Isaya 37 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 37 (Swahili) Isaiah 37 (English)

Ikawa mfalme Hezekia aliposikia hayo, alizirarua nguo zake, akajivika nguo za magunia, akaingia katika nyumba ya Bwana. Isaya 37:1

It happened, when king Hezekiah heard it, that he tore his clothes, and covered himself with sackcloth, and went into the house of Yahweh.

Akamtuma Eliakimu aliyekuwa msimamizi wa nyumba yake na Shebna, mwandishi, na wazee wa makuhani, wamejivika nguo za magunia, waende kwa Isaya nabii, mwana wa Amozi. Isaya 37:2

He sent Eliakim, who was over the household, and Shebna the scribe, and the elders of the priests, covered with sackcloth, to Isaiah the prophet the son of Amoz.

Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wa tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa. Isaya 37:3

They said to him, Thus says Hezekiah, This day is a day of trouble, and of rebuke, and of rejection; for the children have come to the birth, and there is no strength to bring forth.

Yamkini Bwana, Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo amiri ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na Bwana, Mungu wako atayakemea maneno aliyoyasikia; basi, inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia. Isaya 37:4

It may be Yahweh your God will hear the words of Rabshakeh, whom the king of Assyria his master has sent to defy the living God, and will rebuke the words which Yahweh your God has heard. Therefore lift up your prayer for the remnant that is left.

Basi, watumishi wa mfalme Hezekia wakaenda kwa Isaya. Isaya 37:5

So the servants of king Hezekiah came to Isaiah.

Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu maneno haya; Bwana asema hivi, Usiyaogope maneno uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana. Isaya 37:6

Isaiah said to them, Thus shall you tell your master, Thus says Yahweh, Don't be afraid of the words that you have heard, with which the servants of the king of Assyria have blasphemed me.

Tazama, nitatia roho ndani yake, naye atasikia kivumi, na kurudi hata nchi yake mwenyewe, nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe. Isaya 37:7

Behold, I will put a spirit in him, and he shall hear news, and shall return to his own land; and I will cause him to fall by the sword in his own land.

Basi yule amiri akarudi, akamkuta mfalme wa Ashuru anafanya vita juu ya Libna; kwa maana alikuwa amesikia ya kwamba ameondoka, akaacha Lakishi. Isaya 37:8

So Rabshakeh returned, and found the king of Assyria warring against Libnah; for he had heard that he was departed from Lachish.

Naye alisikia habari ya Tirhaka, mfalme wa Kushi, ya kwamba, Ametoka ili kupigana nawe; naye aliposikia hayo, akatuma wajumbe kwa Hezekia, kusema, Isaya 37:9

He heard say concerning Tirhakah king of Ethiopia, He is come out to fight against you. When he heard it, he sent messengers to Hezekiah, saying,

Mwambieni Hezekia, mfalme wa Yuda, maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema, Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru. Isaya 37:10

Thus shall you speak to Hezekiah king of Judah, saying, Don't let your God in whom you trust deceive you, saying, Jerusalem shall not be given into the hand of the king of Assyria.

Tazama, umesikia habari ya mambo yote, ambayo wafalme wa Ashuru wamezitenda nchi zote, kwa kuziangamiza kabisa je! Utaokoka wewe? Isaya 37:11

Behold, you have heard what the kings of Assyria have done to all lands, by destroying them utterly: and shall you be delivered?

Je! Miungu ya mataifa, ambao baba zangu waliwaangamiza, wamewaokoa? Gozani, na Harani, na Resefu, na wana wa Adini waliokuwa katika Telasari? Isaya 37:12

Have the gods of the nations delivered them, which my fathers have destroyed, Gozan, and Haran, and Rezeph, and the children of Eden who were in Telassar?

Yuko wapi mfalme wa Hamathi, na mfalme wa Arpadi, na mfalme wa mji wa Sefarvaimu, wa Hena, na wa Iva? Isaya 37:13

Where is the king of Hamath, and the king of Arpad, and the king of the city of Sepharvaim, of Hena, and Ivvah?

Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya Bwana, akaukunjua mbele za Bwana. Isaya 37:14

Hezekiah received the letter from the hand of the messengers, and read it; and Hezekiah went up to the house of Yahweh, and spread it before Yahweh.

Hezekia akamwomba Bwana, akisema, Isaya 37:15

Hezekiah prayed to Yahweh, saying,

Ee Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia. Wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi. Isaya 37:16

Yahweh of hosts, the God of Israel, who sits [above] the cherubim, you are the God, even you alone, of all the kingdoms of the earth; you have made heaven and earth.

Tega sikio lako, Bwana, usikie; funua macho yako, Bwana, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, aliyopeleka ili kumtukana Mungu aliye hai. Isaya 37:17

Turn your ear, Yahweh, and hear; open your eyes, Yahweh, and behold; and hear all the words of Sennacherib, who has sent to defy the living God.

Ni kweli, Bwana, wafalme wa Ashuru wameziharibu nchi zote, na mashamba yao, Isaya 37:18

Of a truth, Yahweh, the kings of Assyria have laid waste all the countries, and their land,

na kuwatupa miungu yao motoni; kwa maana hao hawakuwa miungu, bali kazi ya mikono ya wanadamu; walikuwa miti na mawe, ndiyo sababu wakawaharibu. Isaya 37:19

and have cast their gods into the fire: for they were no gods, but the work of men's hands, wood and stone; therefore they have destroyed them.

Basi sasa, Bwana, Mungu wetu, utuokoe na mkono wake, falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe Bwana, wewe peke yako. Isaya 37:20

Now therefore, Yahweh our God, save us from his hand, that all the kingdoms of the earth may know that you are Yahweh, even you only.

Ndipo Isaya, mwana wa Amozi, akapeleka ujumbe kwa Hezekia, akisema, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa kuwa umeniomba juu ya Senakeribu, mfalme wa Ashuru, Isaya 37:21

Then Isaiah the son of Amoz sent to Hezekiah, saying, Thus says Yahweh, the God of Israel, Whereas you have prayed to me against Sennacherib king of Assyria,

tamko alilolitamka Bwana katika habari zake ndilo hili; Bikira, binti Sayuni, anakudharau, anakudhihaki sana; binti Yerusalemu anatikisa kichwa chake juu yako. Isaya 37:22

this is the word which Yahweh has spoken concerning him: The virgin daughter of Zion has despised you and ridiculed you; the daughter of Jerusalem has shaken her head at you.

Ni nani uliyemshutumu na kumtukana? Umeinua sauti yako juu ya nani, na kuinua macho yako juu? Juu ya Mtakatifu wa Israeli. Isaya 37:23

Whom have you defied and blasphemed? and against whom have you exalted your voice and lifted up your eyes on high? [even] against the Holy One of Israel.

Umemshutumu Bwana kwa watumishi wako, kwa kuwa umesema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani ya Lebanoni; nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misunobari yake mizuri, nami nitaingia ndani ya mahali pake palipoinuka, palipo mbali sana, msitu wa shamba lake lizaalo sana. Isaya 37:24

By your servants have you defied the Lord, and have said, With the multitude of my chariots am I come up to the height of the mountains, to the innermost parts of Lebanon; and I will cut down the tall cedars of it, and the choice fir trees of it; and I will enter into its farthest height, the forest of its fruitful field;

Nimechimba na kunywa maji, na kwa nyayo za miguu yangu nitaikausha mito yote ya Misri. Isaya 37:25

I have dug and drunk water, and with the sole of my feet will I dry up all the rivers of Egypt.

Je! Hukusikia? Ni mimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale; nikayatimiza sasa, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, ikawe chungu na magofu. Isaya 37:26

Have you not heard how I have done it long ago, and formed it of ancient times? now have I brought it to pass, that it should be your to lay waste fortified cities into ruinous heaps.

Ndiyo sababu wenyeji wao wakawa hawana nguvu, na kufadhaika, na kuhangaika, wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, kama shamba la ngano kabla haijaiva. Isaya 37:27

Therefore their inhabitants were of small power, they were dismayed and confounded; they were as the grass of the field, and as the green herb, as the grass on the housetops, and as a field [of grain] before it is grown up.

Lakini nakujua, kuketi kwako, na kutoka kwako, na kuingia kwako; na ghadhabu yako uliyonighadhibikia. Isaya 37:28

But I know your sitting down, and your going out, and your coming in, and your raging against me.

Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu, nitatia kulabu yangu katika pua yako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha kwa njia ile ile uliyoijia. Isaya 37:29

Because of your raging against me, and because your arrogance is come up into my ears, therefore will I put my hook in your nose, and my bridle in your lips, and I will turn you back by the way by which you came.

Na kwako wewe dalili ndiyo hii; mwaka huu mtakula vitu vimeavyo vyenyewe; na mwaka wa pili mtakula mazao ya mbegu za vitu hivyo; na mwaka wa tatu pandeni mbegu, kavuneni; mkapande mizabibu katika mashamba, mkale matunda yake. Isaya 37:30

This shall be the sign to you: you shall eat this year that which grows of itself, and in the second year that which springs of the same; and in the third year sow you, and reap, and plant vineyards, and eat the fruit of it.

Na mabaki yaliyookoka, yaliyobakia ya nyumba ya Yuda, yatatia mizizi chini, na kuzaa matunda juu. Isaya 37:31

The remnant that is escaped of the house of Judah shall again take root downward, and bear fruit upward.

Maana katika Yerusalemu yatatoka mabaki, nao watakaookoka katika mlima Sayuni; wivu wa Bwana wa majeshi utatimiza mambo hayo. Isaya 37:32

For out of Jerusalem shall go forth a remnant, and out of Mount Zion those who shall escape. The zeal of Yahweh of Hosts will perform this.

Basi, Bwana asema hivi katika habari za mfalme wa Ashuru, Yeye hataingia ndani ya mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake. Isaya 37:33

Therefore thus says Yahweh concerning the king of Assyria, He shall not come to this city, nor shoot an arrow there, neither shall he come before it with shield, nor cast up a mound against it.

Njia ile ile aliyoijia, kwa njia hiyo atarudi zake, wala hataingia ndani ya mji huu; asema Bwana. Isaya 37:34

By the way that he came, by the same shall he return, and he shall not come to this city, says Yahweh.

Nami nitaulinda mji huu, niuokoe kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu. Isaya 37:35

For I will defend this city to save it, for my own sake, and for my servant David's sake.

Basi malaika wa Bwana alitoka, akaua watu mia na themanini na tano elfu katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia. Isaya 37:36

The angel of Yahweh went forth, and struck in the camp of the Assyrians one hundred and eighty-five thousand; and when men arose early in the morning, behold, these were all dead bodies.

Basi Senakeribu, mfalme wa Ashuru akaenda zake, akarudi Ninawi, akakaa huko. Isaya 37:37

So Sennacherib king of Assyria departed, and went and returned, and lived at Nineveh.

Ikawa alipokuwa akiabudu katika nyumba ya Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza, wanawe, wakampiga kwa upanga; wakakimbilia nchi ya Ararati; naye Esar-hadoni, mwanawe, akamiliki badala yake. Isaya 37:38

It happened, as he was worshipping in the house of Nisroch his god, that Adrammelech and Sharezer his sons struck him with the sword; and they escaped into the land of Ararat. Esar Haddon his son reigned in his place.