Ayabu 37 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 37 (Swahili) Job 37 (English)

Moyo wangu hunitetema kwayo pia, Nao hutoka mahali pake. Ayabu 37:1

"Yes, at this my heart trembles, And is moved out of its place.

Zisikizeni hizo kelele za sauti yake, Na uvumi utokao kinywani mwake. Ayabu 37:2

Hear, oh, hear the noise of his voice, The sound that goes out of his mouth.

Yeye huituma iende chini ya mbingu zote, Na radi yake hata miisho ya nchi. Ayabu 37:3

He sends it forth under the whole sky, And his lightning to the ends of the earth.

Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo. Ayabu 37:4

After it a voice roars. He thunders with the voice of his majesty; He doesn't hold back anything when his voice is heard.

Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuelewa nayo. Ayabu 37:5

God thunders marvelously with his voice. He does great things, which we can't comprehend.

Kwani huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na vivyo manyonyota ya mvua, Na hayo maji ya mvua yake kubwa. Ayabu 37:6

For he says to the snow, 'Fall on the earth;' Likewise to the shower of rain, And to the showers of his mighty rain.

Huufunga mkono wa kila binadamu; Ili watu wote aliowaumba wajue. Ayabu 37:7

He seals up the hand of every man, That all men whom he has made may know it.

Hapo wanyama huingia mafichoni, Na kukaa katika mapango yao. Ayabu 37:8

Then the animals take cover, And remain in their dens.

Dhoruba hutoka katika vyumba vyake; Na baridi ghalani mwake. Ayabu 37:9

Out of its chamber comes the storm, And cold out of the north.

Barafu huletwa kwa pumzi za Mungu; Na upana wa maji huganda. Ayabu 37:10

By the breath of God, ice is given, And the breadth of the waters is frozen.

Naam, huyatweka mawingu mazito mzigo wa maji; Hulitandika wingu la umeme wake; Ayabu 37:11

Yes, he loads the thick cloud with moisture. He spreads abroad the cloud of his lightning.

Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake, Ili yafanye yote atakayoyaagiza Juu ya uso wa dunia hii ikaayo watu; Ayabu 37:12

It is turned round about by his guidance, That they may do whatever he commands them On the surface of the habitable world,

Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake, Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye. Ayabu 37:13

Whether it is for correction, or for his land, Or for loving kindness, that he causes it to come.

Sikiliza neno hili, Ee Ayubu; Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu. Ayabu 37:14

"Listen to this, Job: Stand still, and consider the wondrous works of God.

Je! Wajua wewe jinsi Mungu anavyoziagiza, Na kuumulikisha umeme wa wingu lake? Ayabu 37:15

Do you know how God controls them, And causes the lightning of his cloud to shine?

Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa? Ayabu 37:16

Do you know the workings of the clouds, The wondrous works of him who is perfect in knowledge?

Jinsi nguo zako zilivyo na moto, Hapo nchi ituliapo kwa sababu ya upepo wa kusini? Ayabu 37:17

You whose clothing is warm, When the earth is still by reason of the south wind?

Je! Waweza kuzitandaza mbingu pamoja naye, Ambazo zina nguvu kama kioo cha kuyeyushwa? Ayabu 37:18

Can you, with him, spread out the sky, Which is strong as a cast metal mirror?

Utufundishe ni maneno gani tutakayomwambia; Kwa maana hamwezi kuyatengeza kwa sababu ya giza. Ayabu 37:19

Teach us what we shall tell him; For we can't make our case by reason of darkness.

Je! Aambiwe kwamba nataka kunena? Au mtu angetamani kumezwa? Ayabu 37:20

Shall it be told him that I would speak? Or should a man wish that he were swallowed up?

Na sasa watu hawawezi kuutazama mwanga ung'aao mbinguni; Lakini upepo ukipita huzitakasa. Ayabu 37:21

Now men don't see the light which is bright in the skies, But the wind passes, and clears them.

Kaskazini hutokea umemetufu wa dhahabu; Mungu huvikwa ukuu utishao. Ayabu 37:22

Out of the north comes golden splendor; With God is awesome majesty.

yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea. Ayabu 37:23

We can't reach the Almighty, He is exalted in power; In justice and great righteousness he will not oppress.

Kwa hiyo watu humwogopa; Yeye hawaangalii walio na hekima mioyoni. Ayabu 37:24

Therefore men revere him. He doesn't regard any who are wise of heart."