Kumbukumbu la Torati Mlango 27 Deuteronomy

Kumbukumbu la Torati 27:1

Musa na wazee wa Israeli wakawaagiza wale watu wakawaambia, Shikeni maagizo yote niwaagizayo leo.

Kumbukumbu la Torati 27:2

Na iwe, siku mtakayovuka Yordani kwenda nchi akupayo Bwana, Mungu wako, ujisimamishie mawe makubwa, ukayatalize matalizo,

Kumbukumbu la Torati 27:3

uyaandike maneno yote ya torati hii juu yake, utakapokwisha kuvuka; ili upate kuingia nchi akupayo Bwana, Mungu wako, nchi imiminikayo maziwa na asali, kama alivyokuahidi Bwana, Mungu wa baba zako.

Kumbukumbu la Torati 27:4

Na iwe, mtakapokwisha vuka Yordani myasimamishe mawe haya, niwaagizayo hivi leo, katika mlima Ebali, nawe yatalize matalizo.

Kumbukumbu la Torati 27:5

Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake.

Kumbukumbu la Torati 27:6

Jenga hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee Bwana, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;

Kumbukumbu la Torati 27:7

ufanye na sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi mbele za Bwana, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 27:8

Kisha, andika juu ya mawe hayo maneno ya torati hii yote, waziwazi sana.

Kumbukumbu la Torati 27:9

Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa Bwana, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 27:10

Basi isikize sauti ya Bwana, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo.

Kumbukumbu la Torati 27:11

Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema,

Kumbukumbu la Torati 27:12

Hawa na wasimame juu ya mlima wa Gerizimu kwa kuwabarikia watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini;

Kumbukumbu la Torati 27:13

na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali.

Kumbukumbu la Torati 27:14

Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu,

Kumbukumbu la Torati 27:15

Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:16

Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:17

Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:18

Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:19

Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:20

Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:21

Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:22

Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:23

Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:24

Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:25

Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina.

Kumbukumbu la Torati 27:26

Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.