Kumbukumbu la Torati Mlango 32 Deuteronomy

Kumbukumbu la Torati 32:1

Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa changu.

Kumbukumbu la Torati 32:2

Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea.

Kumbukumbu la Torati 32:3

Maana nitalitangaza Jina la Bwana; Mpeni ukuu Mungu wetu.

Kumbukumbu la Torati 32:4

Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.

Kumbukumbu la Torati 32:5

Wametenda mambo ya uharibifu, Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao; Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka.

Kumbukumbu la Torati 32:6

Je! Mnamlipa Bwana hivi, Enyi watu wapumbavu na ujinga? Je! Yeye siye baba yako aliyekununua? Amekufanya, na kukuweka imara.

Kumbukumbu la Torati 32:7

Kumbuka siku za kale, Tafakari miaka ya vizazi vingi; Mwulize baba yako, naye atakuonyesha; Wazee wako, nao watakuambia.

Kumbukumbu la Torati 32:8

Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao, Alipowabagua wanadamu, Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.

Kumbukumbu la Torati 32:9

Maana, sehemu ya Bwana ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake.

Kumbukumbu la Torati 32:10

Alimkuta katika nchi ya ukame, Na katika jangwa tupu litishalo; Alimzunguka, akamtunza; Akamhifadhi kama mboni ya jicho;

Kumbukumbu la Torati 32:11

Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake; Na kupapatika juu ya makinda yake, Alikunjua mbawa zake, akawatwaa, Akawachukua juu ya mbawa zake;

Kumbukumbu la Torati 32:12

Bwana peke yake alimwongoza, Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye.

Kumbukumbu la Torati 32:13

Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;

Kumbukumbu la Torati 32:14

Siagi ya ng'ombe, na maziwa ya kondoo, Pamoja na mafuta ya wana-kondoo, Kondoo waume wa Kibashani, na mbuzi, Na unono wa ngano iliyo nzuri; Ukanywa divai, damu ya mizabibu.

Kumbukumbu la Torati 32:15

Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.

Kumbukumbu la Torati 32:16

Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo.

Kumbukumbu la Torati 32:17

Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa.

Kumbukumbu la Torati 32:18

Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau.

Kumbukumbu la Torati 32:19

Bwana akaona, akawachukia, Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake.

Kumbukumbu la Torati 32:20

Akasema, Nitawaficha uso wangu, Nitaona mwisho wao utakuwaje; Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi, Watoto wasio imani ndani yao.

Kumbukumbu la Torati 32:21

Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu; Wamenikasirisha kwa ubatili wao; Nami nitawatia wivu kwa wasio watu, Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.

Kumbukumbu la Torati 32:22

Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima.

Kumbukumbu la Torati 32:23

Nitaweka madhara juu yao chunguchungu; Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe;

Kumbukumbu la Torati 32:24

Watakonda kwa njaa, wataliwa na makaa ya moto, Na uharibifu mkali; Nitawapelekea meno ya wanyama wakali, Pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini.

Kumbukumbu la Torati 32:25

Nje upanga utawafifiliza Na ndani ya vyumba, utisho; Utaangamiza mvulana na msichana, Anyonyaye pamoja na mwenye mvi,

Kumbukumbu la Torati 32:26

Nalisema, Ningewatawanyia mbali, Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu;

Kumbukumbu la Torati 32:27

Isipokuwa naliogopa makamio ya adui, Adui zao wasije wakafikiri uongo, Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka, Wala Bwana hakuyafanya haya yote.

Kumbukumbu la Torati 32:28

Maana hawa ni taifa wasio shauri, Wala fahamu hamna ndani yao.

Kumbukumbu la Torati 32:29

Laiti wangekuwa na akili, hata wakafahamu haya, Ili watafakari mwisho wao.

Kumbukumbu la Torati 32:30

Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?

Kumbukumbu la Torati 32:31

Maana, Mwamba wao si kama Mwamba wetu, Hata adui zetu wenyewe ndivyo wahukumuvyo.

Kumbukumbu la Torati 32:32

Maana, mzabibu wao ni mzabibu wa Sodoma, Nao ni wa mashamba ya Gomora; Zabibu zao ni zabibu za uchungu, Vichala vyao ni vichungu.

Kumbukumbu la Torati 32:33

Mvinyo yao ni sumu ya majoka, Uchungu mkali wa nyoka.

Kumbukumbu la Torati 32:34

Je! Haya hayakuwekwa akiba kwangu? Na kutiwa muhuri kati ya hazina yangu?

Kumbukumbu la Torati 32:35

Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.

Kumbukumbu la Torati 32:36

Kwa kuwa Bwana atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa,

Kumbukumbu la Torati 32:37

Naye atasema, Iko wapi miungu yao, Mwamba ule walioutumaini;

Kumbukumbu la Torati 32:38

Uliokula shahamu za sadaka zao, Na kunywa divai ya sadaka zao za kinywaji? Na waondoke na kuwasaidia ninyi; Na wawe hao himaya yenu.

Kumbukumbu la Torati 32:39

Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,

Kumbukumbu la Torati 32:40

Maana, nainua mkono wangu mbinguni, Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele,

Kumbukumbu la Torati 32:41

Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, Nitawatoza kisasi adui zangu, Nitawalipa wanaonichukia.

Kumbukumbu la Torati 32:42

Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui.

Kumbukumbu la Torati 32:43

Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake; Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake, Atawatoza kisasi adui zake, Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake.

Kumbukumbu la Torati 32:44

Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni.

Kumbukumbu la Torati 32:45

Musa akamaliza kuwaambia Israeli wote maneno haya yote;

Kumbukumbu la Torati 32:46

akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii.

Kumbukumbu la Torati 32:47

Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.

Kumbukumbu la Torati 32:48

Bwana akasema na Musa siku iyo hiyo, akamwambia,

Kumbukumbu la Torati 32:49

Kwea katika mlima huu wa Abarimu, mpaka kilima cha Nebo, kilicho katika nchi ya Moabu, kuelekea Yeriko; ukaangalie nchi ya Kanaani niwapayo wana wa Israeli kuimiliki;

Kumbukumbu la Torati 32:50

ukafe katika kilima, huko ukweako, ukusanywe uwe pamoja na jamaa zako; kama alivyokufa nduguyo Haruni katika mlima wa Hori, akakusanywa awe pamoja na watu wake;

Kumbukumbu la Torati 32:51

kwa sababu mlinikosa ninyi juu yangu katikati ya wana wa Israeli katika maji ya Meriba huko Kadeshi, katika bara ya Sini; kwa kuwa hamkunitakasa katikati ya wana wa Israeli.

Kumbukumbu la Torati 32:52

Kwani utaiona hiyo nchi mbele yako, lakini hutakwenda huko kuingia hiyo nchi niwapayo wana wa Israeli.