Isaya 43 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 43 (Swahili) Isaiah 43 (English)

Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Isaya 43:1

But now thus says Yahweh who created you, Jacob, and he who formed you, Israel: Don't be afraid, for I have redeemed you; I have called you by your name, you are mine.

Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Isaya 43:2

When you pass through the waters, I will be with you; and through the rivers, they shall not overflow you: when you walk through the fire, you shall not be burned, neither shall the flame kindle on you.

Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. Isaya 43:3

For I am Yahweh your God, the Holy One of Israel, your Savior; I have given Egypt as your ransom, Ethiopia and Seba in your place.

Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako. Isaya 43:4

Since you have been precious in my sight, [and] honorable, and I have loved you; therefore will I give men in your place, and peoples instead of your life.

Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi; Isaya 43:5

Don't be afraid; for I am with you: I will bring your seed from the east, and gather you from the west;

nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia. Isaya 43:6

I will tell the north, Give up; and to the south, Don't keep back; bring my sons from far, and my daughters from the end of the earth;

Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya. Isaya 43:7

everyone who is called by my name, and whom I have created for my glory, whom I have formed, yes, whom I have made.

Walete vipofu walio na macho, na viziwi walio na masikio. Isaya 43:8

Bring forth the blind people who have eyes, and the deaf who have ears.

Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonyesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli. Isaya 43:9

Let all the nations be gathered together, and let the peoples be assembled: who among them can declare this, and show us former things? let them bring their witnesses, that they may be justified; or let them hear, and say, It is truth.

Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Isaya 43:10

You are my witnesses, says Yahweh, and my servant whom I have chosen; that you may know and believe me, and understand that I am he: before me there was no God formed, neither shall there be after me.

Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu mimi hapana mwokozi. Isaya 43:11

I, even I, am Yahweh; and besides me there is no savior.

Nimetangaza habari, nimeokoa, nimeonyesha, na hapakuwa mungu wa kigeni kati yenu; kwa sababu hiyo ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, nami ni Mungu. Isaya 43:12

I have declared, and I have saved, and I have shown; and there was no strange [god] among you: therefore you are my witnesses, says Yahweh, and I am God.

Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia? Isaya 43:13

Yes, since the day was I am he; and there is none who can deliver out of my hand: I will work, and who can hinder it?

Bwana, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Kwa ajili yenu nimetuma ujumbe Babeli nami nitawashusha wote mfano wa wakimbizi, naam, Wakaldayo, katika merikebu zao walizozifurahia. Isaya 43:14

Thus says Yahweh, your Redeemer, the Holy One of Israel: For your sake I have sent to Babylon, and I will bring down all of them as fugitives, even the Chaldeans, in the ships of their rejoicing.

Mimi ni Bwana, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu. Isaya 43:15

I am Yahweh, your Holy One, the Creator of Israel, your King.

Bwana asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu; Isaya 43:16

Thus says Yahweh, who makes a way in the sea, and a path in the mighty waters;

atoaye gari na farasi, jeshi la askari na uwezo; wamelala, hawataondoka; wametoweka, wamezimwa mfano wa utambi. Isaya 43:17

who brings forth the chariot and horse, the army and the mighty man (they lie down together, they shall not rise; they are extinct, they are quenched as a wick):

Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Isaya 43:18

Don't remember the former things, neither consider the things of old.

Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. Isaya 43:19

Behold, I will do a new thing; now shall it spring forth; shall you not know it? I will even make a way in the wilderness, and rivers in the desert.

Wanyama wa kondeni wataniheshimu, mbweha pia na mbuni; kwa sababu nimewapa maji jangwani, na mito nyikani, ili kuwanywesha watu wangu, wateule wangu; Isaya 43:20

The animals of the field shall honor me, the jackals and the ostriches; because I give waters in the wilderness, and rivers in the desert, to give drink to my people, my chosen,

watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu. Isaya 43:21

the people which I formed for myself, that they might set forth my praise.

Lakini hukuniita, Ee Yakobo, bali umechoka nami, Ee Israeli. Isaya 43:22

Yet you have not called on me, Jacob; but you have been weary of me, Israel.

Hukuniletea wana-kondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani. Isaya 43:23

You have not brought me of your sheep for burnt offerings; neither have you honored me with your sacrifices. I have not burdened you with offerings, nor wearied you with frankincense.

Hukuninunulia manukato kwa fedha, wala hukunishibisha kwa mafuta ya sadaka zako; bali umenitumikisha kwa dhambi zako, umenichosha kwa maovu yako. Isaya 43:24

You have bought me no sweet cane with money, neither have you filled me with the fat of your sacrifices; but you have burdened me with your sins, you have wearied me with your iniquities.

Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. Isaya 43:25

I, even I, am he who blots out your transgressions for my own sake; and I will not remember your sins.

Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. Isaya 43:26

Put me in remembrance; let us plead together: set you forth [your cause], that you may be justified.

Baba yako wa kwanza alifanya dhambi, na wakalimani wako wameniasi. Isaya 43:27

Your first father sinned, and your teachers have transgressed against me.

Kwa hiyo nitawatia unajisi wakuu wa patakatifu, nami nitamfanya Yakobo kuwalaani, na Israeli kuwa tukano. Isaya 43:28

Therefore I will profane the princes of the sanctuary; and I will make Jacob a curse, and Israel a reviling.