Yoshua 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 4 (Swahili) Joshua 4 (English)

Ikawa, hapo hilo taifa zima lilipokuwa limekwisha vuka Yordani, ndipo Bwana akanena na Yoshua, akamwambia, Yoshua 4:1

It happened, when all the nation were clean passed over the Jordan, that Yahweh spoke to Joshua, saying,

Haya, twaeni watu waume kumi na wawili katika hao watu, kila kabila mtu mmoja, Yoshua 4:2

Take twelve men out of the people, out of every tribe a man,

kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende nayo mawe hayo, mkayaweke nchi kambini, hapo mtakapolala usiku huu. Yoshua 4:3

and command you them, saying, Take hence out of the midst of the Jordan, out of the place where the priests' feet stood firm, twelve stones, and carry them over with you, and lay them down in the lodging-place, where you shall lodge this night.

Basi Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili, aliokuwa amewaweka tayari tangu hapo, katika wana wa Israeli, kila kabila mtu mmoja; Yoshua 4:4

Then Joshua called the twelve men, whom he had prepared of the children of Israel, out of every tribe a man:

naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la Bwana, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli; Yoshua 4:5

and Joshua said to them, Pass over before the ark of Yahweh your God into the midst of the Jordan, and take up every man of you a stone on his shoulder, according to the number of the tribes of the children of Israel;

ili kwamba jambo hili liwe ishara kati yenu, hapo watoto wenu watakapowauliza ninyi katika siku zijazo, wakisema, Ni nini maana yake mawe haya? Yoshua 4:6

that this may be a sign among you, that when your children ask in time to come, saying, What do you mean by these stones?

Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yalitindika mbele ya sanduku la agano la Bwana; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalitindika; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele. Yoshua 4:7

then you shall tell them, Because the waters of the Jordan were cut off before the ark of the covenant of Yahweh; when it passed over the Jordan, the waters of the Jordan were cut off: and these stones shall be for a memorial to the children of Israel forever.

Basi wana wa Israeli walifanya vile vile kama Yoshua alivyowaamuru, nao wakatwaa mawe kumi na mawili pale katikati ya Yordani, kama Bwana alivyomwambia Yoshua, sawasawa na hesabu ya kabila za wana wa Israeli; wakayachukua wakavuka nayo hata mahali pale walipolala, nao wakayaweka nchi kuko huko. Yoshua 4:8

The children of Israel did so as Joshua commanded, and took up twelve stones out of the midst of the Jordan, as Yahweh spoke to Joshua, according to the number of the tribes of the children of Israel; and they carried them over with them to the place where they lodged, and laid them down there.

Kisha Yoshua akapanga mawe kumi na mawili katikati ya Yordani, mahali pale miguu ya hao makuhani waliolichukua hilo sanduku la agano iliposimama; nayo yapo pale pale hata hivi leo. Yoshua 4:9

Joshua set up twelve stones in the midst of the Jordan, in the place where the feet of the priests who bore the ark of the covenant stood: and they are there to this day.

Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hata mambo yote Bwana aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka. Yoshua 4:10

For the priests who bore the ark stood in the midst of the Jordan, until everything was finished that Yahweh commanded Joshua to speak to the people, according to all that Moses commanded Joshua: and the people hurried and passed over.

Ikawa watu wote walipokuwa wamekwisha vuka kabisa, hilo sanduku la Bwana likavuka, na hao makuhani, mbele ya macho ya hao watu. Yoshua 4:11

It happened, when all the people had completely passed over, that the ark of Yahweh passed over, with the priests, in the presence of the people.

Na wana wa Reubeni, na wana wa Gadi na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wakavuka, hali ya kuvaa silaha mbele ya wana wa Israeli, kama Musa alivyowaambia; Yoshua 4:12

The children of Reuben, and the children of Gad, and the half-tribe of Manasseh, passed over armed before the children of Israel, as Moses spoke to them:

walipata kama watu arobaini elfu hesabu yao, wenye kuvaa silaha tayari kwa vita, waliovuka mbele ya Bwana, waende vitani, hata nchi tambarare za Yeriko. Yoshua 4:13

about forty thousand ready armed for war passed over before Yahweh to battle, to the plains of Jericho.

Siku ile Bwana alimtukuza Yoshua mbele ya macho ya Israeli wote; nao wakamcha, kama walivyokuwa wakimcha Musa, siku zote za maisha yake. Yoshua 4:14

On that day Yahweh magnified Joshua in the sight of all Israel; and they feared him, as they feared Moses, all the days of his life.

Kisha Bwana akanena na Yoshua, akamwambia, Yoshua 4:15

Yahweh spoke to Joshua, saying,

Haya, uwaamuru makuhani, hao waliolichukua sanduku la ushuhuda, kwamba wakwee juu kutoka mle katika Yordani. Yoshua 4:16

Command the priests who bear the ark of the testimony, that they come up out of the Jordan.

Basi Yoshua akawaamuru hao makuhani, akawaambia, Haya, kweeni mtoke Yordani. Yoshua 4:17

Joshua therefore commanded the priests, saying, Come up out of the Jordan.

Ilikuwa, hapo hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana walipokwea juu kutoka mle kati ya Yordani, na nyayo za miguu yao hao makuhani zilipoinuliwa na kutiwa katika nchi kavu, ndipo maji ya Yordani yaliporudi mahali pake, na kujaa na kuipita mipaka yake, kama yalivyokuwa hapo kwanza. Yoshua 4:18

It happened, when the priests who bore the ark of the covenant of Yahweh were come up out of the midst of the Jordan, and the soles of the priests' feet were lifted up to the dry ground, that the waters of the Jordan returned to their place, and went over all its banks, as before.

Na hao watu wakakwea kutoka Yordani siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi Gilgali, katika mpaka wa mashariki wa Yeriko. Yoshua 4:19

The people came up out of the Jordan on the tenth day of the first month, and encamped in Gilgal, on the east border of Jericho.

Na yale mawe kumi na mawili waliyoyatwaa katikati ya Yordani Yoshua akayasimamisha Gilgali. Yoshua 4:20

Those twelve stones, which they took out of the Jordan, did Joshua set up in Gilgal.

Akawaambia wana wa Israeli, akasema, Watoto wenu watakapowauliza baba zao katika siku zijazo, wakisema, Mawe haya maana yake ni nini? Yoshua 4:21

He spoke to the children of Israel, saying, When your children shall ask their fathers in time to come, saying, What mean these stones?

Ndipo mtakapowaarifu watoto wenu mkisema, Israeli walivuka mto huu wa Yordani, kwa njia ya nchi kavu. Yoshua 4:22

Then you shall let your children know, saying, Israel came over this Jordan on dry land.

Kwa sababu Bwana, Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mbele yenu, hata mlipokwisha kuvuka kama Bwana, Mungu wenu, alivyoitenda Bahari ya Shamu, aliyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka; Yoshua 4:23

For Yahweh your God dried up the waters of the Jordan from before you, until you were passed over, as Yahweh your God did to the Red Sea, which he dried up from before us, until we were passed over;

watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa Bwana, ya kuwa ni mkono wenye uweza, ili wamche Bwana, Mungu wenu, milele. Yoshua 4:24

that all the peoples of the earth may know the hand of Yahweh, that it is mighty; that you may fear Yahweh your God forever.