Isaya 57 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 57 (Swahili) Isaiah 57 (English)

Mwenye haki hupotea, wala hakuna atiaye hayo moyoni; na watu watauwa huondolewa, wala hakuna afikiriye ya kuwa mwenye haki ameondolewa asipatikane na mabaya. Isaya 57:1

The righteous perishes, and no man lays it to heart; and merciful men are taken away, none considering that the righteous is taken away from the evil [to come].

Yeye huingia katika amani; wao hustarehe katika vitanda vyao, kila mtu aendaye katika unyofu wake. Isaya 57:2

He enters into peace; they rest in their beds, each one who walks in his uprightness.

Lakini ninyi karibuni hapa, enyi wana wa mwanamke mchawi, uzao wa mzinzi na kahaba. Isaya 57:3

But draw near here, you sons of the sorceress, the seed of the adulterer and the prostitute.

Mnafanya dhihaka yenu juu ya nani? Mmepanua vinywa vyenu, na kutoa ndimi zenu? Je, ninyi si wana wa uasi, uzao wa uongo; Isaya 57:4

Against whom do you sport yourselves? against whom make you a wide mouth, and put out the tongue? Aren't you children of disobedience, a seed of falsehood,

ninyi mnaowasha tamaa zenu kati ya mialoni, chini ya kila mti wenye majani mabichi; ninyi mnaoua watoto mabondeni, chini ya mianya ya majabali? Isaya 57:5

you who inflame yourselves among the oaks, under every green tree; who kill the children in the valleys, under the clefts of the rocks?

Sehemu yako i katika makokoto ya bonde; hayo ndiyo kura yako; umeyamwagia hayo sadaka ya kinywaji, umeyatolea sadaka ya unga; je! Niwe radhi na mambo hayo? Isaya 57:6

Among the smooth [stones] of the valley is your portion; they, they are your lot; even to them have you poured a drink-offering, you have offered an offering. Shall I be appeased for these things?

Umeweka kitanda chako juu ya mlima mrefu ulioinuka sana; ukaenda huko ili kutoa dhabihu. Isaya 57:7

On a high and lofty mountain have you set your bed; there also you went up to offer sacrifice.

Na nyuma ya milango na miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua nafsi yako kwa ajili ya mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua kitanda chako, nawe umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo ulipokiona. Isaya 57:8

Behind the doors and the posts have you set up your memorial: for you have uncovered [yourself] to another than me, and are gone up; you have enlarged your bed, and made you a covenant with them: you loved their bed where you saw it.

Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hata kuzimu. Isaya 57:9

You went to the king with oil, and did increase your perfumes, and did send your ambassadors far off, and did debase yourself even to Sheol.

Ulikuwa umechoka kwa ajili ya urefu wa njia yako; lakini hukusema, Hapana matumaini; ulipata kuhuishwa nguvu zako; kwa sababu hiyo hukuugua. Isaya 57:10

You were wearied with the length of your way; yet you didn't say, It is in vain: you found a reviving of your strength; therefore you weren't faint.

Tena ni nani uliyemwogopa na kumhofu, hata ukasema uongo, wala hukunikumbuka mimi, wala kuweka hayo moyoni? Je! Mimi sikunyamaza tangu zamani, hata huniogopi? Isaya 57:11

Of whom have you been afraid and in fear, that you lie, and have not remembered me, nor laid it to your heart? Haven't I held my peace even of long time, and you don't fear me?

Mimi nitatangaza haki yako, na matendo yako hayatakufaa. Isaya 57:12

I will declare your righteousness; and as for your works, they shall not profit you.

Utakapolia, na wakuponye hao uliowakusanya; lakini upepo utawachukua; uvuvio tu utawachukulia mbali; lakini yeye anayenitumaini ataimiliki nchi, na kuurithi mlima wangu mtakatifu. Isaya 57:13

When you cry, let those who you have gathered deliver you; but the wind shall take them, a breath shall carry them all away: but he who takes refuge in me shall possess the land, and shall inherit my holy mountain.

Naye atasema, Tutieni, tutieni, Itengenezeni njia, Kiondoeni kila kikwazacho Katika njia ya watu wangu. Isaya 57:14

He will say, Cast up, cast up, prepare the way, take up the stumbling-block out of the way of my people.

Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu. Isaya 57:15

For thus says the high and lofty One who inhabits eternity, whose name is Holy: I dwell in the high and holy place, with him also who is of a contrite and humble spirit, to revive the spirit of the humble, and to revive the heart of the contrite.

Kwa kuwa sitashindana na watu siku zote, wala sitakuwa na hasira siku zote; maana roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi nilizozifanya. Isaya 57:16

For I will not contend forever, neither will I be always angry; for the spirit would faint before me, and the souls who I have made.

Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake naliona hasira, nikampiga; nalificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe. Isaya 57:17

For the iniquity of his covetousness was I angry, and struck him; I hid [my face] and was angry; and he went on backsliding in the way of his heart.

Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia. Isaya 57:18

I have seen his ways, and will heal him: I will lead him also, and restore comforts to him and to his mourners.

Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema Bwana; nami nitamponya. Isaya 57:19

I create the fruit of the lips: Peace, peace, to him who is far off and to him who is near, says Yahweh; and I will heal him.

Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka. Isaya 57:20

But the wicked are like the troubled sea; for it can't rest, and its waters cast up mire and dirt.

Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu. Isaya 57:21

There is no peace, says my God, to the wicked.