Yoshua 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 5 (Swahili) Joshua 5 (English)

Ikawa, wafalme wa Waamori, waliokaa ng'ambo ya Yordani pande za magharibi, na wafalme wote wa Wakanaani, waliokuwa karibu na bahari, waliposikia jinsi Bwana alivyoyakausha maji ya Yordani mbele ya wana wa Israeli, hata tulipokwisha kuvuka, basi mioyo yao iliyeyuka, wala haikuwamo roho ya nguvu ndani yao tena; kwa ajili ya wana wa Israeli. Yoshua 5:1

It happened, when all the kings of the Amorites, who were beyond the Jordan westward, and all the kings of the Canaanites, who were by the sea, heard how that Yahweh had dried up the waters of the Jordan from before the children of Israel, until we were passed over, that their heart melted, neither was there spirit in them any more, because of the children of Israel.

Wakati huo Bwana akamwambia Yoshua, Haya, jifanyie visu vya mawe ya gumegume, watahiri tena wana wa Israeli mara ya pili. Yoshua 5:2

At that time Yahweh said to Joshua, Make you flint knives, and circumcise again the children of Israel the second time.

Basi Yoshua akajifanyia visu vya mawe ya gumegume, akawatahiri wana wa Israeli huko Gibea-haaralothi. Yoshua 5:3

Joshua made himself flint knives, and circumcised the children of Israel at the hill of the foreskins.

Na sababu ya Yoshua kutahiri ni hii; watu wote waliotoka Misri, waliokuwa waume, hao watu waume wote waendao vitani walikufa katika bara njiani, baada ya wao kutoka Misri. Yoshua 5:4

This is the cause why Joshua did circumcise: all the people who came forth out of Egypt, who were males, even all the men of war, died in the wilderness by the way, after they came forth out of Egypt.

Kwa kuwa watu wote waliotoka walikuwa wamekwisha kutahiriwa; lakini watu wote waliozaliwa katika bara njiani walipokwisha kutoka Misri, hao hawakutahiriwa. Yoshua 5:5

For all the people who came out were circumcised; but all the people who were born in the wilderness by the way as they came forth out of Egypt, they had not circumcised.

Kwa kuwa wana wa Israeli walitembea muda wa miaka arobaini barani, hata hilo taifa zima, yaani, watu waume waendao vitani, waliotoka Misri, walipokuwa wameangamia; kwa sababu hawakuisikiza sauti ya Bwana; nao ndio Bwana aliowaapia ya kwamba hatawaacha waione hiyo nchi, ambayo Bwana aliwaapia baba zao kwamba atatupa sisi; nchi ijaayo maziwa na asali. Yoshua 5:6

For the children of Israel walked forty years in the wilderness, until all the nation, even the men of war who came forth out of Egypt, were consumed, because they didn't listen to the voice of Yahweh: to whom Yahweh swore that he wouldn't let them see the land which Yahweh swore to their fathers that he would give us, a land flowing with milk and honey.

Na watoto wao, aliowainua badala yao ndio hao aliowatahiri Yoshua; kwa kuwa wao walikuwa hawakutahiriwa, kwa maana walikuwa hawakuwatahiri njiani. Yoshua 5:7

Their children, whom he raised up in their place, them did Joshua circumcise: for they were uncircumcised, because they had not circumcised them by the way.

Ilikuwa walipokwisha kutahiriwa taifa zima, wakakaa kila mtu mahali pake maragoni, hata walipopoa. Yoshua 5:8

It happened, when they had done circumcising all the nation, that they abode in their places in the camp, until they were whole.

Bwana akamwambia Yoshua, Siku hii ya leo nimeivingirisha hiyo aibu ya Misri iondoke juu yenu. Kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Gilgali, hata hivi leo. Yoshua 5:9

Yahweh said to Joshua, This day have I rolled away the reproach of Egypt from off you. Therefore the name of that place was called Gilgal, to this day.

Basi wana wa Israeli wakapanga hema zao huko Gilgali; nao wakala sikukuu ya pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi, jioni, katika nchi tambarare za Yeriko. Yoshua 5:10

The children of Israel encamped in Gilgal; and they kept the Passover on the fourteenth day of the month at even in the plains of Jericho.

Nao wakala katika mazao ya nchi siku ya pili ya kuiandama hiyo sikukuu ya pasaka, mikate isiyotiwa chachu, na bisi, siku iyo hiyo. Yoshua 5:11

They ate of the produce of the land on the next day after the Passover, unleavened cakes and parched grain, in the same day.

Ndipo ile mana ikakoma siku ya pili yake, baada ya wao kuyala hayo mazao ya nchi; na hao wana wa Israeli hawakuwa na mana tena; lakini wakala katika viliwa vya nchi ya Kanaani mwaka huo. Yoshua 5:12

The manna ceased on the next day, after they had eaten of the produce of the land; neither had the children of Israel manna any more; but they ate of the fruit of the land of Canaan that year.

Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? Yoshua 5:13

It happened, when Joshua was by Jericho, that he lifted up his eyes and looked, and, behold, there stood a man over against him with his sword drawn in his hand: and Joshua went to him, and said to him, Are you for us, or for our adversaries?

Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake? Yoshua 5:14

He said, No; but [as] prince of the host of Yahweh am I now come. Joshua fell on his face to the earth, and did worship, and said to him, What says my lord to his servant?

Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo. Yoshua 5:15

The prince of Yahweh's host said to Joshua, Put off your shoe from off your foot; for the place whereon you stand is holy. Joshua did so.