Isaya 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 11 (Swahili) Isaiah 11 (English)

Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. Isaya 11:1

There shall come forth a shoot out of the stock of Jesse, and a branch out of his roots shall bear fruit.

Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; Isaya 11:2

The Spirit of Yahweh shall rest on him, the spirit of wisdom and understanding, the spirit of counsel and might, the spirit of knowledge and of the fear of Yahweh.

na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; Isaya 11:3

His delight shall be in the fear of Yahweh; and he shall not judge after the sight of his eyes, neither decide after the hearing of his ears;

bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. Isaya 11:4

but with righteousness shall he judge the poor, and decide with equity for the humble of the earth; and he shall strike the earth with the rod of his mouth; and with the breath of his lips shall he kill the wicked.

Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia. Isaya 11:5

Righteousness shall be the belt of his waist, and faithfulness the belt of his loins.

Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Isaya 11:6

The wolf shall dwell with the lamb, and the leopard shall lie down with the kid; and the calf and the young lion and the fattened calf together; and a little child shall lead them.

Ng'ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng'ombe. Isaya 11:7

The cow and the bear shall feed; their young ones shall lie down together; and the lion shall eat straw like the ox.

Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Isaya 11:8

The sucking child shall play on the hole of the asp, and the weaned child shall put his hand on the adder's den.

Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari. Isaya 11:9

They shall not hurt nor destroy in all my holy mountain; for the earth shall be full of the knowledge of Yahweh, as the waters cover the sea.

Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu. Isaya 11:10

It shall happen in that day, that the root of Jesse, who stands for an ensign of the peoples, to him shall the nations seek; and his resting-place shall be glorious.

Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Isaya 11:11

It shall happen in that day, that the Lord will set his hand again the second time to recover the remnant of his people, who shall remain, from Assyria, and from Egypt, and from Pathros, and from Cush, and from Elam, and from Shinar, and from Hamath, and from the islands of the sea.

Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia. Isaya 11:12

He will set up an ensign for the nations, and will assemble the outcasts of Israel, and gather together the dispersed of Judah from the four corners of the earth.

Na wivu wa Efraimu utaondoka, na wale wanaomwudhi Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamhusudu Yuda, wala Yuda hatamwudhi Efraimu. Isaya 11:13

The envy also of Ephraim shall depart, and those who vex Judah shall be cut off: Ephraim shall not envy Judah, and Judah shall not vex Ephraim.

Nao watashuka, watalirukia bega la Wafilisti upande wa magharibi; nao pamoja watawateka wana wa mashariki; watanyosha mkono juu ya Edomu na Moabu; na wana wa Amoni watawatii. Isaya 11:14

They shall fly down on the shoulder of the Philistines on the west; together shall they despoil the children of the east: they shall put forth their hand on Edom and Moab; and the children of Ammon shall obey them.

Na Bwana atauangamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo wake uteketezao atatikisa mkono wake juu ya Mto, naye ataupiga, uwe vijito saba, na kuwavusha watu wenye viatu vikavu. Isaya 11:15

Yahweh will utterly destroy the tongue of the Egyptian sea; and with his scorching wind will he wave his hand over the River, and will strike it into seven streams, and cause men to march over in sandals.

Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri. Isaya 11:16

There shall be a highway for the remnant of his people, who shall remain, from Assyria; like as there was for Israel in the day that he came up out of the land of Egypt.