Isaya 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 7 (Swahili) Isaiah 7 (English)

Hata ikawa katika siku za Ahazi, mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, Resini, mfalme wa Shamu, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakapanda wakaenda Yerusalemu ili kupigana nao, lakini hawakuweza kuushinda. Isaya 7:1

It happened in the days of Ahaz the son of Jotham, the son of Uzziah, king of Judah, that Rezin the king of Syria, and Pekah the son of Remaliah, king of Israel, went up to Jerusalem to war against it, but could not prevail against it.

Kisha watu wa nyumba ya Daudi wakaambiwa kwamba Shamu wamefanya mapatano na Efraimu. Na moyo wake ukataharuki, na moyo wa watu wake, kama miti ya mwituni itikiswavyo na upepo. Isaya 7:2

It was told the house of David, saying, "Syria is allied with Ephraim." His heart trembled, and the heart of his people, as the trees of the forest tremble with the wind.

Basi Bwana akamwambia Isaya, Haya, toka, umlaki Ahazi, wewe na Shear-yashubu mwana wako, huko mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja wa dobi; Isaya 7:3

Then Yahweh said to Isaiah, "Go out now to meet Ahaz, you, and Shearjashub your son, at the end of the conduit of the upper pool, on the highway of the fuller's field.

ukamwambie, Angalia, ukatulie; usiogope wala usife moyo, kwa sababu ya mikia hii miwili ya vinga hivi vitokavyo moshi; kwa sababu ya hasira kali ya Resini na Shamu, na mwana wa Remalia. Isaya 7:4

Tell him, 'Be careful, and keep calm. Don't be afraid, neither let your heart be faint because of these two tails of smoking firebrands, for the fierce anger of Rezin and Syria, and of the son of Remaliah.

Kwa kuwa Shamu amekusudia mabaya juu yako, pamoja na Efraimu na mwana wa Remalia, wakisema, Isaya 7:5

Because Syria, Ephraim, and the son of Remaliah, have plotted evil against you, saying,

Haya, na tupande ili kupigana na Yuda na kuwasumbua, tukabomoe mahali tupate kuingia, na kummilikisha mfalme ndani yake, huyo mwana wa Tabeeli. Isaya 7:6

"Let's go up against Judah, and tear it apart, and let's divide it among ourselves, and set up a king in the midst of it, even the son of Tabeel."

Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa. Isaya 7:7

This is what the Lord Yahweh says: "It shall not stand, neither shall it happen."

Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila ya watu tena; Isaya 7:8

For the head of Syria is Damascus, and the head of Damascus is Rezin; and within sixty-five years Ephraim shall be broken in pieces, so that it shall not be a people;

tena kichwa cha Efraimu ni Samaria, na kichwa cha Samaria ni mwana wa Remalia. Kwamba hamtaki kusadiki, bila shaka hamtathibitika. Isaya 7:9

and the head of Ephraim is Samaria, and the head of Samaria is Remaliah's son. If you will not believe, surely you shall not be established.'"

Tena Bwana akasema na Ahazi akinena, Isaya 7:10

Yahweh spoke again to Ahaz, saying,

Jitakie ishara ya Bwana, Mungu wako; itake katika mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana. Isaya 7:11

"Ask a sign of Yahweh your God; ask it either in the depth, or in the height above."

Lakini Ahazi akasema, Sitaitaka, wala sitamjaribu Bwana. Isaya 7:12

But Ahaz said, "I will not ask, neither will I tempt Yahweh."

Naye akasema, Sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia? Isaya 7:13

He said, "Listen now, house of David: Is it not enough for you to try the patience of men, that you will try the patience of my God also?

Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. Isaya 7:14

Therefore the Lord himself will give you a sign. Behold, the virgin will conceive, and bear a son, and shall call his name Immanuel.{"Immanuel" means "God with us."}

Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema. Isaya 7:15

He shall eat butter and honey when he knows to refuse the evil, and choose the good.

Kwa maana kabla mtoto huyo hajajua kuyakataa mabaya na kuyachagua mema, nchi ile, ambayo wewe unawachukia wafalme wake wawili, itaachwa ukiwa. Isaya 7:16

For before the child knows to refuse the evil, and choose the good, the land whose two kings you abhor shall be forsaken.

Bwana ataleta juu yako, na juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako, siku zisizokuja bado, tangu siku ile aliyoondoka Efraimu kutoka katika Yuda; yaani, mfalme wa Ashuru. Isaya 7:17

Yahweh will bring on you, on your people, and on your father's house, days that have not come, from the day that Ephraim departed from Judah; even the king of Assyria.

Tena itakuwa katika siku hiyo Bwana atampigia kelele inzi aliye katika pande za mwisho za mito ya Misri, na nyuki aliye katika nchi ya Ashuru Isaya 7:18

It will happen in that day that Yahweh will whistle for the fly that is in the uttermost part of the rivers of Egypt, and for the bee that is in the land of Assyria.

Nao watakuja na kutulia katika mabonde yaliyo ukiwa, na katika pango za majabali, na juu ya michongoma yote, na juu ya malisho yote. Isaya 7:19

They shall come, and shall all rest in the desolate valleys, in the clefts of the rocks, on all thorn-hedges, and on all pastures.

Katika siku hiyo Bwana atanyoa kichwa na malaika ya miguuni, kwa wembe ulioajiriwa pande za ng'ambo ya Mto, yaani, kwa mfalme wa Ashuru, nao utazimaliza ndevu nazo. Isaya 7:20

In that day the Lord will shave with a razor that is hired in the parts beyond the River, even with the king of Assyria, the head and the hair of the feet; and it shall also consume the beard.

Katika siku hiyo itakuwa ya kwamba mtu atalisha ng'ombe mke mchanga na kondoo wake wawili; Isaya 7:21

It shall happen in that day that a man shall keep alive a young cow, and two sheep;

kisha itakuwa, kwa sababu wanyama hao watatoa maziwa mengi, atakula siagi; kwa maana kila mtu aliyesalia katika nchi hii atakula siagi na asali. Isaya 7:22

and it shall happen, that because of the abundance of milk which they shall give he shall eat butter: for everyone will eat butter and honey that is left in the midst of the land.

Tena itakuwa katika siku hiyo kila mahali palipokuwa na mizabibu elfu, iliyopata fedha elfu, patakuwa mahali pa mbigili na miiba tu. Isaya 7:23

It will happen in that day that every place where there were a thousand vines at a thousand silver shekels, shall be for briers and thorns.

Mtu atakayekwenda huko atakwenda na mishale na upinde; kwa sababu nchi yote itakuwa ina mibigili na miiba. Isaya 7:24

People will go there with arrows and with bow, because all the land will be briers and thorns.

Na vilima vyote vilivyolimwa kwa jembe, hutafika huko kwa sababu ya kuiogopa mibigili na miiba, lakini hapo patakuwa mahali pa kupeleka ng'ombe, mahali pa kukanyagwa na kondoo. Isaya 7:25

All the hills that were cultivated with the hoe, you shall not come there for fear of briers and thorns; but it shall be for the sending forth of oxen, and for the treading of sheep."