Ayabu 42 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ayabu 42 (Swahili) Job 42 (English)

Ndipo Ayubu akamjibu Bwana, na kusema. Ayabu 42:1

Then Job answered Yahweh,

Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. Ayabu 42:2

"I know that you can do all things, And that no purpose of yours can be restrained.

Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. Ayabu 42:3

You asked, 'Who is this who hides counsel without knowledge?' Therefore I have uttered that which I did not understand, Things too wonderful for me, which I didn't know.

Sikiliza, nakusihi, nami nitanena; Nitakuuliza neno, nawe niambie. Ayabu 42:4

You said, 'Listen, now, and I will speak; I will question you, and you will answer me.'

Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona. Ayabu 42:5

I had heard of you by the hearing of the ear, But now my eye sees you.

Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu. Ayabu 42:6

Therefore I abhor myself, And repent in dust and ashes."

Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. Ayabu 42:7

It was so, that after Yahweh had spoken these words to Job, Yahweh said to Eliphaz the Temanite, "My wrath is kindled against you, and against your two friends; for you have not spoken of me the thing that is right, as my servant Job has.

Basi sasa, jitwalieni ng'ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. Ayabu 42:8

Now therefore, take to yourselves seven bulls and seven rams, and go to my servant Job, and offer up for yourselves a burnt offering; and my servant Job shall pray for you, for I will accept him, that I not deal with you according to your folly. For you have not spoken of me the thing that is right, as my servant Job has."

Basi Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya kama vile Bwana alivyowaamuru; naye Bwana akamridhia Ayubu. Ayabu 42:9

So Eliphaz the Temanite and Bildad the Shuhite and Zophar the Naamathite went, and did what Yahweh commanded them, and Yahweh accepted Job.

Kisha Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza. Ayabu 42:10

Yahweh turned the captivity of Job, when he prayed for his friends. Yahweh gave Job twice as much as he had before.

Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote Bwana aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja. Ayabu 42:11

Then came there to him all his brothers, and all his sisters, and all those who had been of his acquaintance before, and ate bread with him in his house. They comforted him, and consoled him concerning all the evil that Yahweh had brought on him. Everyone also gave him a piece of money,{Literally, kesitah, a unit of money, probably silver} and everyone a ring of gold.

Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu, na punda wake elfu. Ayabu 42:12

So Yahweh blessed the latter end of Job more than his beginning. He had fourteen thousand sheep, six thousand camels, one thousand yoke of oxen, and a thousand female donkeys.

Tena alikuwa na wana waume saba, na binti watatu. Ayabu 42:13

He had also seven sons and three daughters.

Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima; na wa pili akamwita jina lake Kesia; na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu. Ayabu 42:14

He called the name of the first, Jemimah; and the name of the second, Keziah; and the name of the third, Keren Happuch.

Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri kama hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi kati ya ndugu zao wana waume. Ayabu 42:15

In all the land were no women found so beautiful as the daughters of Job. Their father gave them an inheritance among their brothers.

Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vinne. Ayabu 42:16

After this Job lived one hundred forty years, and saw his sons, and his sons' sons, to four generations.

Basi Ayubu akafa, mzee sana mwenye kujawa na siku. Ayabu 42:17

So Job died, being old and full of days.