Ayabu 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 5 (Swahili) Job 5 (English)

Haya, ita sasa; je! Yuko atakayekujibu? Nawe utamwelekea yupi katika hao watakatifu? Ayabu 5:1

"Call now; is there any who will answer you? To which of the holy ones will you turn?

Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga. Ayabu 5:2

For resentment kills the foolish man, And jealousy kills the simple.

Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi; Lakini mara niliyalaani maskani yake. Ayabu 5:3

I have seen the foolish taking root, But suddenly I cursed his habitation.

Watoto wake wako mbali na wokovu, Nao wamesongwa langoni, Wala hapana atakayewaponya. Ayabu 5:4

His children are far from safety, They are crushed in the gate. Neither is there any to deliver them,

Mavuno yake wale wenye njaa huyala, Na kuyatwaa hata kuyatoa miibani, Nao wenye kiu huzitwetea mali zao. Ayabu 5:5

Whose harvest the hungry eats up, And take it even out of the thorns; The snare gapes for their substance.

Kwani taabu haitoki mchangani, Wala mashaka hayachipuki katika nchi; Ayabu 5:6

For affliction doesn't come forth from the dust, Neither does trouble spring out of the ground;

Lakini mwanadamu huzaliwa ili apate mashaka, Kama cheche za moto zirukavyo juu. Ayabu 5:7

But man is born to trouble, As the sparks fly upward.

Lakini mimi ningemtafuta Mungu, Ningemwekea Mungu daawa yangu; Ayabu 5:8

"But as for me, I would seek God, To God would I commit my cause;

Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana; Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu; Ayabu 5:9

Who does great things that can't be fathomed, Marvelous things without number;

Yeye atoaye mvua inyeshe juu ya nchi, Na kuyapeleka maji mashambani; Ayabu 5:10

Who gives rain on the earth, And sends waters on the fields;

Awainuaye juu hao walio chini; Na hao waombolezao hukuzwa wawe salama. Ayabu 5:11

So that he sets up on high those who are low, Those who mourn are exalted to safety.

Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao. Ayabu 5:12

He frustrates the devices of the crafty, So that their hands can't perform their enterprise.

Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka. Ayabu 5:13

He takes the wise in their own craftiness; The counsel of the cunning is carried headlong.

Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vilevile kama usiku. Ayabu 5:14

They meet with darkness in the day-time, And grope at noonday as in the night.

Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari. Ayabu 5:15

But he saves from the sword of their mouth, Even the needy from the hand of the mighty.

Basi hivi huyo maskini ana matumaini, Na uovu hufumba kinywa chake. Ayabu 5:16

So the poor has hope, And injustice shuts her mouth.

Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye; Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi. Ayabu 5:17

"Behold, happy is the man whom God corrects: Therefore do not despise the chastening of the Almighty.

Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya. Ayabu 5:18

For he wounds, and binds up; He injures, and his hands make whole.

Yeye atakuokoa na mateso sita; Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa. Ayabu 5:19

He will deliver you in six troubles; Yes, in seven there shall no evil touch you.

Wakati wa njaa atakukomboa na mauti; Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga. Ayabu 5:20

In famine he will redeem you from death; In war, from the power of the sword.

Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja. Ayabu 5:21

You shall be hidden from the scourge of the tongue, Neither shall you be afraid of destruction when it comes.

Wewe utayacheka maangamizo na njaa; Wala hutawaogopa wanyama wakali wa nchi. Ayabu 5:22

At destruction and famine you shall laugh, Neither shall you be afraid of the animals of the earth.

Kwani utakuwa na mapatano na mawe ya bara; Nao wanyama wa bara watakuwa na amani kwako. Ayabu 5:23

For you shall be in league with the stones of the field. The animals of the field shall be at peace with you.

Nawe utajua ya kwamba hema yako ina salama; Na zizi lako utaliaua, wala usikose kitu. Ayabu 5:24

You shall know that your tent is in peace. You shall visit your fold, and shall miss nothing.

Tena utajua ya kwamba uzao wako utakuwa mwingi, Na vizazi vyako watakuwa kama nyasi za nchi. Ayabu 5:25

You shall know also that your seed shall be great, Your offspring as the grass of the earth.

Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake. Ayabu 5:26

You shall come to your grave in a full age, Like a shock of grain comes in its season.

Tazama, haya tumeyapeleleza, ndivyo yalivyo; Yasikie, uyajue, ili upate mema. Ayabu 5:27

Look this, we have searched it, so it is; Hear it, and know it for your good."