Yoshua 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 11 (Swahili) Joshua 11 (English)

Kisha ikawa, hapo huyo Yabini, mfalme wa Hazori, aliposikia habari ya mambo hayo, akatuma mjumbe aende kwa Yobabu, mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni, na mfalme wa Akshafu, Yoshua 11:1

It happened, when Jabin king of Hazor heard of it, that he sent to Jobab king of Madon, and to the king of Shimron, and to the king of Achshaph,

na hao wafalme waliokuwa upande wa kaskazini, katika nchi ya vilima, na katika Araba upande wa kusini wa Kinerethi, na katika Shefela, na katika nchi zilizoinuka za Dori upande wa magharibi, Yoshua 11:2

and to the kings who were on the north, in the hill-country, and in the Arabah south of Chinneroth, and in the lowland, and in the heights of Dor on the west,

na kwa Mkanaani upande wa mashariki, na upande wa magharibi, na kwa Mwamori, na Mhiti, na Mperizi na Myebusi katika nchi ya vilima, na kwa Mhivi pale chini ya Hermoni katika nchi ya Mispa. Yoshua 11:3

to the Canaanite on the east and on the west, and the Amorite, and the Hittite, and the Perizzite, and the Jebusite in the hill-country, and the Hivite under Hermon in the land of Mizpah.

Nao wakatoka nje, wao na jeshi zao zote pamoja nao, watu wengi mno, kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi, pamoja na farasi na magari mengi sana. Yoshua 11:4

They went out, they and all their hosts with them, much people, even as the sand that is on the sea-shore in multitude, with horses and chariots very many.

Wafalme hao wote wakakutana pamoja; wakaenda na kupanga mahema yao pamoja hapo penye maji ya Meromu, ili kupigana na Israeli. Yoshua 11:5

All these kings met together; and they came and encamped together at the waters of Merom, to fight with Israel.

Bwana akamwambia Yoshua, Usiche wewe kwa ajili ya hao; kwani kesho wakati kama huu nitawatoa hali wameuawa wote mbele ya Israeli; utawatema farasi zao, na magari yao utayapiga moto. Yoshua 11:6

Yahweh said to Joshua, Don't be afraid because of them; for tomorrow at this time will I deliver them up all slain before Israel: you shall hamstring their horses, and burn their chariots with fire.

Basi Yoshua akaenda, na watu wote wa vita pamoja naye, ili kupigana nao hapo penye maji ya Meromu ghafula; wakawaangukia. Yoshua 11:7

So Joshua came, and all the people of war with him, against them by the waters of Merom suddenly, and fell on them.

Bwana akawatia mkononi mwa Israeli, nao wakawapiga, na kuwafukuza hata kufikilia Sidoni ulio mkuu, na hata kufikilia Misrefoth-maimu, tena hata kufikilia bonde la Mispa upande wa mashariki; wakawapiga hata wasiwasaze hata mtu mmoja aliyesalia. Yoshua 11:8

Yahweh delivered them into the hand of Israel, and they struck them, and chased them to great Sidon, and to Misrephoth Maim, and to the valley of Mizpeh eastward; and they struck them, until they left them none remaining.

Yoshua akawafanyia vile vile kama Bwana alivyomwamuru; akawatema farasi zao, na magari yao akayapiga moto. Yoshua 11:9

Joshua did to them as Yahweh bade him: he hamstrung their horses, and burnt their chariots with fire.

Yoshua akarudi wakati huo na kuutwaa Hazori, akampiga mfalme wa Hazori kwa upanga; kwa kuwa Hazori hapo kwanza ulikuwa ni kichwa cha falme hizo zote. Yoshua 11:10

Joshua turned back at that time, and took Hazor, and struck the king of it with the sword: for Hazor before was the head of all those kingdoms.

Nao wakawapiga wote pia waliokuwamo ndani ya Hazori kwa makali ya upanga, wakawaangamiza kabisa; hakusazwa hata mmoja aliyevuta pumzi; kisha akauteketeza Hazori kwa moto. Yoshua 11:11

They struck all the souls who were therein with the edge of the sword, utterly destroying them; there was none left who breathed: and he burnt Hazor with fire.

Tena miji yote ya wafalme hao, na wafalme wake wote, Yoshua akawatwaa, akawapiga kwa makali ya upanga, na kuwaangamiza kabisa; vile vile kama huyo Musa mtumishi wa Bwana alivyomwamuru. Yoshua 11:12

All the cities of those kings, and all the kings of them, did Joshua take, and he struck them with the edge of the sword, and utterly destroyed them; as Moses the servant of Yahweh commanded.

Lakini katika habari ya miji hiyo iliyosimama katika vilima vyao, Israeli hawakuipiga moto miji hiyo, isipokuwa ni mji wa Hazori tu; mji huo Yoshua aliupiga moto. Yoshua 11:13

But as for the cities that stood on their mounds, Israel burned none of them, save Hazor only; that did Joshua burn.

Tena nyara zote za miji hiyo, na wanyama wa miji, wana wa Israeli walitwaa kuwa nyara zao wenyewe; lakini kila mtu wakampiga kwa makali ya upanga, hata walipokuwa wamewaangamiza wote, wala hawakumsaza mmoja mwenye kuvuta pumzi. Yoshua 11:14

All the spoil of these cities, and the cattle, the children of Israel took for a prey to themselves; but every man they struck with the edge of the sword, until they had destroyed them, neither left they any who breathed.

Vile vile kama Bwana alivyomwamuru Musa mtumishi wake, ndivyo Musa alivyomwamuru Yoshua; naye Yoshua akafanya vivyo; hakukosa kufanya neno lo lote katika hayo yote Bwana aliyomwamuru Musa. Yoshua 11:15

As Yahweh commanded Moses his servant, so did Moses command Joshua: and so did Joshua; he left nothing undone of all that Yahweh commanded Moses.

Hivyo Yoshua akatwaa nchi hiyo yote, hiyo nchi ya vilima, na nchi yote ya Negebu, na nchi yote ya Gosheni, na hiyo Shefela, na hiyo Araba na nchi ya vilima vilima ya Israeli, na hiyo nchi tambarare; Yoshua 11:16

So Joshua took all that land, the hill-country, and all the South, and all the land of Goshen, and the lowland, and the Arabah, and the hill-country of Israel, and the lowland of the same;

tangu kilima cha Halaki, kiendeleacho upande wa Seiri, mpaka Baal-gadi katika bonde la Lebanoni chini ya kilima cha Hermoni; naye akawatwaa wafalme wao wote, akawapiga, na kuwaua. Yoshua 11:17

from Mount Halak, that goes up to Seir, even to Baal Gad in the valley of Lebanon under Mount Hermon: and all their kings he took, and struck them, and put them to death.

Yoshua akapiga vita siku nyingi na wafalme hao wote. Yoshua 11:18

Joshua made war a long time with all those kings.

Haukuwapo mji hata mmoja uliofanya amani na wana wa Israeli, isipokuwa ni wale Wahivi wenye kukaa Gibeoni; wakaitwaa yote vitani. Yoshua 11:19

There was not a city that made peace with the children of Israel, save the Hivites the inhabitants of Gibeon: they took all in battle.

Kwa kuwa lilikuwa ni la Bwana kuifanya mioyo yao kuwa migumu, hata wakatoka kupigana na Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, wasihurumiwe lakini apate kuwaangamiza, kama vile Bwana alivyomwamuru Musa. Yoshua 11:20

For it was of Yahweh to harden their hearts, to come against Israel in battle, that he might utterly destroy them, that they might have no favor, but that he might destroy them, as Yahweh commanded Moses.

Wakati huo Yoshua akaenda na kuwakatilia mbali hao Waanaki watoke nchi ya vilima, kutoka Hebroni, na kutoka Debiri, na kutoka Anabu, na kutoka katika nchi yote ya vilima vilima ya Yuda, na kutoka katika nchi yote ya vilima vilima ya Israeli; Yoshua akawaangamiza kabisa na miji yao. Yoshua 11:21

Joshua came at that time, and cut off the Anakim from the hill-country, from Hebron, from Debir, from Anab, and from all the hill-country of Judah, and from all the hill-country of Israel: Joshua utterly destroyed them with their cities.

Hawakusalia Waanaki hata mmoja katika nchi ya wana wa Israeli; isipokuwa katika Gaza, na katika Gathi, na katika Ashdodi walisalia. Yoshua 11:22

There was none of the Anakim left in the land of the children of Israel: only in Gaza, in Gath, and in Ashdod, did some remain.

Basi Yoshua akaitwaa hiyo nchi yote, sawasawa na hayo yote Bwana aliyokuwa amemwambia Musa; Yoshua naye akawapa Israeli kuwa ni urithi wao, sawasawa na walivyogawanyikana kwa kabila zao. Kisha nchi ikatulia isiwe na vita tena. Yoshua 11:23

So Joshua took the whole land, according to all that Yahweh spoke to Moses; and Joshua gave it for an inheritance to Israel according to their divisions by their tribes. The land had rest from war.