Yoshua 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 8 (Swahili) Joshua 8 (English)

Kisha Bwana akamwambia Yoshua, Usiche, wala usifadhaike; wachukue watu wote wa vita waende pamoja nawe, nanyi inukeni, mwende Ai, angalia, mimi nimemtia mkononi mwako huyo mfalme wa Ai, na watu wake, na mji wake, na nchi yake; Yoshua 8:1

Yahweh said to Joshua, Don't be afraid, neither be dismayed: take all the people of war with you, and arise, go up to Ai; behold, I have given into your hand the king of Ai, and his people, and his city, and his land;

nawe utautenda mji wa Ai na mfalme wake kama ulivyoutenda mji wa Yeriko na mfalme wake; lakini nyara zake na wanyama wake wa mji mtavitwaa kuwa mateka yenu wenyewe; huo mji uuwekee waoteaji upande wa nyuma. Yoshua 8:2

You shall do to Ai and her king as you did to Jericho and her king: only the spoil of it, and the cattle of it, shall you take for a prey to yourselves: set you an ambush for the city behind it.

Basi Yoshua akainuka, na watu wote wa vita pamoja naye, ili waende Ai; Yoshua akachagua watu thelathini elfu, watu mashujaa wenye uwezo, akawapeleka wakati wa usiku. Yoshua 8:3

So Joshua arose, and all the people of war, to go up to Ai: and Joshua chose out thirty thousand men, the mighty men of valor, and sent them forth by night.

Akawaagiza, akasema, Angalieni, mtaotea kuuvizia ule mji, upande wa nyuma wa mji; msiende mbali sana na mji, lakini kaeni tayari nyote; Yoshua 8:4

He commanded them, saying, Behold, you shall lie in ambush against the city, behind the city; don't go very far from the city, but be all ready:

na mimi, na watu wote walio pamoja nami, tutaukaribia mji; kisha itakuwa, hapo watakapotoka nje kupigana nasi, kama walivyofanya hapo kwanza, sisi tutakimbia mbele yao; Yoshua 8:5

and I, and all the people who are with me, will approach to the city. It shall happen, when they come out against us, as at the first, that we will flee before them;

nao watatoka nje watufuate, hata tuwavute waende mbali na mji wao; kwa kuwa watasema, Wakimbia mbele yetu, kama walivyofanya kwanza; nasi tutakimbia mbele yao; Yoshua 8:6

and they will come out after us, until we have drawn them away from the city; for they will say, They flee before us, as at the first: so we will flee before them;

basi ninyi mtainuka mtoke hapo mwoteapo, na kuushika mji; kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, atautia mikononi mwenu. Yoshua 8:7

and you shall rise up from the ambush, and take possession of the city: for Yahweh your God will deliver it into your hand.

Kisha itakuwa, mtakapoushika mji, ndipo mtauteketeza mji kwa moto; sawasawa na hilo neno la Bwana; angalieni, nimewaagiza. Yoshua 8:8

It shall be, when you have seized on the city, that you shall set the city on fire; according to the word of Yahweh shall you do: behold, I have commanded you.

Basi Yoshua akawatuma; nao wakaenda hata hapo watakapootea, wakakaa kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa Ai; lakini Yoshua akalala usiku huo kati ya watu. Yoshua 8:9

Joshua sent them forth; and they went to set up the ambush, and stayed between Bethel and Ai, on the west side of Ai: but Joshua lodged that night among the people.

Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakutanisha watu, kisha akatangulia kukwea kwenda Ai mbele ya hao watu, yeye na wazee wa Israeli. Yoshua 8:10

Joshua arose up early in the morning, and mustered the people, and went up, he and the elders of Israel, before the people to Ai.

Watu wote, hao wa vita, waliokuwa pamoja naye, wakaenda wakakaribia, na kufikilia mbele ya mji, wakatua upande wa kaskazini wa Ai; napo palikuwa na bonde kati ya yeye na Ai. Yoshua 8:11

All the people, [even] the [men of] war who were with him, went up, and drew near, and came before the city, and encamped on the north side of Ai: now there was a valley between him and Ai.

Kisha akatwaa watu kama elfu tano, akawaweka kuotea kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa huo mji. Yoshua 8:12

He took about five thousand men, and set them in ambush between Bethel and Ai, on the west side of the city.

Basi wakawaweka hao watu, jeshi zima lililokuwa upande wa kaskazini wa mji, na wale waliokuwa waotea upande wa magharibi wa mji; naye Yoshua akaenda usiku huo katikati ya hilo bonde. Yoshua 8:13

So they set the people, even all the host who was on the north of the city, and their liers-in-wait who were on the west of the city; and Joshua went that night into the midst of the valley.

Kisha ikawa hapo huyo mfalme wa Ai alipoona jambo hilo, ndipo walipofanya haraka, na wakaamka asubuhi na mapema, na watu waume wa mji wakatoka nje waende kupigana na Israeli, yeye na watu wake wote, kwa wakati ulioamriwa, kuikabili Araba; lakini hakujua ya kwamba walikuwako waviziao kinyume chake kwa upande wa nyuma wa mji. Yoshua 8:14

It happened, when the king of Ai saw it, that they hurried and rose up early, and the men of the city went out against Israel to battle, he and all his people, at the time appointed, before the Arabah; but he didn't know that there was an ambush against him behind the city.

Kisha Yoshua na watu wa Israeli wote walifanya kana kwamba wameshindwa mbele yao, wakakimbia kwa njia ya nyika. Yoshua 8:15

Joshua and all Israel made as if they were beaten before them, and fled by the way of the wilderness.

Watu wote waliokuwa ndani ya mji waliitwa wakusanyike pamoja ili kuwafuatia; nao wakamfuatia Yoshua, wakasongea mbele na kuuacha mji. Yoshua 8:16

All the people who were in the city were called together to pursue after them: and they pursued after Joshua, and were drawn away from the city.

Hakusalia mtu ye yote ndani ya Ai, au katika Betheli, asiyetoka nje kuwafuatia Israeli; wakauacha mji wazi na kuwafuatia Israeli. Yoshua 8:17

There was not a man left in Ai or Beth El, who didn't go out after Israel: and they left the city open, and pursued after Israel.

Kisha Bwana akamwambia Yoshua, Haya, unyoshe huo mkuki ulio nao mkononi mwako, uuelekeze upande wa Ai; kwa kuwa nitautia mkononi mwako. Basi Yoshua akaunyosha huo mkuki uliokuwa mkononi mwake kuuelekea huo mji. Yoshua 8:18

Yahweh said to Joshua, Stretch out the javelin that is in your hand toward Ai; for I will give it into your hand. Joshua stretched out the javelin that was in his hand toward the city.

Wale watu waliovizia wakainuka kwa upesi kutoka mahali pao, nao wakapiga mbio mara hapo alipokuwa amekwisha unyosha mkono wake, wakaingia ndani ya mji, na kuushika; nao wakafanya haraka kuuteketeza kwa moto huo mji. Yoshua 8:19

The ambush arose quickly out of their place, and they ran as soon as he had stretched out his hand, and entered into the city, and took it; and they hurried and set the city on fire.

Kisha hapo hao watu wa Ai walipotazama nyuma yao, wakaona, na tazama, moshi wa huo mji ulikuwa unapaa juu kwenda mawinguni, nao hawakuwa na nguvu za kukimbia huku wala huku; na wale watu waliokuwa wamekimbia kuenenda nyikani wakageuka na kuwarudia hao waliokuwa wakiwafuatia. Yoshua 8:20

When the men of Ai looked behind them, they saw, and, behold, the smoke of the city ascended up to heaven, and they had no power to flee this way or that way: and the people who fled to the wilderness turned back on the pursuers.

Basi hapo Yoshua na Israeli wote walipoona ya kwamba hao waliovizia wamekwisha kuushika huo mji, na ya kwamba moshi wa mji umepaa juu, ndipo wakageuka tena, na kuwaua watu wa Ai. Yoshua 8:21

When Joshua and all Israel saw that the ambush had taken the city, and that the smoke of the city ascended, then they turned again, and killed the men of Ai.

Tena hao; wengine wakatoka nje kuutoka huo mji kinyume chao; basi hivyo walikuwa wa katikati ya Israeli, wengine upande huu na wengine upande huu; nao wakawapiga, hata wasimwache hata mmoja miongoni mwao aliyesalia, wala kupona. Yoshua 8:22

The others came forth out of the city against them; so they were in the midst of Israel, some on this side, and some on that side: and they struck them, so that they let none of them remain or escape.

Kisha wakamshika mfalme wa Ai ali hai, nao wakamleta kwa Yoshua. Yoshua 8:23

The king of Ai they took alive, and brought him to Joshua.

Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamekwisha kuwaua wenyeji wote wa Ai katika bara, hapo katika nyika walipokuwamo wakiwafuatia, nao walikuwa wamekwisha anguka wote kwa makali ya upanga, hata walipokuwa wameangamizwa wote, ndipo Israeli wakarejea Ai, na kuupiga huo mji kwa makali ya upanga. Yoshua 8:24

It happened, when Israel had made an end of killing all the inhabitants of Ai in the field, in the wilderness in which they pursued them, and they were all fallen by the edge of the sword, until they were consumed, that all Israel returned to Ai, and struck it with the edge of the sword.

Wote walioanguka siku hiyo waume kwa wake, walikuwa ni kumi na mbili elfu, yaani, watu wote wa mji wa Ai. Yoshua 8:25

All that fell that day, both of men and women, were twelve thousand, even all the men of Ai.

Kwani huyo Yoshua hakuuzuia mkono wake, huo ulionyosha huo mkuki, hata hapo alipokuwa amewaangamiza kabisa wenyeji wote wa Ai. Yoshua 8:26

For Joshua didn't draw back his hand, with which he stretched out the javelin, until he had utterly destroyed all the inhabitants of Ai.

Isipokuwa wanyama wa mji na nyara za mji Israeli wakatwaa wenyewe kuwa ni mapato yao, sawasawa na hilo neno la Bwana alilomwamuru Yoshua. Yoshua 8:27

Only the cattle and the spoil of that city Israel took for prey to themselves, according to the word of Yahweh which he commanded Joshua.

Basi Yoshua akaupiga moto mji wa Ai, na kuufanya kuwa ni chungu ya magofu hata milele, kuwa ni ukiwa hata siku hii ya leo. Yoshua 8:28

So Joshua burnt Ai, and made it a heap forever, even a desolation, to this day.

Na huyo mfalme wa Ai akamtundika katika mti hata wakati wa jioni; kisha hapo jua lilipokuchwa Yoshua akaagiza, nao wakauondoa mzoga wake katika huo mti, na kuutupa hapo penye maingilio ya lango la mji, kisha wakaweka pale juu yake chungu kubwa ya mawe, hata hivi leo. Yoshua 8:29

The king of Ai he hanged on a tree until the evening: and at the going down of the sun Joshua commanded, and they took his body down from the tree, and cast it at the entrance of the gate of the city, and raised thereon a great heap of stones, to this day.

Ndipo Yoshua alijenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wa Israeli katika mlima Ebali. Yoshua 8:30

Then Joshua built an altar to Yahweh, the God of Israel, in Mount Ebal,

Kama Musa, mtumishi wa Bwana, alivyowaamuru wana wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha torati ya Musa, madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo mtu hakutumia juu yake chombo cha chuma; nao wakatoa juu yake sadaka za kuteketezwa kwa Bwana, na kuchinja sadaka za amani. Yoshua 8:31

as Moses the servant of Yahweh commanded the children of Israel, as it is written in the book of the law of Moses, an altar of uncut stones, on which no man had lifted up any iron: and they offered thereon burnt offerings to Yahweh, and sacrificed peace-offerings.

Akaandika huko juu ya mawe hayo nakala ya torati ya Musa, aliyoiandika mbele ya wana wa Israeli. Yoshua 8:32

He wrote there on the stones a copy of the law of Moses, which he wrote, in the presence of the children of Israel.

Na Israeli wote, na wazee wao, na maakida yao, na makadhi yao, wakasimama upande huu wa sanduku na upande huu, mbele ya makuhani Walawi, waliolichukua sanduku la agano la Bwana, huyo aliyekuwa mgeni pamoja na huyo mzalia; nusu yao mbele ya mlima Gerizimu, na nusu yao mbele ya mlima Ebali, kama Musa, mtumishi wa Bwana, alivyoamuru, ili wawabarikie watu wa Israeli kwanza. Yoshua 8:33

All Israel, and their elders and officers, and their judges, stood on this side of the ark and on that side before the priests the Levites, who bore the ark of the covenant of Yahweh, as well the foreigner as the native; half of them in front of Mount Gerizim, and half of them in front of Mount Ebal; as Moses the servant of Yahweh had commanded at the first, that they should bless the people of Israel.

Na baadaye alisoma maneno yote ya torati, baraka na laana, sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati. Yoshua 8:34

Afterward he read all the words of the law, the blessing and the curse, according to all that is written in the book of the law.

Hapakuwa na hata neno moja katika hayo aliyoamuru Musa, ambalo Yoshua hakulisoma mbele ya kusanyiko lote la Israeli, na mbele ya wanawake, na watoto, na wageni waliokaa nao.

Yoshua 8:35

There was not a word of all that Moses commanded, which Joshua didn't read before all the assembly of Israel, and the women, and the little ones, and the foreigners who were among them.