Ayabu 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 15 (Swahili) Job 15 (English)

Ndipo Elifazi, Mtemani, akajibu, na kusema, Ayabu 15:1

Then Eliphaz the Temanite answered,

Je! Yapasa mtu mwenye hekima kujibu kwa ujuzi wa uvuvio, Na kujaza tumbo lake na upepo wa mashariki? Ayabu 15:2

"Should a wise man answer with vain knowledge, And fill himself with the east wind?

Je! Ahoji na mazungumzo yasiyo faida, Au kwa maneno ambayo hawezi kufanya mema kwayo? Ayabu 15:3

Should he reason with unprofitable talk, Or with speeches with which he can do no good?

Naam, wewe waondoa kicho, Nawe wazuia ibada mbele za Mungu. Ayabu 15:4

Yes, you do away with fear, And hinder devotion before God.

Kwani uovu wako unakufundisha kinywa chako, Nawe wachagua ulimi wake mwenye hila. Ayabu 15:5

For your iniquity teaches your mouth, And you choose the language of the crafty.

Kinywa chako mwenyewe chakuhukumia makosa, wala si mimi; Naam, midomo yako mwenyewe hushuhudia juu yako. Ayabu 15:6

Your own mouth condemns you, and not I; Yes, your own lips testify against you.

Je! Wewe u mtu wa kwanza aliyezaliwa? Au, ulizawa wewe kabla ya milima? Ayabu 15:7

"Are you the first man who was born? Or were you brought forth before the hills?

Je! Umesikia mashauri ya siri ya Mungu? Nawe je! Wazuia hekima iwe yako tu? Ayabu 15:8

Have you heard the secret counsel of God? Do you limit wisdom to yourself?

Je! Wewe wajua neno lipi, ambalo sisi hatulijui? Nawe wafahamu nini, ambalo halimo ndani yetu? Ayabu 15:9

What do you know, that we don't know? What do you understand, which is not in us?

Wenye mvi, na walio wazee sana, wote wapo pamoja nasi, Ambao ni wazee kuliko baba yako. Ayabu 15:10

With us are both the gray-headed and the very aged men, Much elder than your father.

Je! Utulizi wa Mungu ni mdogo sana kwako, Na hilo neno la upole si kitu kwako? Ayabu 15:11

Are the consolations of God too small for you, Even the word that is gentle toward you?

Mbona moyo wako unakutaharakisha! Na macho yako, je! Kwani kung'ariza? Ayabu 15:12

Why does your heart carry you away? Why do your eyes flash,

Hata ukageuza roho yako iwe kinyume cha Mungu, Na kuyatoa maneno kama hayo kinywani mwako. Ayabu 15:13

That you turn your spirit against God, And let such words go out of your mouth?

Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi? Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki? Ayabu 15:14

What is man, that he should be clean? He who is born of a woman, that he should be righteous?

Yeye hawategemei watakatifu wake; Naam, mbingu nazo si safi machoni pake. Ayabu 15:15

Behold, he puts no trust in his holy ones; Yes, the heavens are not clean in his sight:

Sembuse mtu ambaye ni mwenye kuchukiza na uchafu, Mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji! Ayabu 15:16

How much less one who is abominable and corrupt, A man who drinks iniquity like water!

Mimi nitakuonyesha, unisikilize; Na hayo yote niliyoyaona nitayanena; Ayabu 15:17

"I will show you, listen to me; That which I have seen I will declare:

(Ambayo watu wenye hekima wameyatangaza Tokea baba zao, wala hawakuyaficha; Ayabu 15:18

(Which wise men have told From their fathers, and have not hidden it;

Waliopewa hiyo nchi peke yao, Wala mgeni hakupita kati yao); Ayabu 15:19

To whom alone the land was given, And no stranger passed among them):

Mtu mwovu huwa na uchungu siku zake zote, Hata hesabu ya miaka aliyowekewa mwenye kuonea. Ayabu 15:20

The wicked man travails with pain all his days, Even the number of years that are laid up for the oppressor.

Sauti za utisho zi masikioni mwake; Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake; Ayabu 15:21

A sound of terrors is in his ears; In prosperity the destroyer shall come on him.

Yeye hasadiki kwamba atarudi kutoka gizani, Naye hungojewa na upanga; Ayabu 15:22

He doesn't believe that he shall return out of darkness, He is waited for by the sword.

Hutanga-tanga ili apate chakula, akisema, Ki wapi? Ajua kwamba siku ya giza i tayari karibu yake; Ayabu 15:23

He wanders abroad for bread, saying, 'Where is it?' He knows that the day of darkness is ready at his hand.

Mateso na dhiki humtia hofu; Humshinda kama vile mfalme aliye tayari kwa vita; Ayabu 15:24

Distress and anguish make him afraid; They prevail against him, as a king ready to the battle.

Kwa kuwa amenyosha mkono wake juu ya Mungu, Na kuendelea kwa kiburi kinyume cha Mwenyezi; Ayabu 15:25

Because he has stretched out his hand against God, And behaves himself proudly against the Almighty;

Humshambulia na shingo ngumu, Kwa mafundo makubwa ya ngao zake; Ayabu 15:26

He runs at him with a stiff neck, With the thick shields of his bucklers;

Kwa kuwa amefunika uso wake na kunona kwake, Na kuwandisha mafuta kiunoni mwake; Naye amekaa katika miji iliyo ukiwa, Ayabu 15:27

Because he has covered his face with his fatness, And gathered fat on his loins.

Katika nyumba ambazo hapana mtu azikaaye, Zilizokuwa tayari kuwa magofu. Ayabu 15:28

He has lived in desolate cities, In houses which no one inhabited, Which were ready to become heaps.

Hatakuwa tajiri, wala mali zake hazitadumu, Wala maongeo yao hayatainama nchi. Ayabu 15:29

He shall not be rich, neither shall his substance continue, Neither shall their possessions be extended on the earth.

Hataondoka gizani; Ndimi za moto zitayakausha matawi yake, Naye ataondoka kwa pumzi za kinywa chake. Ayabu 15:30

He shall not depart out of darkness; The flame shall dry up his branches, By the breath of God's mouth shall he go away.

Asiutumainie ubatili, na kujidanganya; Kwa kuwa huo ubatili ndio utakaokuwa ujira wake. Ayabu 15:31

Let him not trust in emptiness, deceiving himself; For emptiness shall be his reward.

Jambo hili litatendeka kabla ya wakati wake, Na tawi lake halitasitawi. Ayabu 15:32

It shall be accomplished before his time. His branch shall not be green.

Atayapukutisha mapooza yake kama mzabibu, Na kuyatupa maua yake kama mzeituni. Ayabu 15:33

He shall shake off his unripe grape as the vine, And shall cast off his flower as the olive tree.

Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa. Ayabu 15:34

For the company of the godless shall be barren, And fire shall consume the tents of bribery.

Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu, Nalo tumbo lao hutengeza udanganyifu.

Ayabu 15:35

They conceive mischief, and bring forth iniquity. Their heart prepares deceit."