Kumbukumbu la Torati 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 1 (Swahili) Deuteronomy 1 (English)

Haya ndiyo maneno Musa aliyowaambia Israeli wote ng'ambo ya Yordani barani, katika Araba lililoelekea Sufu, kati ya Parani, na Tofeli, na Labani, na Hazerothi, na Dizahabu. Kumbukumbu la Torati 1:1

These are the words which Moses spoke to all Israel beyond the Jordan in the wilderness, in the Arabah over against Suph, between Paran, and Tophel, and Laban, and Hazeroth, and Dizahab.

Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya mlima wa Seiri mpaka Kadesh-barnea. Kumbukumbu la Torati 1:2

It is eleven days' [journey] from Horeb by the way of Mount Seir to Kadesh-barnea.

Ikawa mwaka wa arobaini, mwezi wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, Musa akawaambia wana wa Israeli kama yote aliyopewa na Bwana ya kuwaamuru; Kumbukumbu la Torati 1:3

It happened in the fortieth year, in the eleventh month, on the first day of the month, that Moses spoke to the children of Israel, according to all that Yahweh had given him in commandment to them;

alipokwisha kumpiga Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa akikaa Ashtarothi iliyo katika Edrei; Kumbukumbu la Torati 1:4

after he had struck Sihon the king of the Amorites, who lived in Heshbon, and Og the king of Bashan, who lived in Ashtaroth, at Edrei.

ni ng'ambo ya Yordani katika nchi ya Moabu, alipoanza Musa kufunua torati hii, akisema, Kumbukumbu la Torati 1:5

Beyond the Jordan, in the land of Moab, began Moses to declare this law, saying,

Bwana, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu vyatosha; Kumbukumbu la Torati 1:6

Yahweh our God spoke to us in Horeb, saying, You have lived long enough in this mountain:

geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima-vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani-pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati. Kumbukumbu la Torati 1:7

turn you, and take your journey, and go to the hill-country of the Amorites, and to all [the places] near thereunto, in the Arabah, in the hill-country, and in the lowland, and in the South, and by the sea-shore, the land of the Canaanites, and Lebanon, as far as the great river, the river Euphrates.

Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi Bwana aliyowaapia baba zenu, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao. Kumbukumbu la Torati 1:8

Behold, I have set the land before you: go in and possess the land which Yahweh swore to your fathers, to Abraham, to Isaac, and to Jacob, to give to them and to their seed after them.

Nami wakati ule niliwaambia, nikasema, Siwezi mimi mwenyewe kuwachukua peke yangu. Kumbukumbu la Torati 1:9

I spoke to you at that time, saying, I am not able to bear you myself alone:

Bwana, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi. Kumbukumbu la Torati 1:10

Yahweh your God has multiplied you, and, behold, you are this day as the stars of the sky for multitude.

Bwana, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabarikia, kama alivyowaahidi. Kumbukumbu la Torati 1:11

Yahweh, the God of your fathers, make you a thousand times as many as you are, and bless you, as he has promised you!

Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu, na mzigo wenu, na mateto yenu? Kumbukumbu la Torati 1:12

How can I myself alone bear your encumbrance, and your burden, and your strife?

Jitwalieni watu wenye akili na fahamu, watu wanaojulikana, kwa kadiri ya kabila zenu, nami nitawafanya wawe vichwa juu yenu. Kumbukumbu la Torati 1:13

Take wise men of understanding and well known according to your tribes, and I will make them heads over you.

Nanyi mkanijibu, mkaniambia, Jambo ulilonena ni jema la kufanya. Kumbukumbu la Torati 1:14

You answered me, and said, The thing which you have spoken is good [for us] to do.

Basi nikatwaa vichwa vya kabila zenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe vichwa juu yenu, maakida ya elfu elfu, na maakida ya mia mia, na maakida ya hamsini hamsini, na maakida ya kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya kabila zenu. Kumbukumbu la Torati 1:15

So I took the heads of your tribes, wise men, and known, and made them heads over you, captains of thousands, and captains of hundreds, and captains of fifties, and captains of tens, and officers, according to your tribes.

Nikawaagiza wakati ule waamuzi wenu, nikawaambia, Sikizeni ninyi maneno kati ya ndugu zenu, mkaamue kwa haki kati ya mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye. Kumbukumbu la Torati 1:16

I charged your judges at that time, saying, Hear [the causes] between your brothers, and judge righteously between a man and his brother, and the foreigner who is living with him.

Msitazame nafsi za watu katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu awaye yote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza. Kumbukumbu la Torati 1:17

You shall not show partiality in judgment; you shall hear the small and the great alike; you shall not be afraid of the face of man; for the judgment is God's: and the cause that is too hard for you, you shall bring to me, and I will hear it.

Nikawaamuru wakati huo mambo yote yaliyowapasa ninyi kuyafanya. Kumbukumbu la Torati 1:18

I commanded you at that time all the things which you should do.

Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama Bwana, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea. Kumbukumbu la Torati 1:19

We traveled from Horeb, and went through all that great and terrible wilderness which you saw, by the way to the hill-country of the Amorites, as Yahweh our God commanded us; and we came to Kadesh-barnea.

Nami nikawaambia, Mmefika nchi ya vilima ya Waamori, anayotupa sisi Bwana, Mungu wetu. Kumbukumbu la Torati 1:20

I said to you, You are come to the hill-country of the Amorites, which Yahweh our God gives to us.

Tazama, Bwana, Mungu wako, ameiweka nchi mbele yako; haya panda, itamalaki, kama Bwana, Mungu wa baba zako, alivyokuambia; usiogope wala usifadhaike. Kumbukumbu la Torati 1:21

Behold, Yahweh your God has set the land before you: go up, take possession, as Yahweh, the God of your fathers, has spoken to you; don't be afraid, neither be dismayed.

Nanyi mkanikaribia kila mmoja wenu, mkasema, Na tupeleke watu mbele yetu, ili watupelelezee nchi na kutuletea habari za njia itupasayo kuipandia, na za miji tutakayoifikia. Kumbukumbu la Torati 1:22

You came near to me everyone of you, and said, Let us send men before us, that they may search the land for us, and bring us word again of the way by which we must go up, and the cities to which we shall come.

Neno hili likanipendeza sana; nikatwaa watu kumi na wawili, mtu mmoja wa kila kabila. Kumbukumbu la Torati 1:23

The thing pleased me well; and I took twelve men of you, one man for every tribe:

Nao wakageuka, wakapanda mlimani wakafika bonde la Eshkoli, wakalipeleleza. Kumbukumbu la Torati 1:24

and they turned and went up into the hill-country, and came to the valley of Eshcol, and spied it out.

Wakatwaa baadhi ya matunda ya nchi ile mikononi mwao, wakatuletea huku chini, wakatuletea habari tena, wakasema, Nchi hii anayotupa Bwana, Mungu wetu, ni nchi njema. Kumbukumbu la Torati 1:25

They took of the fruit of the land in their hands, and brought it down to us, and brought us word again, and said, It is a good land which Yahweh our God gives to us.

Lakini hamkukubali kukwea huko, mlihalifu neno la Bwana, Mungu wenu; Kumbukumbu la Torati 1:26

Yet you wouldn't go up, but rebelled against the commandment of Yahweh your God:

mkanung'unika hemani mwenu, mkasema, Ni kwa sababu Bwana ametuchukia, ndipo akatutoa katika nchi ya Misri, apate kututia katika mikono ya Waamori, ili kutuangamiza. Kumbukumbu la Torati 1:27

and you murmured in your tents, and said, Because Yahweh hated us, he has brought us forth out of the land of Egypt, to deliver us into the hand of the Amorites, to destroy us.

Twakwea kwenda wapi? Ndugu zetu wameiyeyusha mioyo yetu, wakituambia, Wale watu ni wengi, ni warefu kuliko sisi; miji nayo ni mikubwa, imejengewa kuta hata mbinguni; na zaidi ya hayo huko tumewaona Waanaki. Kumbukumbu la Torati 1:28

Where are we going up? our brothers have made our heart to melt, saying, The people are greater and taller than we; the cities are great and fortified up to the sky; and moreover we have seen the sons of the Anakim there.

Ndipo nikawaambieni, Msifanye hofu, wala msiwache. Kumbukumbu la Torati 1:29

Then I said to you, Don't dread, neither be afraid of them.

Bwana, Mungu wenu, anayetangulia mbele yenu, ndiye atakayewapigania, kwa mfano wa yote aliyowafanyia huko Misri mbele ya macho yenu; Kumbukumbu la Torati 1:30

Yahweh your God who goes before you, he will fight for you, according to all that he did for you in Egypt before your eyes,

na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua Bwana, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafikilia mahali hapa. Kumbukumbu la Torati 1:31

and in the wilderness, where you have seen how that Yahweh your God bore you, as a man does bear his son, in all the way that you went, until you came to this place.

Lakini katika jambo hili hamkumwamini Bwana, Mungu wenu, Kumbukumbu la Torati 1:32

Yet in this thing you didn't believe Yahweh your God,

aliyewatangulia njiani, usiku kwa moto, kuwaonyesha njia mtakayoiendea, na mchana kwa hilo wingu, ili apate kuwatafutia mahali pa kusimamisha hema zenu. Kumbukumbu la Torati 1:33

who went before you in the way, to seek you out a place to pitch your tents in, in fire by night, to show you by what way you should go, and in the cloud by day.

Bwana akaisikia sauti ya maneno yenu, akaghadhibika, akaapa, akasema, Kumbukumbu la Torati 1:34

Yahweh heard the voice of your words, and was angry, and swore, saying,

Hakika yangu hapana mmoja miongoni mwa watu hawa wa kizazi hiki kibaya atakayeiona nchi hiyo nzuri, niliyowaapia baba zenu kuwapa, Kumbukumbu la Torati 1:35

Surely there shall not one of these men of this evil generation see the good land, which I swore to give to your fathers,

isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, huyo ataiona; nami nitampa yeye na watoto wake nchi hiyo aliyoikanyaga; kwa kuwa amemfuata Bwana kwa kila neno. Kumbukumbu la Torati 1:36

save Caleb the son of Jephunneh: he shall see it; and to him will I give the land that he has trodden on, and to his children, because he has wholly followed Yahweh.

Na Bwana alinikasirikia mimi kwa ajili yenu, akasema, Wala wewe hutaingia humo; Kumbukumbu la Torati 1:37

Also Yahweh was angry with me for your sakes, saying, You also shall not go in there:

Yoshua mwana wa Nuni asimamaye mbele yako ndiye atakayeingia; mtie moyo; kwa kuwa yeye atawarithisha Israeli. Kumbukumbu la Torati 1:38

Joshua the son of Nun, who stands before you, he shall go in there: encourage you him; for he shall cause Israel to inherit it.

Tena, wadogo wenu, mliosema watakuwa mateka, na wana wenu, wasiokuwa leo na maarifa ya mabaya wala mema, ndio watakaoingia, nao ndio nitakaowapa, nao wataimiliki. Kumbukumbu la Torati 1:39

Moreover your little ones, whom you said should be a prey, and your children, who this day have no knowledge of good or evil, they shall go in there, and to them will I give it, and they shall possess it.

Na ninyi basi geukeni, mshike safari yenu, mwende jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu. Kumbukumbu la Torati 1:40

But as for you, turn you, and take your journey into the wilderness by the way to the Red Sea.

Ndipo mkanijibu, mkaniambia, Sisi tumefanya dhambi juu ya Bwana, tutakwea kupigana kwa mfano wa yote tuliyoamriwa na Bwana. Mkajifunga kila mtu silaha zake za vita, mkafanya wepesi kukwea mlimani. Kumbukumbu la Torati 1:41

Then you answered and said to me, We have sinned against Yahweh, we will go up and fight, according to all that Yahweh our God commanded us. You girded on every man his weapons of war, and were forward to go up into the hill-country.

Bwana akaniambia, Uwaambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi si kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu. Kumbukumbu la Torati 1:42

Yahweh said to me, Tell them, Don't go up, neither fight; for I am not among you; lest you be struck before your enemies.

Basi niliwaambia, msinisikize, bali mliasi amri ya Bwana, mkajikinai, na kukwea mlimani. Kumbukumbu la Torati 1:43

So I spoke to you, and you didn't listen; but you rebelled against the commandment of Yahweh, and were presumptuous, and went up into the hill-country.

Na Waamori waliokuwa wakikaa katika mlima huo, waliwatokea juu yenu, wakawafukuza, kama wafukuzwao na nyuki, wakawapomoshea Seiri mpaka Horma. Kumbukumbu la Torati 1:44

The Amorites, who lived in that hill-country, came out against you, and chased you, as bees do, and beat you down in Seir, even to Hormah.

Mkarudi mkalia mbele za Bwana; Bwana asiisikize sauti yenu, wala hakuelekeza masikio yake kwenu. Kumbukumbu la Torati 1:45

You returned and wept before Yahweh; but Yahweh didn't listen to your voice, nor gave ear to you.

Ndipo mkakaa Kadeshi siku nyingi, kwa kadiri ya hizo siku mlizokaa. Kumbukumbu la Torati 1:46

So you abode in Kadesh many days, according to the days that you abode [there].