Ayabu 40 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 40 (Swahili) Job 40 (English)

Bwana akafuliza kumjibu Ayubu, na kusema, Ayabu 40:1

Moreover Yahweh answered Job,

Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye. Ayabu 40:2

"Shall he who argues contend with the Almighty? He who argues with God, let him answer it."

Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema, Ayabu 40:3

Then Job answered Yahweh,

Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini? Naweka mkono wangu kinywani pangu. Ayabu 40:4

"Behold, I am of small account. What shall I answer you? I lay my hand on my mouth.

Nimenena mara moja, nami sitajibu; Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi. Ayabu 40:5

I have spoken once, and I will not answer; Yes, twice, but I will proceed no further."

Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Ayabu 40:6

Then Yahweh answered Job out of the whirlwind,

Jifunge viuno kama mwanamume, Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie. Ayabu 40:7

"Now brace yourself like a man. I will question you, and you will answer me.

Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki? Ayabu 40:8

Will you even annul my judgment? Will you condemn me, that you may be justified?

Au je! Wewe una mkono kama Mungu? Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye? Ayabu 40:9

Or have you an arm like God? Can you thunder with a voice like him?

Haya! Jivike sasa fahari na ukuu; Jipambe heshima na enzi. Ayabu 40:10

"Now deck yourself with excellency and dignity. Array yourself with honor and majesty.

Mwaga mafuriko ya hasira zako, Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili. Ayabu 40:11

Pour forth the fury of your anger. Look on everyone who is proud, and bring him low.

Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe, Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo. Ayabu 40:12

Look on everyone who is proud, and humble him. Crush the wicked in their place.

Wafiche mavumbini pamoja, Wafunge nyuso zao mahali palipositirika. Ayabu 40:13

Hide them in the dust together. Bind their faces in the hidden place.

Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako, Ya kuwa mkono wako wa kuume waweza kukuokoa. Ayabu 40:14

Then I will also admit to you That your own right hand can save you.

Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe; Yeye hula nyasi kama vile ng'ombe, Ayabu 40:15

"See now, behemoth, which I made as well as you. He eats grass as an ox.

Tazama basi, nguvu zake ni katika viuno vyake, Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake. Ayabu 40:16

Look now, his strength is in his loins, His force is in the muscles of his belly.

Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi; Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja. Ayabu 40:17

He moves his tail like a cedar: The sinews of his thighs are knit together.

Mifupa yake ni kama mirija ya shaba; Mbavu zake ni kama vipande vya chuma. Ayabu 40:18

His bones are like tubes of brass. His limbs are like bars of iron.

Yeye ni mkuu wa njia za Mungu; Yeye aliyemfanya alimpa upanga wake. Ayabu 40:19

He is the chief of the ways of God. He who made him gives him his sword.

Hakika milima humtolea chakula; Hapo wachezapo wanyama wote wa barani. Ayabu 40:20

Surely the mountains bring him forth food, Where all the animals of the field do play.

Hulala chini ya miti yenye vivuli, Mafichoni penye mianzi, na matopeni. Ayabu 40:21

He lies under the lotus trees, In the covert of the reed, and the marsh.

Hiyo miti yenye vivuli humfunika kwa vivuli vyao; Mierebi ya vijito humzunguka. Ayabu 40:22

The lotuses cover him with their shade. The willows of the brook surround him.

Tazama, mto ukifurika, yeye hatetemeki; Hujiona yu salama, ijapokuwa Yordani hufurika hata kinywani pake. Ayabu 40:23

Behold, if a river overflows, he doesn't tremble. He is confident, though the Jordan swells even to his mouth.

Je! Mtu ye yote atamnasa akiwa yu macho, Au, kumtoboa pua yake kwa mtego? Ayabu 40:24

Shall any take him when he is on the watch, Or pierce through his nose with a snare?