunk at the hand of Yahweh the cup of his wrath; you have drunken the bowl of the cup of staggering, and drained it.

Hapana hata mmoja wa kumwongoza Miongoni mwa wana wote aliowazaa, Wala hapana hata mmoja wa kumshika mkono Miongoni mwa wana wote aliowalea. Isaya 51:18

There is none to guide her among all the sons whom she has brought forth; neither is there any who takes her by the hand among all the sons who she has brought up.

Mambo haya mawili yamekupata; Ni nani awezaye kukusikitikia? Ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga; Niwezeje kukutuliza? Isaya 51:19

These two things have happened to you. Who will bemoan you? Desolation and destruction, and the famine and the sword; how shall I comfort you?

Wana wako wamezimia, Wamelala penye pembe za njia kuu zote Kama kulungu wavuni; Wamejaa hasira ya Bwana, Lawama ya Mungu wako. Isaya 51:20

Your sons have fainted, they lie at the head of all the streets, as an antelope in a net; they are full of the wrath of Yahweh, the rebuke of your God.

Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo; Isaya 51:21

Therefore hear now this, you afflicted, and drunken, but now with wine:

Bwana, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevya-levya, hilo bakuli la kikombe cha hasira yangu; hutakinywea tena; Isaya 51:22

Thus says your Lord Yahweh, and your God who pleads the cause of his people, Behold, I have taken out of your hand the cup of staggering, even the bowl of the cup of my wrath; you shall no more drink it again:

nami nitakitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake. Isaya 51:23

and I will put it into the hand of those who afflict you, who have said to your soul, Bow down, that we may go over; and you have laid your back as the ground, and as the street, to those who go over.