Isaya 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 20 (Swahili) Isaiah 20 (English)

Katika mwaka ule jemadari Yule alipofika Ashdodi,alipotumwa na Sargoni mfalme wa Ashuru;naye alipigana na Ashdodi akautwaa. Isaya 20:1

In the year that Tartan came to Ashdod, when Sargon the king of Assyria sent him, and he fought against Ashdod and took it;

wakati huo Bwana alinena kwa kinywa cha Isaya, mwana wa Amozi, akisema, Haya, uvue nguo ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako miguuni mwako. Isaya 20:2

at that time Yahweh spoke by Isaiah the son of Amoz, saying, Go, and loose the sackcloth from off your loins, and put your shoe from off your foot. He did so, walking naked and barefoot.

Naye akafanya hivyo akaenda uchi, miguu yake haina viatu. Bwana akasema, Kama vile mtumishi wangu Isaya anavyokwenda uchi, hana viatu, awe ishara na ajabu kwa muda wa miaka mitatu juu ya Misri na juu ya Kushi; Isaya 20:3

Yahweh said, Like as my servant Isaiah has walked naked and barefoot three years for a sign and a wonder concerning Egypt and concerning Ethiopia;

vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, hawana viatu, matako yao wazi, Misri iaibishwe. Isaya 20:4

so shall the king of Assyria lead away the captives of Egypt, and the exiles of Ethiopia, young and old, naked and barefoot, and with buttocks uncovered, to the shame of Egypt.

Nao watafadhaika, na kuona haya kwa ajili ya Kushi, matumaini yao, na Misri, utukufu wao. Isaya 20:5

They shall be dismayed and confounded, because of Ethiopia their expectation, and of Egypt their glory.

Na mwenyeji wa nchi ya pwani atasema katika siku hiyo, Angalia, haya ndiyo yaliyowapata watu wale tuliowatumaini, ambao tuliwakimbilia watuokoe na mfalme wa Ashuru; na sisi je! Twawezaje kupona? Isaya 20:6

The inhabitant of this coast-land shall say in that day, Behold, such is our expectation, where we fled for help to be delivered from the king of Assyria: and we, how shall we escape?