Ayabu 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 8 (Swahili) Job 8 (English)

Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema, Ayabu 8:1

Then Bildad the Shuhite answered,

Wewe utanena maneno haya hata lini? Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini? Ayabu 8:2

"How long will you speak these things? Shall the words of your mouth be a mighty wind?

Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? Ayabu 8:3

Does God pervert justice? Or does the Almighty pervert righteousness?

Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao; Ayabu 8:4

If your children have sinned against him, He has delivered them into the hand of their disobedience;

Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; Ayabu 8:5

If you want to seek God diligently, Make your supplication to the Almighty.

Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa. Ayabu 8:6

If you were pure and upright, Surely now he would awaken for you, And make the habitation of your righteousness prosperous.

Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana. Ayabu 8:7

Though your beginning was small, Yet your latter end would greatly increase.

Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta; Ayabu 8:8

"Please inquire of past generations, Find out about the learning of their fathers.

(Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;) Ayabu 8:9

(For we are but of yesterday, and know nothing, Because our days on earth are a shadow.)

Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao? Ayabu 8:10

Shall they not teach you, tell you, And utter words out of their heart?

Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope Na makangaga kumea pasipo maji? Ayabu 8:11

"Can the papyrus grow up without mire? Can the rushes grow without water?

Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine. Ayabu 8:12

While it is yet in its greenness, not cut down, It withers before any other reed.

Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia; Ayabu 8:13

So are the paths of all who forget God. The hope of the godless man shall perish,

Uthabiti wake utavunjika, Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui. Ayabu 8:14

Whose confidence shall break apart, Whose trust is a spider's web.

Ataitegemea nyumba yake, isisimame; Atashikamana nayo, isidumu. Ayabu 8:15

He shall lean on his house, but it shall not stand. He shall cling to it, but it shall not endure.

Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua, Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake. Ayabu 8:16

He is green before the sun, His shoots go forth over his garden.

Mizizi yake huzonga-zonga chuguu, Huangalia mahali penye mawe. Ayabu 8:17

His roots are wrapped around the rock pile, He sees the place of stones.

Lakini, aking'olewa mahali pake, Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona. Ayabu 8:18

If he is destroyed from his place, Then it shall deny him, saying, 'I have not seen you.'

Tazama, furaha ya njia yake ni hii, Na wengine watachipuka kutoka katika nchi. Ayabu 8:19

Behold, this is the joy of his way: Out of the earth shall others spring.

Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu. Ayabu 8:20

"Behold, God will not cast away a blameless man, Neither will he uphold the evil-doers.

Bado atakijaza kinywa chako kicheko, Na midomo yako ataijaza shangwe. Ayabu 8:21

He will still fill your mouth with laughter, Your lips with shouting.

Hao wakuchukiao watavikwa aibu; Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena. Ayabu 8:22

Those who hate you shall be clothed with shame. The tent of the wicked shall be no more."