Yoshua 24 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 24 (Swahili) Joshua 24 (English)

Yoshua akawakusanya kabila zote za Israeli huko Shekemu, akawaita wazee wa Israeli, na wakuu wao, na waamuzi wao, na maakida wao nao wakahudhuria mbele za Mungu. Yoshua 24:1

Joshua gathered all the tribes of Israel to Shechem, and called for the elders of Israel, and for their heads, and for their judges, and for their officers; and they presented themselves before God.

Yoshua akawaambia watu wote, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Baba zenu hapo zamani walikaa ng'ambo ya Mto, maana Tera, baba yake Ibrahimu, naye ni baba yake Nahori; wakaitumikia miungu mingine. Yoshua 24:2

Joshua said to all the people, Thus says Yahweh, the God of Israel, Your fathers lived of old time beyond the River, even Terah, the father of Abraham, and the father of Nahor: and they served other gods.

Nami nikamtwaa Ibrahimu baba yenu toka ng'ambo ya Mto, nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani; nikaongeza uzao wake, nikampa Isaka. Yoshua 24:3

I took your father Abraham from beyond the River, and led him throughout all the land of Canaan, and multiplied his seed, and gave him Isaac.

Kisha nikampa huyo Isaka, Yakobo na Esau; nami nikampa Esau mlima Seiri aumiliki; Yakobo na watoto wake wakashuka Misri. Yoshua 24:4

I gave to Isaac Jacob and Esau: and I gave to Esau Mount Seir, to possess it: and Jacob and his children went down into Egypt.

Kisha nikawatuma Musa na Haruni nikaipiga nchi ya Misri, kwa hayo yote niliyoyatenda kati yake; hatimaye nikawatoa ninyi. Yoshua 24:5

I sent Moses and Aaron, and I plagued Egypt, according to that which I did in the midst of it: and afterward I brought you out.

Nikawatoa baba zenu watoke Misri; nanyi mkaifikilia bahari; Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka bahari ya Shamu. Yoshua 24:6

I brought your fathers out of Egypt: and you came to the sea; and the Egyptians pursued after your fathers with chariots and with horsemen to the Red Sea.

Nao walipomlilia Bwana, akaweka giza kati ya ninyi na Wamisri, akaileta bahari juu yao, akawafunikiza; nayo macho yenu yaliyaona mambo niliyoyatenda huko Misri; kisha mkakaa jangwani siku nyingi. Yoshua 24:7

When they cried out to Yahweh, he put darkness between you and the Egyptians, and brought the sea on them, and covered them; and your eyes saw what I did in Egypt: and you lived in the wilderness many days.

Kisha nikawaleta na kuwaingiza katika nchi ya Waamori waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani; nao wakapigana nanyi; nikawatia mikononi mwenu, mkaimiliki nchi yao; nami nikawaangamiza mbele yenu. Yoshua 24:8

I brought you into the land of the Amorites, that lived beyond the Jordan: and they fought with you; and I gave them into your hand, and you possessed their land; and I destroyed them from before you.

Ndipo Balaki, mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, akainuka, akapigana na Israeli; tena akatuma watu akamwita Balaamu, mwana wa Beori, aje awalaani; Yoshua 24:9

Then Balak the son of Zippor, king of Moab, arose and fought against Israel: and he sent and called Balaam the son of Beor to curse you;

lakini sikukubali kumsikiliza Balaamu; kwa hiyo akafuliza kuwabarikia ninyi; basi nikawatoa katika mkono wake. Yoshua 24:10

but I would not listen to Balaam; therefore he blessed you still: so I delivered you out of his hand.

Nanyi mliuvuka Yordani, mkafika Yeriko; nao watu wa Yeriko wakapigana nanyi, Mwamori, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhiti, na Mgirgashi, na Mhivi, na Myebusi; nami nikawatia mikononi mwenu. Yoshua 24:11

You went over the Jordan, and came to Jericho: and the men of Jericho fought against you, the Amorite, and the Perizzite, and the Canaanite, and the Hittite, and the Girgashite, the Hivite, and the Jebusite; and I delivered them into your hand.

Nikatuma mavu mbele yenu, waliowafukuza mbele yenu hao wafalme wawili wa Waamori, si kwa upanga wako, wala kwa upinde wako. Yoshua 24:12

I sent the hornet before you, which drove them out from before you, even the two kings of the Amorites; not with your sword, nor with your bow.

Nami nimewapa ninyi nchi msiyoitendea kazi, na miji msiyoijenga, nanyi mmekaa humo; mnakula matunda ya mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda. Yoshua 24:13

I gave you a land whereon you had not labored, and cities which you didn't build, and you dwell therein; of vineyards and olive groves which you didn't plant do you eat.

Basi sasa mcheni Bwana, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye Bwana. Yoshua 24:14

Now therefore fear Yahweh, and serve him in sincerity and in truth; and put away the gods which your fathers served beyond the River, and in Egypt; and serve you Yahweh.

Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana. Yoshua 24:15

If it seem evil to you to serve Yahweh, choose you this day whom you will serve; whether the gods which your fathers served that were beyond the River, or the gods of the Amorites, in whose land you dwell: but as for me and my house, we will serve Yahweh.

Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache Bwana, ili kuitumikia miungu mingine; Yoshua 24:16

The people answered, Far be it from us that we should forsake Yahweh, to serve other gods;

kwa maana Bwana, Mungu wetu, yeye ndiye aliyetupandisha sisi na baba zetu kutoka nchi ya Misri; kutoka nyumba ya utumwa; naye ndiye aliyezifanya ishara zile kubwa mbele ya macho yetu, na kutulinda katika njia ile yote tuliyoiendea, na kati ya watu wa mataifa yote tuliopita katikati yao. Yoshua 24:17

for Yahweh our God, he it is who brought us and our fathers up out of the land of Egypt, from the house of bondage, and who did those great signs in our sight, and preserved us in all the way in which we went, and among all the peoples through the midst of whom we passed;

Bwana ndiye aliyewafukuza watu wa mataifa yote watoke mbele yetu, naam, Waamori waliokaa katika nchi hii; basi, kwa sababu hiyo sisi nasi tutamtumikia Bwana, maana yeye ndiye Mungu wetu. Yoshua 24:18

and Yahweh drove out from before us all the peoples, even the Amorites who lived in the land: therefore we also will serve Yahweh; for he is our God.

Yoshua akawaambia watu, Hamwezi kumtumikia Bwana; kwa kuwa yeye ni Mungu mtakatifu; yeye ni Mungu mwenye wivu; hatawasamehe makosa yenu, wala dhambi zenu. Yoshua 24:19

Joshua said to the people, You can't serve Yahweh; for he is a holy God; he is a jealous God; he will not forgive your disobedience nor your sins.

Kama mkimwacha Bwana na kuitumikia miungu migeni, ndipo atageuka na kuwatenda mabaya na kuwaangamiza, baada ya kuwatendea mema. Yoshua 24:20

If you forsake Yahweh, and serve foreign gods, then he will turn and do you evil, and consume you, after that he has done you good.

Lakini hao watu wakamwambia Yoshua, La! Lakini tutamtumikia Bwana. Yoshua 24:21

The people said to Joshua, No; but we will serve Yahweh.

Yoshua akawaambia watu, Ninyi mmekuwa mashahidi juu ya nafsi zenu, ya kuwa mmemchagua Bwana, ili kumtumikia yeye. Wakasema, Sisi tu mashahidi. Yoshua 24:22

Joshua said to the people, You are witnesses against yourselves that you have chosen you Yahweh, to serve him. They said, We are witnesses.

Akasema, Basi sasa, iondoeni miungu migeni iliyo kati yenu, mkaielekeze mioyo yenu kwa Bwana, Mungu wa Israeli. Yoshua 24:23

Now therefore put away, [said he], the foreign gods which are among you, and incline your heart to Yahweh, the God of Israel.

Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, Bwana, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii. Yoshua 24:24

The people said to Joshua, Yahweh our God will we serve, and to his voice will we listen.

Basi Yoshua akafanya agano na wale watu siku ile, akawapa amri na agizo huko Shekemu. Yoshua 24:25

So Joshua made a covenant with the people that day, and set them a statute and an ordinance in Shechem.

Yoshua akayaandika maneno haya katika kitabu cha torati ya Mungu; kisha akatwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko, chini ya ule mwaloni uliokuwa karibu na patakatifu pa Bwana. Yoshua 24:26

Joshua wrote these words in the book of the law of God; and he took a great stone, and set it up there under the oak that was by the sanctuary of Yahweh.

Yoshua akawaambia watu wote, Tazama, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya Bwana aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu. Yoshua 24:27

Joshua said to all the people, Behold, this stone shall be a witness against us; for it has heard all the words of Yahweh which he spoke to us: it shall be therefore a witness against you, lest you deny your God.

Basi Yoshua akawaruhusu watu, wakaenda zao, kila mtu kwenye urithi wake. Yoshua 24:28

So Joshua sent the people away, every man to his inheritance.

Ikawa, baada ya hayo, Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa, mwenye umri wa miaka mia na kumi. Yoshua 24:29

It happened after these things, that Joshua the son of Nun, the servant of Yahweh, died, being one hundred ten years old.

Wakamzika katika mpaka wa urithi wake, huko Timnath-sera; ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi. Yoshua 24:30

They buried him in the border of his inheritance in Timnathserah, which is in the hill-country of Ephraim, on the north of the mountain of Gaash.

Nao Israeli wakamtumikia Bwana siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioishi baada ya kufa kwake Yoshua, hao walioijua kazi yote ya Bwana, aliyowatendea Israeli. Yoshua 24:31

Israel served Yahweh all the days of Joshua, and all the days of the elders who outlived Joshua, and had known all the work of Yahweh, that he had worked for Israel.

Na hiyo mifupa ya Yusufu, ambayo wana wa Israeli walikuwa wameileta kutoka Misri, wakaizika huko Shekemu katika ile sehemu ya nchi, Yakobo aliyoinunua kwa wana wa Hamori, babaye Shekemu, kwa vipande mia vya fedha; nayo ikawa ni urithi wa wana wa Yusufu. Yoshua 24:32

The bones of Joseph, which the children of Israel brought up out of Egypt, buried they in Shechem, in the parcel of ground which Jacob bought of the sons of Hamor the father of Shechem for a hundred pieces of money: and they became the inheritance of the children of Joseph.

Huyo Eleazari mwana wa Haruni naye akafa; wakamzika katika kilima cha Finehasi mwanawe, ambacho alipewa yeye katika nchi ya vilima ya Efraimu. Yoshua 24:33

Eleazar the son of Aaron died; and they buried him in the hill of Phinehas his son, which was given him in the hill-country of Ephraim.