Isaya 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 1 (Swahili) Isaiah 1 (English)

Haya ni maono ya Isaya, mwana wa Amozi, aliyoyaona katika habari za Yuda na Yerusalemu, siku za Uzia na Yothamu na Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda. Isaya 1:1

The vision of Isaiah the son of Amoz, which he saw concerning Judah and Jerusalem, in the days of Uzziah, Jotham, Ahaz, and Hezekiah, kings of Judah.

Sikieni, enyi mbingu, tega sikio, Ee nchi, kwa maana Bwana amenena; Nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi. Isaya 1:2

Hear, heavens, And listen, earth; for Yahweh has spoken: I have nourished and brought up children, And they have rebelled against me.

Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri. Isaya 1:3

The ox knows his owner, And the donkey his master's crib; But Israel doesn't know, My people don't consider.

Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha Bwana, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma. Isaya 1:4

Ah sinful nation, A people loaded with iniquity, A seed of evil-doers, Children who deal corruptly! They have forsaken Yahweh. They have despised the Holy One of Israel. They are estranged and backward.

Mbona mnataka kupigwa hata sasa, hata mkazidi kuasi? Kichwa chote ni kigonjwa, moyo wote umezimia. Isaya 1:5

Why should you be beaten more, That you revolt more and more? The whole head is sick, And the whole heart faint.

Tangu wayo wa mguu hata kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwa-zongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta. Isaya 1:6

From the sole of the foot even to the head there is no soundness in it: Wounds, welts, and open sores. They haven't been closed, neither bandaged, neither soothed with oil.

Nchi yenu ni ukiwa; miji yenu imeteketezwa kwa moto; nchi yenu, wageni wameila mbele ya macho yenu; nayo ni ukiwa, kana kwamba imeangamizwa na wageni. Isaya 1:7

Your country is desolate. Your cities are burned with fire. Strangers devour your land in your presence, And it is desolate, As overthrown by strangers.

Na binti Sayuni ameachwa kama kibanda katika shamba la mizabibu, kama kipenu katika shamba la matango, kama mji uliohusuriwa. Isaya 1:8

The daughter of Zion is left like a shelter in a vineyard, Like a hut in a field of melons, Like a besieged city.

Kama Bwana wa majeshi asingalituachia mabaki machache sana, tungalikuwa kama Sodoma, tungalifanana na Gomora. Isaya 1:9

Unless Yahweh of hosts had left to us a very small remnant, We would have been as Sodom; We would have been like Gomorrah.

Lisikieni neno la Bwana, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora. Isaya 1:10

Hear the word of Yahweh, you rulers of Sodom! Listen to the law of our God, you people of Gomorrah!

Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema Bwana. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo waume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng'ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi waume. Isaya 1:11

"What are the multitude of your sacrifices to me?," says Yahweh. "I have had enough of the burnt offerings of rams, And the fat of fed animals. I don't delight in the blood of bulls, Or of lambs, Or of male goats.

Mjapo ili kuonekana mbele zangu, ni nani aliyetaka neno hili mikononi mwenu, kuzikanyaga nyua zangu? Isaya 1:12

When you come to appear before me, Who has required this at your hand, to trample my courts?

Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada. Isaya 1:13

Bring no more vain offerings. Incense is an abomination to me; New moons, Sabbaths, and convocations: I can't bear with evil assemblies.

Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua. Isaya 1:14

My soul hates your New Moons and your appointed feasts; They are a burden to me. I am weary of bearing them.

Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu. Isaya 1:15

When you spread forth your hands, I will hide my eyes from you; Yes, when you make many prayers, I will not hear. Your hands are full of blood.

Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; Isaya 1:16

Wash yourselves, make yourself clean. Put away the evil of your doings from before my eyes; Cease to do evil.

jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. Isaya 1:17

Learn to do well. Seek justice, Relieve the oppressed, Judge the fatherless, Plead for the widow."

Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Isaya 1:18

"Come now, and let us reason together," says Yahweh: "Though your sins be as scarlet, they shall be as white as snow. Though they be red like crimson, they shall be as wool.

Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; Isaya 1:19

If you are willing and obedient, You shall eat the good of the land;

bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya. Isaya 1:20

But if you refuse and rebel, you shall be devoured with the sword; For the mouth of Yahweh has spoken it."

Mji huu uliokuwa mwaminifu umekuwaje kahaba! Yeye aliyejaa hukumu ya haki; haki ilikaa ndani yake, bali sasa wauaji! Isaya 1:21

How the faithful city has become a prostitute! She was full of justice; righteousness lodged in her, But now murderers.

Fedha yako imekuwa takataka, divai yako imechanganywa na maji. Isaya 1:22

Your silver has become dross, Your wine mixed with water.

Wakuu wako ni waasi, na rafiki za wevi; kila mtu hupenda rushwa, hufuata malipo; hawampatii yatima haki yake, wala maneno ya mjane hayawawasilii. Isaya 1:23

Your princes are rebellious, and companions of thieves. Everyone loves bribes, and follows after rewards. They don't judge the fatherless, Neither does the cause of the widow come to them.

Kwa hiyo, asema Bwana, Bwana wa majeshi, Mwenye enzi, wa Israeli, Nitapata faraja kwa hao wanipingao, nitatwaa kisasi kwa adui zangu; Isaya 1:24

Therefore the Lord, Yahweh of Hosts, The Mighty One of Israel, says: "Ah, I will get relief from my adversaries, And avenge myself of my enemies;

nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote; Isaya 1:25

And I will turn my hand on you, Thoroughly purge away your dross, And will take away all your tin.

nami nitarejeza upya waamuzi wako kama walivyokuwa hapo kwanza, na washauri wako kama hapo mwanzo; baada ya hayo utaitwa, Mji wa haki, mji mwaminifu. Isaya 1:26

I will restore your judges as at the first, And your counselors as at the beginning. Afterward you shall be called 'The city of righteousness, A faithful town.'

Sayuni itakombolewa kwa hukumu, na waongofu wake kwa haki. Isaya 1:27

Zion shall be redeemed with justice, And her converts with righteousness.

Lakini kuharibika kwao wakosao nao wenye dhambi kutatokea wakati mmoja, nao wamwachao Bwana watateketezwa. Isaya 1:28

But the destruction of transgressors and sinners shall be together, And those who forsake Yahweh shall be consumed.

Kwa maana watatahayarika kwa sababu ya mialoni mliyoitamani, nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua. Isaya 1:29

For they shall be ashamed of the oaks which you have desired, And you shall be confounded for the gardens that you have chosen.

Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka, na kama bustani isiyo na maji. Isaya 1:30

For you shall be as an oak whose leaf fades, And as a garden that has no water.

Na mtu hodari atakuwa kama makumbi, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima. Isaya 1:31

The strong will be like tinder, And his work like a spark. They will both burn together, And no one will quench them."