Isaya 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 5 (Swahili) Isaiah 5 (English)

Na nimwimbie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu katika habari za shamba lake la mizabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu, Kilimani penye kuzaa sana; Isaya 5:1

Let me sing for my well beloved a song of my beloved about his vineyard. My beloved had a vineyard on a very fruitful hill.

Akafanya handaki kulizunguka pande zote, Akatoa mawe yake, Akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri, Akajenga mnara katikati yake, Akachimba shinikizo ndani yake; Akatumaini ya kuwa utazaa zabibu, Nao ukazaa zabibu-mwitu. Isaya 5:2

He dug it up, Gathered out its stones, Planted it with the choicest vine, Built a tower in its midst, And also cut out a winepress therein. He looked for it to yield grapes, But it yielded wild grapes.

Na sasa, enyi wenyeji wa Yerusalemu, nanyi watu wa Yuda, amueni, nawasihi, kati ya mimi na shamba langu la mizabibu. Isaya 5:3

"Now, inhabitants of Jerusalem and men of Judah, Please judge between me and my vineyard.

Je! Ni kazi gani iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi, nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibu-mwitu? Isaya 5:4

What could have been done more to my vineyard, that I have not done in it? Why, when I looked for it to yield grapes, did it yield wild grapes?

Haya basi, sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa kitalu chake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa; Isaya 5:5

Now I will tell you what I will do to my vineyard. I will take away its hedge, and it will be eaten up. I will break down its wall of it, and it will be trampled down.

nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake. Isaya 5:6

I will lay it a wasteland. It won't be pruned nor hoed, But it will grow briers and thorns. I will also command the clouds that they rain no rain on it."

Kwa maana shamba la mizabibu la Bwana wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio. Isaya 5:7

For the vineyard of Yahweh of Hosts is the house of Israel, And the men of Judah his pleasant plant: And he looked for justice, but, behold, oppression; For righteousness, but, behold, a cry of distress.

Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hata hapana nafasi tena, nanyi hamna budi kukaa peke yenu kati ya nchi! Isaya 5:8

Woe to those who join house to house, Who lay field to field, until there is no room, And you are made to dwell alone in the midst of the land!

Bwana wa majeshi asema katika masikio yangu, Hakika majumba mengi yatakuwa ukiwa, naam, majumba makubwa, mazuri, yatakuwa hayana watu. Isaya 5:9

In my ears, Yahweh of Hosts says: "Surely many houses will be desolate, Even great and beautiful, unoccupied.

Kwa maana shamba la mizabibu la eka kumi litatoa bathi moja tu, na homeri ya mbegu itatoa efa tu. Isaya 5:10

For ten acres{Literally, ten yokes, or the amount of land that ten yokes of oxen can plow in one day, which is about 10 acres or 4 hectares.} of vineyard shall yield one bath,{1 bath is about 22 litres, 5.8 U. S. gallons, or 4.8 imperial gallons} And a homer{1 homer is about 220 litres or 6 bushels} of seed shall yield an ephah.{1 ephah is about 22 litres or 0.6 bushels or about 2 pecks)-- only one tenth of what was sown.}"

Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! Isaya 5:11

Woe to those who rise up early in the morning, that they may follow strong drink; Who stay late into the night, until wine inflames them!

Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao; lakini hawaiangalii kazi ya Bwana wala kuyafikiri matendo ya mikono yake. Isaya 5:12

The harp, lyre, tambourine, and flute, with wine, are at their feasts; But they don't regard the work of Yahweh, Neither have they considered the operation of his hands.

Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana. Isaya 5:13

Therefore my people go into captivity for lack of knowledge; Their honorable men are famished, And their multitudes are parched with thirst.

Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo. Isaya 5:14

Therefore Sheol{Sheol is the place of the dead.} has enlarged its desire, And opened its mouth without measure; And their glory, their multitude, their pomp, and he who rejoices among them, descend into it.

Na mtu mnyonge ainamishwa, na mtu mkubwa amedhilika, na macho yao walioinuka hunyenyekezwa, Isaya 5:15

So man is brought low, Mankind is humbled, And the eyes of the arrogant ones are humbled;

bali Bwana wa majeshi ametukuzwa katika hukumu, na Mungu aliye Mtakatifu ametakaswa katika haki. Isaya 5:16

But Yahweh of Hosts is exalted in justice, And God the Holy One is sanctified in righteousness.

Ndipo wana-kondoo watakapolisha kama katika malisho yao wenyewe, na mahali pao waliowanda, palipoachwa ukiwa, wageni watakula. Isaya 5:17

Then the lambs will graze as in their pasture, And strangers will eat the ruins of the rich.

Ole wao wavutao uovu kwa kamba za ubatili, na dhambi kama kwa kamba za gari! Isaya 5:18

Woe to those who draw iniquity with cords of falsehood, And wickedness as with cart rope;

Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona. Isaya 5:19

Who say, "Let him make speed, let him hasten his work, that we may see it; And let the counsel of the Holy One of Israel draw near and come, That we may know it!"

Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu! Isaya 5:20

Woe to those who call evil good, and good evil; Who put darkness for light, And light for darkness; Who put bitter for sweet, And sweet for bitter!

Ole wao walio wenye hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe! Isaya 5:21

Woe to those who are wise in their own eyes, And prudent in their own sight!

Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo; Isaya 5:22

Woe to those who are mighty to drink wine, And champions at mixing strong drink;

wampao haki mwenye uovu, ili wapewe ijara, na kumwondolea mwenye haki haki yake! Isaya 5:23

Who acquit the guilty for a bribe, But deny justice for the innocent!

Kwa hiyo kama vile mwali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika mwali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya Bwana wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli. Isaya 5:24

Therefore as the tongue of fire devours the stubble, And as the dry grass sinks down in the flame, So their root shall be as rottenness, And their blossom shall go up as dust; Because they have rejected the law of Yahweh of Hosts, And despised the word of the Holy One of Israel.

Kwa sababu hiyo hasira ya Bwana imewaka juu ya watu wake, naye amenyosha mkono wake juu yao; akawapiga, navyo vilima vilitetemeka, na mizoga yao ilikuwa kama takataka katika njia kuu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa. Isaya 5:25

Therefore Yahweh's anger burns against his people, And he has stretched out his hand against them, and has struck them. The mountains tremble, And their dead bodies are as refuse in the midst of the streets. For all this, his anger is not turned away, But his hand is still stretched out.

Naye atawatwekea bendera mataifa toka mbali, Naye atawapigia miunzi tokea mwisho wa nchi; Na tazama, watakuja mbio mbio upesi sana. Isaya 5:26

He will lift up a banner to the nations from far, And he will whistle for them from the end of the earth. Behold, they will come speedily and swiftly.

Miongoni mwao hakuna achokaye wala kukwaa; Hakuna asinziaye wala kulala usingizi; Wala mshipi wa viuno vyao hautalegea. Wala ukanda wa viatu vyao hautakatika; Isaya 5:27

None shall be weary nor stumble among them; None shall slumber nor sleep; Neither shall the belt of their loins be untied, Nor the latchet of their shoes be broken:

Mishale yao ni mikali, na pindi zao zote zimepindika; Kwato za farasi zao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli; Isaya 5:28

Whose arrows are sharp, And all their bows bent. Their horses' hoofs will be like flint, And their wheels like a whirlwind.

Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wana-simba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa. Isaya 5:29

Their roaring will be like a lioness. They will roar like young lions. Yes, they shall roar, And seize their prey and carry it off, And there will be no one to deliver.

Nao watanguruma juu yao siku hiyo Kama ngurumo ya bahari; Na mtu akiitazama nchi, ataona giza na dhiki Nayo nuru imetiwa giza katika mawingu yake. Isaya 5:30

They will roar against them in that day like the roaring of the sea. If one looks to the land, behold, darkness and distress. The light is darkened in its clouds.