Ayabu 28 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 28 (Swahili) Job 28 (English)

Hakika kuna shimo wachimbako fedha, Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo. Ayabu 28:1

"Surely there is a mine for silver, And a place for gold which they refine.

Chuma hufukuliwa katika ardhi, Na shaba huyeyushwa katika mawe. Ayabu 28:2

Iron is taken out of the earth, And copper is smelted out of the ore.

Binadamu hukomesha giza; Huyatafuta-tafuta hata mpaka ulio mbali, Mawe ya giza kuu, giza tupu. Ayabu 28:3

Man sets an end to darkness, And searches out, to the furthest bound, The stones of obscurity and of thick darkness.

Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning'inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko. Ayabu 28:4

He breaks open a shaft away from where people live. They are forgotten by the foot. They hang far from men, they swing back and forth.

Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula; Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto. Ayabu 28:5

As for the earth, out of it comes bread; Underneath it is turned up as it were by fire.

Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti; Nayo ina mchanga wa dhahabu. Ayabu 28:6

Sapphires come from its rocks. It has dust of gold.

Njia ile hapana ndege mkali aijuaye, Wala jicho la tai halijaiona; Ayabu 28:7

That path no bird of prey knows, Neither has the falcon's eye seen it.

Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga, Wala simba mkali hajaipita. Ayabu 28:8

The proud animals have not trodden it, Nor has the fierce lion passed by there.

Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake. Ayabu 28:9

He puts forth his hand on the flinty rock, And he overturns the mountains by the roots.

Hukata mifereji kati ya majabali; Na jicho lake huona kila kito cha thamani Ayabu 28:10

He cuts out channels among the rocks. His eye sees every precious thing.

Hufunga vijito visichuruzike; Na kitu kilichostirika hukifunua. Ayabu 28:11

He binds the streams that they don't trickle; The thing that is hidden he brings forth to light.

Bali hekima itapatikana wapi? Na mahali pa ufahamu ni wapi? Ayabu 28:12

"But where shall wisdom be found? Where is the place of understanding?

Mwanadamu hajui thamani yake, Wala haionekani katika nchi ya walio hai. Ayabu 28:13

Man doesn't know its price; Neither is it found in the land of the living.

Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu; Na bahari yasema, Haiko kwangu. Ayabu 28:14

The deep says, 'It isn't in me.' The sea says, 'It isn't with me.'

Haipatikani kwa dhahabu, Wala fedha haitapimwa iwe thamani yake. Ayabu 28:15

It can't be gotten for gold, Neither shall silver be weighed for its price.

Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti ya samawi. Ayabu 28:16

It can't be valued with the gold of Ophir, With the precious onyx, or the sapphire{or, lapis lazuli}.

Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi. Ayabu 28:17

Gold and glass can't equal it, Neither shall it be exchanged for jewels of fine gold.

Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani. Ayabu 28:18

No mention shall be made of coral or of crystal: Yes, the price of wisdom is above rubies.

Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo, Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi. Ayabu 28:19

The topaz of Ethiopia shall not equal it, Neither shall it be valued with pure gold.

Basi hekima yatoka wapi? Na mahali pa ufahamu ni wapi? Ayabu 28:20

Whence then comes wisdom? Where is the place of understanding?

Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai, Na kusitirika na ndege wa angani. Ayabu 28:21

Seeing it is hidden from the eyes of all living, And kept close from the birds of the sky.

Uharibifu na Mauti husema, Tumesikia habari zake kwa masikio yetu. Ayabu 28:22

Destruction and Death say, 'We have heard a rumor of it with our ears.'

Mungu ndiye aijuaye njia yake, Naye anajua mahali pake. Ayabu 28:23

"God understands its way, And he knows its place.

Maana anatazama hata miisho ya nchi, Na kuona chini ya mbingu nzima. Ayabu 28:24

For he looks to the ends of the earth, And sees under the whole sky.

Apate kuufanyia upepo uzito wake; Naam, anayapima maji kwa kipimo. Ayabu 28:25

He establishes the force of the wind; Yes, he measures out the waters by measure.

Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa umeme wa radi. Ayabu 28:26

When he made a decree for the rain, And a way for the lightning of the thunder;

Ndipo alipoiona na kuitangaza; Aliithibitisha, naam, na kuichunguza. Ayabu 28:27

Then did he see it, and declare it. He established it, yes, and searched it out.

Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu. Ayabu 28:28

To man he said, 'Behold, the fear of the Lord, that is wisdom. To depart from evil is understanding.'"