Ayabu 29 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 29 (Swahili) Job 29 (English)

Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema, Ayabu 29:1

Job again took up his parable, and said,

Laiti ningekuwa kama nilivyokuwa katika miezi ya kale, Kama katika siku hizo Mungu aliponilinda; Ayabu 29:2

"Oh that I were as in the months of old, As in the days when God watched over me;

Hapo taa yake ilipomulika juu yangu kichwani, Nami nilitembea gizani kwa njia ya mwanga wake; Ayabu 29:3

When his lamp shone on my head, And by his light I walked through darkness;

Kama nilivyokuwa katika siku zangu za kukomaa, Hapo siri ya Mungu ilipokuwa hemani mwangu; Ayabu 29:4

As I was in the ripeness of my days, When the friendship of God was in my tent;

Wakati Mwenyezi alipokuwa akali pamoja nami, Nao watoto wangu walipokuwa wakinizunguka; Ayabu 29:5

When the Almighty was yet with me, And my children were around me;

Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi, Nalo jabali liliponimiminia mito ya mafuta! Ayabu 29:6

When my steps were washed with butter, And the rock poured out streams of oil for me!

Wakati nilipotoka kwenda mjini, hata langoni, Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu, Ayabu 29:7

When I went forth to the city gate, When I prepared my seat in the street,

Hao vijana waliniona wakajificha, Nao wazee wakaniondokea na kusimama; Ayabu 29:8

The young men saw me and hid themselves, The aged rose up and stood;

Wakuu wakanyamaa wasinene, Na kuweka mikono yao vinywani mwao; Ayabu 29:9

The princes refrained from talking, And laid their hand on their mouth;

Sauti yao masheki ilinyamaa, Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao. Ayabu 29:10

The voice of the nobles was hushed, And their tongue stuck to the roof of their mouth.

Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia. Ayabu 29:11

For when the ear heard me, then it blessed me; And when the eye saw me, it commended me:

Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia. Ayabu 29:12

Because I delivered the poor who cried, And the fatherless also, who had none to help him.

Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha. Ayabu 29:13

The blessing of him who was ready to perish came on me, And I caused the widow's heart to sing for joy.

Nalijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba. Ayabu 29:14

I put on righteousness, and it clothed me. My justice was as a robe and a diadem.

Nalikuwa macho kwa kipofu, Nalikuwa miguu kwa aliyechechemea. Ayabu 29:15

I was eyes to the blind, And feet to the lame.

Nalikuwa baba kwa mhitaji, Na daawa ya mtu nisiyemjua naliichunguza. Ayabu 29:16

I was a father to the needy. The cause of him who I didn't know, I searched out.

Nami nilizivunja taya za wasio haki, Na kumpokonya mawindo katika meno yake. Ayabu 29:17

I broke the jaws of the unrighteous, And plucked the prey out of his teeth.

Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kioto changu, Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga; Ayabu 29:18

Then I said, 'I shall die in my own house, I shall number my days as the sand.

Shina langu limeenea hata kufika majini, Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu; Ayabu 29:19

My root is spread out to the waters, The dew lies all night on my branch;

Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu. Ayabu 29:20

My glory is fresh in me, My bow is renewed in my hand.'

Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja, Wakanyamaa kimya wapate sikia mashauri yangu. Ayabu 29:21

"Men listened to me, waited, And kept silence for my counsel.

Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu; Matamko yangu yakadondoka juu yao. Ayabu 29:22

After my words they didn't speak again; My speech fell on them.

Walikuwa wakiningojea kama kungojea mvua; Wakafunua vinywa vyao sana kama mvua ya masika. Ayabu 29:23

They waited for me as for the rain. Their mouths drank as with the spring rain.

Walipokata tamaa nikacheka nao; Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha. Ayabu 29:24

I smiled on them when they had no confidence. They didn't reject the light of my face.

Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao. Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari, Mfano wa awafarijiye hao waombolezao. Ayabu 29:25

I chose out their way, and sat as chief. I lived as a king in the army, As one who comforts the mourners.