Ayabu 27 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 27 (Swahili) Job 27 (English)

Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema, Ayabu 27:1

Job again took up his parable, and said,

Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu; Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu; Ayabu 27:2

"As God lives, who has taken away my right, The Almighty, who has made my soul bitter.

(Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu, Na roho ya Mungu i katika pua yangu;) Ayabu 27:3

(For the length of my life is still in me, And the spirit of God is in my nostrils);

Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki, Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu. Ayabu 27:4

Surely my lips shall not speak unrighteousness, Neither shall my tongue utter deceit.

Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki; Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu. Ayabu 27:5

Far be it from me that I should justify you. Until I die I will not put away my integrity from me.

Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha; Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai. Ayabu 27:6

I hold fast to my righteousness, and will not let it go. My heart shall not reproach me so long as I live.

Adui yangu na awe kama huyo mwovu, Na mwenye kuondoka kinyume changu na awe kama asiye haki. Ayabu 27:7

"Let my enemy be as the wicked, Let him who rises up against me be as the unrighteous.

Kwani tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida, Hapo Mungu amwondoleapo roho yake? Ayabu 27:8

For what is the hope of the godless, when he is cut off, When God takes away his life?

Je! Mungu atakisikia kilio chake, Taabu zitakapomfikilia? Ayabu 27:9

Will God hear his cry, When trouble comes on him?

Je! Atajifurahisha katika Mwenyezi, Na kumlingana Mungu nyakati zote? Ayabu 27:10

Will he delight himself in the Almighty, And call on God at all times?

Nitawafundisha ninyi mambo ya mkono wa Mungu; Hayo yaliyo kwa Mwenyezi sitayaficha. Ayabu 27:11

I will teach you about the hand of God. That which is with the Almighty will I not conceal.

Tazama, ninyi nyote mmeyaona wenyewe; Mbona basi mmebatilika kabisa? Ayabu 27:12

Behold, all of you have seen it yourselves; Why then have you become altogether vain?

Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu, Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi. Ayabu 27:13

"This is the portion of a wicked man with God, The heritage of oppressors, which they receive from the Almighty.

Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga; Na wazao wake hawatashiba chakula. Ayabu 27:14

If his children are multiplied, it is for the sword. His offspring shall not be satisfied with bread.

Hao watakaosalia kwake watazikwa katika kufa, Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza. Ayabu 27:15

Those who remain of him shall be buried in death. His widows shall make no lamentation.

Ajapokusanya fedha kama mavumbi, Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi; Ayabu 27:16

Though he heap up silver as the dust, And prepare clothing as the clay;

Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa, Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha. Ayabu 27:17

He may prepare it, but the just shall put it on, And the innocent shall divide the silver.

Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu, Na kama kibanda afanyacho mlinzi. Ayabu 27:18

He builds his house as the moth, As a booth which the watchman makes.

Yeye hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho; Hufunua macho yake, naye hayuko. Ayabu 27:19

He lies down rich, but he shall not do so again. He opens his eyes, and he is not.

Vitisho vyampata kama maji mengi; Dhoruba humwiba usiku. Ayabu 27:20

Terrors overtake him like waters; A tempest steals him away in the night.

Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka; Na kumkumba atoke mahali pake. Ayabu 27:21

The east wind carries him away, and he departs; It sweeps him out of his place.

Kwani Mungu atamtupia asimhurumie; Angependa kuukimbia mkono wake. Ayabu 27:22

For it hurls at him, and does not spare, As he flees away from his hand.

Watu watampigia makofi, Na kumzomea atoke mahali pake.

Ayabu 27:23

Men shall clap their hands at him, And shall hiss him out of his place.