Kumbukumbu la Torati 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 17 (Swahili) Deuteronomy 17 (English)

Usimchinjie Bwana, Mungu wako, ng'ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako. Kumbukumbu la Torati 17:1

You shall not sacrifice to Yahweh your God an ox, or a sheep, in which is a blemish, [or] anything evil; for that is an abomination to Yahweh your God.

Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake, Kumbukumbu la Torati 17:2

If there be found in the midst of you, within any of your gates which Yahweh your God gives you, man or woman, who does that which is evil in the sight of Yahweh your God, in transgressing his covenant,

naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi; Kumbukumbu la Torati 17:3

and has gone and served other gods, and worshiped them, or the sun, or the moon, or any of the host of the sky, which I have not commanded;

ukiambiwa hayo nawe umeyasikia, ndipo utafute kwa bidii, na tazama, ikiwa ni kweli lina hakika jambo lile, kuwa yafanywa machukizo kama hayo katika Israeli; Kumbukumbu la Torati 17:4

and it be told you, and you have heard of it, then shall you inquire diligently; and, behold, if it be true, and the thing certain, that such abomination is done in Israel,

ndipo umchukue nje malangoni kwako, yule mtu mume, au yule mwanamke, aliyefanya jambo lile ovu; ukawapige kwa mawe, wafe. Kumbukumbu la Torati 17:5

then shall you bring forth that man or that woman, who has done this evil thing, to your gates, even the man or the woman; and you shall stone them to death with stones.

Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili, au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja. Kumbukumbu la Torati 17:6

At the mouth of two witnesses, or three witnesses, shall he who is to die be put to death; at the mouth of one witness he shall not be put to death.

Mikono ya wale mashahidi na iwe juu yake kwanza kwa kumwua, kisha mikono ya watu wote. Uondoe vivyo uovu katikati yako. Kumbukumbu la Torati 17:7

The hand of the witnesses shall be first on him to put him to death, and afterward the hand of all the people. So you shall put away the evil from the midst of you.

Ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya daawa na daawa, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; Kumbukumbu la Torati 17:8

If there arise a matter too hard for you in judgment, between blood and blood, between plea and plea, and between stroke and stroke, being matters of controversy within your gates; then shall you arise, and go up to the place which Yahweh your God shall choose;

uwaendee makuhani Walawi, na mwamuzi atakayekuwako siku hizo; uwaulize; nao watakuonyesha hukumu ya maamuzi; Kumbukumbu la Torati 17:9

and you shall come to the priests the Levites, and to the judge who shall be in those days: and you shall inquire; and they shall show you the sentence of judgment.

nawe fanya sawasawa na hukumu watakayokuonyesha mahali hapo atakapochagua Bwana; nawe tunza kufanya kwa mfano wa yote watakayokufunza; Kumbukumbu la Torati 17:10

You shall do according to the tenor of the sentence which they shall show you from that place which Yahweh shall choose; and you shall observe to do according to all that they shall teach you:

kwa mfano wa sheria watakayokufunza, na kwa mfano wa hukumu watakayokuambia, fanya vivyo; usigeuke katika hukumu watakayokuonyesha, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto. Kumbukumbu la Torati 17:11

according to the tenor of the law which they shall teach you, and according to the judgment which they shall tell you, you shall do; you shall not turn aside from the sentence which they shall show you, to the right hand, nor to the left.

Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia Bwana, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli. Kumbukumbu la Torati 17:12

The man who does presumptuously, in not listening to the priest who stands to minister there before Yahweh your God, or to the judge, even that man shall die: and you shall put away the evil from Israel.

Na hao watu wote watasikia na kuogopa, wasifanye tena kwa kujikinai. Kumbukumbu la Torati 17:13

All the people shall hear, and fear, and do no more presumptuously.

Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, Nitaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kando-kando yangu; Kumbukumbu la Torati 17:14

When you are come to the land which Yahweh your God gives you, and shall possess it, and shall dwell therein, and shall say, I will set a king over me, like all the nations that are round about me;

usiache kumweka yule atakayechaguliwa na Bwana, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako. Kumbukumbu la Torati 17:15

you shall surely set him king over you, whom Yahweh your God shall choose: one from among your brothers shall you set king over you; you may not put a foreigner over you, who is not your brother.

Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa Bwana amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile. Kumbukumbu la Torati 17:16

Only he shall not multiply horses to himself, nor cause the people to return to Egypt, to the end that he may multiply horses; because Yahweh has said to you, You shall henceforth return no more that way.

Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno. Kumbukumbu la Torati 17:17

Neither shall he multiply wives to himself, that his heart not turn away: neither shall he greatly multiply to himself silver and gold.

Tena na iwe, zamani aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika chuo, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi; Kumbukumbu la Torati 17:18

It shall be, when he sits on the throne of his kingdom, that he shall write him a copy of this law in a book, out of [that which is] before the priests the Levites:

na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya; Kumbukumbu la Torati 17:19

and it shall be with him, and he shall read therein all the days of his life; that he may learn to fear Yahweh his God, to keep all the words of this law and these statutes, to do them;

moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kuume wala wa kushoto; ili apate kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya Israeli. Kumbukumbu la Torati 17:20

that his heart not be lifted up above his brothers, and that he not turn aside from the commandment, to the right hand, or to the left: to the end that he may prolong his days in his kingdom, he and his children, in the midst of Israel.