Isaya 61 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 61 (Swahili) Isaiah 61 (English)

Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Isaya 61:1

The Spirit of the Lord Yahweh is on me; because Yahweh has anointed me to preach good news to the humble; he has sent me to bind up the broken-hearted, to proclaim liberty to the captives, and the opening [of the prison] to those who are bound;

Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; Isaya 61:2

to proclaim the year of Yahweh's favor, and the day of vengeance of our God; to comfort all who mourn;

kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe. Isaya 61:3

to appoint to those who mourn in Zion, to give to them a garland for ashes, the oil of joy for mourning, the garment of praise for the spirit of heaviness; that they may be called trees of righteousness, the planting of Yahweh, that he may be glorified.

Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi. Isaya 61:4

They shall build the old wastes, they shall raise up the former desolations, and they shall repair the waste cities, the desolations of many generations.

Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu. Isaya 61:5

Strangers shall stand and feed your flocks, and foreigners shall be your plowmen and your vine-dressers.

Bali ninyi mtaitwa makuhani wa Bwana; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao. Isaya 61:6

But you shall be named the priests of Yahweh; men shall call you the ministers of our God: you shall eat the wealth of the nations, and in their glory shall you boast yourselves.

Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele. Isaya 61:7

Instead of your shame [you shall have] double; and instead of dishonor they shall rejoice in their portion: therefore in their land they shall possess double; everlasting joy shall be to them.

Maana mimi, Bwana, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wivi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele. Isaya 61:8

For I, Yahweh, love justice, I hate robbery with iniquity; and I will give them their recompense in truth, and I will make an everlasting covenant with them.

Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika kabila za watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na Bwana. Isaya 61:9

Their seed shall be known among the nations, and their offspring among the peoples; all who see them shall acknowledge them, that they are the seed which Yahweh has blessed.

Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu. Isaya 61:10

I will greatly rejoice in Yahweh, my soul shall be joyful in my God; for he has clothed me with the garments of salvation, he has covered me with the robe of righteousness, as a bridegroom decks himself with a garland, and as a bride adorns herself with her jewels.

Maana kama nchi itoavyo machipuko yake, na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote. Isaya 61:11

For as the earth brings forth its bud, and as the garden causes the things that are sown in it to spring forth; so the Lord Yahweh will cause righteousness and praise to spring forth before all the nations.