1
Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
And the LORD said to Moses,
2
Walipize kisasi wana wa Israeli juu ya Wamidiani; kisha baadaye utakusanywa uwe pamoja na watu wako.
“Take vengeance on the Midianites for the Israelites. After that, you will be gathered to your people.”
3
Basi Musa akanena na watu, na kuwaambia, Wavikeni silaha watu miongoni mwenu waende vitani, ili waende kupigana na Midiani, wapate kumlipiza kisasi Bwana, juu ya Midiani.
So Moses told the people, “Arm some of your men for war, that they may go against the Midianites and execute the LORD’s vengeance on them.
4
Katika kila kabila mtatoa watu elfu, katika kabila zote za Israeli, nanyi mtawapeleka waende vitani.
Send into battle a thousand men from each tribe of Israel.”
5
Basi walitolewa katika maelfu ya Israeli, elfu moja ya kila kabila, watu waume kumi na mbili elfu walioandaliwa kwa vita.
So a thousand men were recruited from each tribe of Israel—twelve thousand armed for war.
6
Basi Musa akawapeleka, watu elfu wa kila kabila waende vitani, wao na Finehasi mwana wa Eleazari kuhani, waende vitani, na vile vyombo vya mahali patakatifu, na hizo tarumbeta za kupiga sauti za kugutusha mkononi mwake.
And Moses sent the thousand from each tribe into battle, along with Phinehas son of Eleazar the priest, who took with him the vessels of the sanctuary and the trumpets for signaling.
7
Nao wakapigana na Midiani kama Bwana alivyomwagiza Musa; nao wakamwua kila mume.
Then they waged war against Midian, as the LORD had commanded Moses, and they killed every male.
8
Nao wafalme wa Midiani wakawaua pamoja na watu wengine waliouawa; Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao wafalme watano wa Midiani; Balaamu mwana wa Beori naye wakamwua kwa upanga.
Among the slain were Evi, Rekem, Zur, Hur, and Reba—the five kings of Midian. They also killed Balaam son of Beor with the sword.
9
Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng'ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara.
The Israelites captured the Midianite women and their children, and they plundered all their herds, flocks, and goods.
10
Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na marago yao yote wakayateketeza kwa moto.
Then they burned all the cities where the Midianites had lived, as well as all their encampments,
11
Nao wakatwaa hizo nyara zote, na mateka yote, ya wanadamu na ya wanyama.
and carried away all the plunder and spoils, both people and animals.
12
Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo maragoni katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.
They brought the captives, spoils, and plunder to Moses, to Eleazar the priest, and to the congregation of Israel at the camp on the plains of Moab, by the Jordan across from Jericho.
13
Basi Musa, na Eleazari kuhani, na wakuu wote wa huo mkutano, wakatoka nje kwenda kuwalaki nje ya marago.
And Moses, Eleazar the priest, and all the leaders of the congregation went to meet them outside the camp.
14
Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao maakida wa elfu elfu, na wakuu wa mia mia, hao waliorudi kutoka katika kupiga vita.
But Moses was angry with the officers of the army—the commanders of thousands and commanders of hundreds—who were returning from the battle.
15
Musa akawauliza, Je! Mmewaponya wanawake wote hai?
“Have you spared all the women?” he asked them.
16
Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie Bwana dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa Bwana.
“Look, these women caused the sons of Israel, through the counsel of Balaam, to turn unfaithfully against the LORD at Peor, so that the plague struck the congregation of the LORD.
17
Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye.
So now, kill all the boys, as well as every woman who has had relations with a man,
18
Lakini hao watoto wote wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye, mtawaweka hai kwa ajili yenu.
but spare for yourselves every girl who has never had relations with a man.
19
Nanyi fanyeni matuo yenu nje ya marago muda wa siku saba; mtu awaye yote aliyemwua mtu, na awaye yote aliyemgusa mtu aliyeuawa, jitakaseni nafsi zenu siku ya tatu, na siku ya saba, ninyi na mateka yenu.
All of you who have killed a person or touched the dead are to remain outside the camp for seven days. On the third day and the seventh day you are to purify both yourselves and your captives.
20
Na katika habari ya kila nguo, na kila kitu kilichofanywa cha ngozi, na kazi yote ya singa za mbuzi, na vyombo vyote vilivyofanywa vya mti, mtajitakasa wenyewe;
And purify every garment and leather good, everything made of goat’s hair, and every article of wood.”
21
Kisha Eleazari kuhani akawaambia waume wa vita wote waliokwenda vitani, Hii ndiyo amri ya sheria Bwana aliyomwagiza Musa;
Then Eleazar the priest said to the soldiers who had gone into battle, “This is the statute of the law which the LORD has commanded Moses:
22
lakini dhahabu, na fedha, na shaba, na chuma, na bati, na risasi,
Only the gold, silver, bronze, iron, tin, and lead—
23
kila kitu kiwezacho kuuhimili moto, mtakipitisha katika moto, nacho kitakuwa safi, pamoja na haya kitatakaswa kwa hayo maji ya farakano; na kila kitu kisichouhimili moto mtakipitisha katika hayo maji.
everything that can withstand the fire—must be put through the fire, and it will be clean. But it must still be purified with the water of purification. And everything that cannot withstand the fire must pass through the water.
24
Nanyi mtazifua nguo zenu siku ya saba, nanyi mtakuwa safi, kisha baadaye mtaingia maragoni.
On the seventh day you are to wash your clothes, and you will be clean. After that you may enter the camp.”
25
Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
The LORD said to Moses,
26
Fanya jumla ya hayo mateka ya wanadamu, na ya wanyama pia, wewe, na Eleazari kuhani, na wakuu wa nyumba za baba za mkutano;
“You and Eleazar the priest and the family heads of the congregation are to take a count of what was captured, both of man and beast.
27
ukagawanye nyara mafungu mawili; kati ya watu waliozoea vita, waliotoka nje waende vitani, na huo mkutano wote;
Then divide the captives between the troops who went out to battle and the rest of the congregation.
28
kisha uwatoze hao watu wa vita waliotoka kwenda vitani sehemu kwa ajili ya Bwana; mmoja katika mia tano, katika wanadamu, na katika ng'ombe, na katika punda, na katika kondoo;
Set aside a tribute for the LORD from what belongs to the soldiers who went into battle: one out of every five hundred, whether persons, cattle, donkeys, or sheep.
29
twaa katika nusu yao, ukampe Eleazari kuhani, kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana.
Take it from their half and give it to Eleazar the priest as an offering to the LORD.
30
Na katika hiyo nusu ya wana wa Israeli utatwaa mmoja atakayetolewa katika kila hamsini, katika wanadamu, na katika ng'ombe, na katika punda, na katika kondoo, maana, katika wanyama wote, ukawape Walawi, hao walindao ulinzi wa maskani ya Bwana.
From the Israelites’ half, take one out of every fifty, whether persons, cattle, donkeys, sheep, or other animals, and give them to the Levites who keep charge of the tabernacle of the LORD.”
31
Musa na Eleazari kuhani wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Musa.
So Moses and Eleazar the priest did as the LORD had commanded Moses,
32
Basi masazo ya hizo nyara walizotwaa watu wa vita, zilikuwa ni kondoo mia sita na sabini na tano elfu,
and this plunder remained from the spoils the soldiers had taken: 675,000 sheep,
33
na ng'ombe sabini na mbili elfu,
72,000 cattle,
34
na punda sitini na moja elfu,
61,000 donkeys,
35
tena wanadamu jumla yao ilikuwa thelathini na mbili elfu, katika hao wanawake ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye.
and 32,000 women who had not slept with a man.
36
Na hiyo nusu ambayo ilikuwa ni sehemu ya hao waliotoka kwenda vitani, hesabu yake ilikuwa kondoo mia tatu na thelathini na saba elfu na mia tano;
This was the half portion for those who had gone to war: 337,500 sheep,
37
na kodi ya Bwana katika hao kondoo ilikuwa kondoo mia sita na sabini na watano.
including a tribute to the LORD of 675,
38
Tena, ng'ombe walikuwa thelathini na sita elfu; na katika hao kodi ya Bwana ilikuwa ng'ombe sabini na wawili.
36,000 cattle, including a tribute to the LORD of 72,
39
Na punda walikuwa thelathini elfuna mia tano, katika hao kodi ya Bwana ilikuwa punda sitini na mmoja.
30,500 donkeys, including a tribute to the LORD of 61,
40
Na wanadamu walikuwa watu kumi na sita elfu; katika hao sehemu ya Bwana ilikuwa ni watu thelathini na wawili.
and 16,000 people, including a tribute to the LORD of 32.
41
Basi Musa akampa Eleazari kuhani hiyo sehemu, iliyokuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Musa.
Moses gave the tribute to Eleazar the priest as an offering for the LORD, as the LORD had commanded Moses.
42
Tena katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, ambayo Musa aliitenga na watu waliokwenda vitani,
From the Israelites’ half, which Moses had set apart from the men who had gone to war,
43
(basi hiyo nusu ya mkutano ilikuwa ni kondoo mia tatu na thelathini na saba elfu na mia tano,
this half belonged to the congregation: 337,500 sheep,
44
na ng'ombe thelathini na sita elfu,
36,000 cattle,
45
na punda thelathini elfu, na mia tano,
30,500 donkeys,
46
na wanadamu kumi na sita elfu;)
and 16,000 people.
47
na katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, Musa akatwaa mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, wa binadamu na wa wanyama, akawapa Walawi, waliolinda ulinzi wa maskani ya Bwana; kama Bwana alivyomwagiza Musa.
From the Israelites’ half, Moses took one out of every fifty persons and animals and gave them to the Levites who kept charge of the tabernacle of the LORD, as the LORD had commanded him.
48
Na majemadari waliokuwa juu ya elfu elfu za hiyo jeshi, na maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, wakamkaribia Musa;
Then the officers who were over the units of the army—the commanders of thousands and of hundreds—approached Moses
49
wakamwambia Musa wakisema, Sisi watumishi wako tumefanya jumla ya hesabu ya watu wa vita walio chini ya mikono yetu, na hapana hata mmoja aliyetupungukia.
and said, “Your servants have counted the soldiers under our command, and not one of us is missing.
50
Nasi tumeleta matoleo ya Bwana, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za muhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele ya Bwana.
So we have brought to the LORD an offering of the gold articles each man acquired—armlets, bracelets, rings, earrings, and necklaces—to make atonement for ourselves before the LORD.”
51
Musa na Eleazari kuhani wakapokea kwao hiyo dhahabu, maana, vile vyombo vyote vilivyofanyizwa.
So Moses and Eleazar the priest received from them all the articles made out of gold.
52
Na dhahabu yote ya sadaka ya kuinuliwa waliyosongeza kwa Bwana, ya maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, ilikuwa shekeli kumi na sita elfu na mia saba na hamsini.
All the gold that the commanders of thousands and of hundreds presented as an offering to the LORD weighed 16,750 shekels.
53
(Kwa kuwa hao watu wa vita walikuwa wametwaa nyara, kila mtu nafsi yake.)
Each of the soldiers had taken plunder for himself.
54
Basi Musa na Eleazari kuhani wakapokea hiyo dhahabu mikononi mwa hao maakida wa elfu elfu na wa mia mia, na kuileta ndani ya hema ya kukutania, ili iwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za Bwana. </p>
And Moses and Eleazar the priest received the gold from the commanders of thousands and of hundreds and brought it into the Tent of Meeting as a memorial for the Israelites before the LORD.