Isaya 33 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 33 (Swahili) Isaiah 33 (English)

Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe. Isaya 33:1

Woe to you who destroy, and you weren't destroyed; and deal treacherously, and they didn't deal treacherously with you! When you have ceased to destroy, you shall be destroyed; and when you have made an end of dealing treacherously, they shall deal treacherously with you.

Ee Bwana, uturehemu; tumekungoja wewe; uwe wewe mkono wetu kila asubuhi,na wokovu wetu pia wakati wa taabu. Isaya 33:2

Yahweh, be gracious to us; we have waited for you: be our arm every morning, our salvation also in the time of trouble.

Kabila za watu wamekimbia wakisikia kelele za fujo; mataifa wametawanyika ulipojiinua nafsi yako. Isaya 33:3

At the noise of the thunder the peoples are fled; at the lifting up of yourself the nations are scattered.

Na mateka yako yatakumbwa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige. Isaya 33:4

Your spoil shall be gathered as the caterpillar gathers: as locusts leap shall men leap on it.

Bwana ametukuka; kwa maana anakaa juu; amejaza Sayuni hukumu na haki. Isaya 33:5

Yahweh is exalted; for he dwells on high: he has filled Zion with justice and righteousness.

Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha Bwana ni hazina yake ya akiba. Isaya 33:6

There shall be stability in your times, abundance of salvation, wisdom, and knowledge: the fear of Yahweh is your treasure.

Angalia, mashujaa wao wanalia nje, wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu. Isaya 33:7

Behold, their valiant ones cry outside; the ambassadors of peace weep bitterly.

Njia kuu zimeachwa, msafiri amekoma; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu. Isaya 33:8

The highways lie waste, the wayfaring man ceases: [the enemy] has broken the covenant, he has despised the cities, he doesn't regard man.

Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani. Isaya 33:9

The land mourns and languishes; Lebanon is confounded and withers away; Sharon is like a desert; and Bashan and Carmel shake off [their leaves].

Basi, sasa nitasimama; asema Bwana; sasa nitajiinua, sasa nitajitukuza. Isaya 33:10

Now will I arise, says Yahweh; now will I lift up myself; now will I be exalted.

Ninyi mtachukua mimba ya makapi, mtazaa majani makavu; pumzi yenu ni moto utakaowateketeza wenyewe. Isaya 33:11

You shall conceive chaff, you shall bring forth stubble: your breath is a fire that shall devour you.

Nao mataifa watakuwa kama kuchoma chokaa, kama miiba iliyokatika, iteketezwayo motoni. Isaya 33:12

The peoples shall be as the burning of lime, as thorns cut down, that are burned in the fire.

Sikieni, ninyi mlio mbali, niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uweza wangu. Isaya 33:13

Hear, you who are far off, what I have done; and, you who are near, acknowledge my might.

Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele? Isaya 33:14

The sinners in Zion are afraid; trembling has seized the godless ones: Who among us can dwell with the devouring fire? who among us can dwell with everlasting burning?

Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung'utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu. Isaya 33:15

He who walks righteously, and speaks blamelessly; he who despises the gain of oppressions, who shakes his hands from taking a bribe, who stops his ears from hearing of blood, and shuts his eyes from looking on evil:

Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma. Isaya 33:16

He shall dwell on high; his place of defense shall be the munitions of rocks; his bread shall be given [him]; his waters shall be sure.

Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri wake, yataona nchi iliyoenea sana. Isaya 33:17

Your eyes shall see the king in his beauty: they shall see a land that reaches afar.

Moyo wako utatafakari hofu ile; Yuko wapi yeye aliyehesabu? Yuko wapi yeye aliyeupima ushuru? Yuko wapi yeye aliyeihesabu minara? Isaya 33:18

Your heart shall muse on the terror: Where is he who counted, where is he who weighed [the tribute]? where is he who counted the towers?

Hutawaona watu wale wakali; watu wa maneno magumu usiyoweza kuyafahamu; wenye lugha ya kigeni usiyoweza kuelewa nayo. Isaya 33:19

You shall not see the fierce people, a people of a deep speech that you can not comprehend, of a strange language that you can not understand.

Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika. Isaya 33:20

Look on Zion, the city of our solemnities: your eyes shall see Jerusalem a quiet habitation, a tent that shall not be removed, the stakes of it shall never be plucked up, neither shall any of the cords of it be broken.

Bali huko Bwana atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo. Isaya 33:21

But there Yahweh will be with us in majesty, a place of broad rivers and streams, in which shall go no galley with oars, neither shall gallant ship pass thereby.

Kwa maana Bwana ndiye mwamuzi wetu; Bwana ndiye mfanya sheria wetu; Bwana ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa. Isaya 33:22

For Yahweh is our judge, Yahweh is our lawgiver, Yahweh is our king; he will save us.

Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza sana shina la mlingoti wao; hawakuweza kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka. Isaya 33:23

Your rigging is untied; they could not strengthen the foot of their mast, they could not spread the sail: then was the prey of a great spoil divided; the lame took the prey.

Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao. Isaya 33:24

The inhabitant shall not say, I am sick: the people who dwell therein shall be forgiven their iniquity.