Kumbukumbu la Torati 14 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kumbukumbu la Torati 14 (Swahili) Deuteronomy 14 (English)

Ninyi mmekuwa wana wa Bwana, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa. Kumbukumbu la Torati 14:1

You are the children of Yahweh your God: you shall not cut yourselves, nor make any baldness between your eyes for the dead.

Kwa kuwa u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako, na Bwana amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi. Kumbukumbu la Torati 14:2

For you are a holy people to Yahweh your God, and Yahweh has chosen you to be a people for his own possession, above all peoples who are on the face of the earth.

Usile kitu cho chote kichukizacho. Kumbukumbu la Torati 14:3

You shall not eat any abominable thing.

Wanyama mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, Kumbukumbu la Torati 14:4

These are the animals which you may eat: the ox, the sheep, and the goat,

kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima; Kumbukumbu la Torati 14:5

the hart, and the gazelle, and the roebuck, and the wild goat, and the ibex, and the antelope, and the chamois.

na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla. Kumbukumbu la Torati 14:6

Every animal that parts the hoof, and has the hoof cloven in two, [and] chews the cud, among the animals, that may you eat.

Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu; Kumbukumbu la Torati 14:7

Nevertheless these you shall not eat of them that chew the cud, or of those who have the hoof cloven: the camel, and the hare, and the rabbit; because they chew the cud but don't part the hoof, they are unclean to you.

na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse. Kumbukumbu la Torati 14:8

The pig, because it has a split hoof but doesn't chew the cud, is unclean to you: of their flesh you shall not eat, and their carcasses you shall not touch.

Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula; Kumbukumbu la Torati 14:9

These you may eat of all that are in the waters: whatever has fins and scales may you eat;

na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu. Kumbukumbu la Torati 14:10

and whatever doesn't have fins and scales you shall not eat; it is unclean to you.

Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi. Kumbukumbu la Torati 14:11

Of all clean birds you may eat.

Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu; Kumbukumbu la Torati 14:12

But these are they of which you shall not eat: the eagle, and the gier-eagle, and the ospray,

na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake; Kumbukumbu la Torati 14:13

and the red kite, and the falcon, and the kite after its kind,

na kila kunguru kwa aina zake; Kumbukumbu la Torati 14:14

and every raven after its kind,

na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; Kumbukumbu la Torati 14:15

and the ostrich, and the night-hawk, and the sea-mew, and the hawk after its kind,

na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa; Kumbukumbu la Torati 14:16

the little owl, and the great owl, and the horned owl,

na mwari, na nderi, na mnandi; Kumbukumbu la Torati 14:17

and the pelican, and the vulture, and the cormorant,

na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo. Kumbukumbu la Torati 14:18

and the stork, and the heron after its kind, and the hoopoe, and the bat.

Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale. Kumbukumbu la Torati 14:19

All winged creeping things are unclean to you: they shall not be eaten.

Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi. Kumbukumbu la Torati 14:20

Of all clean birds you may eat.

Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye. Kumbukumbu la Torati 14:21

You shall not eat of anything that dies of itself: you may give it to the foreigner living among you who is within your gates, that he may eat it; or you may sell it to a foreigner: for you are a holy people to Yahweh your God. You shall not boil a kid in its mother's milk.

Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. Kumbukumbu la Torati 14:22

You shall surely tithe all the increase of your seed, that which comes forth from the field year by year.

Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima. Kumbukumbu la Torati 14:23

You shall eat before Yahweh your God, in the place which he shall choose, to cause his name to dwell there, the tithe of your grain, of your new wine, and of your oil, and the firstborn of your herd and of your flock; that you may learn to fear Yahweh your God always.

Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako; Kumbukumbu la Torati 14:24

If the way be too long for you, so that you are not able to carry it, because the place is too far from you, which Yahweh your God shall choose, to set his name there, when Yahweh your God shall bless you;

ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; Kumbukumbu la Torati 14:25

then shall you turn it into money, and bind up the money in your hand, and shall go to the place which Yahweh your God shall choose:

na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; Kumbukumbu la Torati 14:26

and you shall bestow the money for whatever your soul desires, for oxen, or for sheep, or for wine, or for strong drink, or for whatever your soul asks of you; and you shall eat there before Yahweh your God, and you shall rejoice, you and your household.

na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe. Kumbukumbu la Torati 14:27

The Levite who is within your gates, you shall not forsake him; for he has no portion nor inheritance with you.

Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; Kumbukumbu la Torati 14:28

At the end of every three years you shall bring forth all the tithe of your increase in the same year, and shall lay it up within your gates:

na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo. Kumbukumbu la Torati 14:29

and the Levite, because he has no portion nor inheritance with you, and the foreigner living among you, and the fatherless, and the widow, who are within your gates, shall come, and shall eat and be satisfied; that Yahweh your God may bless you in all the work of your hand which you do.