Yoshua 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 7 (Swahili) Joshua 7 (English)

Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya Bwana ikawaka juu ya wana wa Israeli. Yoshua 7:1

But the children of Israel committed a trespass in the devoted thing; for Achan, the son of Carmi, the son of Zabdi, the son of Zerah, of the tribe of Judah, took of the devoted thing: and the anger of Yahweh was kindled against the children of Israel.

Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ulio karibu na Bethaveni, upande wa mashariki wa Betheli, akawaambia, akisema, Pandeni juu mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu wakaupeleleza Ai. Yoshua 7:2

Joshua sent men from Jericho to Ai, which is beside Beth Aven, on the east side of Bethel, and spoke to them, saying, Go up and spy out the land. The men went up and spied out Ai.

Wakarejea kwa Yoshua wakamwambia, Wasiende watu wote, ila waende watu kama elfu mbili, tatu, wakaupige Ai; usiwataabishe watu wote kwa kuwaendesha huko; maana watu hao ni wachache tu. Yoshua 7:3

They returned to Joshua, and said to him, Don't let all the people go up; but let about two or three thousand men go up and strike Ai; don't make all the people to toil there; for they are but few.

Basi watu wakaenda huko wapata elfu tatu tu; nao wakakimbia mbele ya watu wa Ai. Yoshua 7:4

So there went up there of the people about three thousand men: and they fled before the men of Ai.

Watu wa Ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; wakawafuatia kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu, wakawapiga huko kwenye matelemko; mioyo ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji. Yoshua 7:5

The men of Ai struck of them about thirty-six men; and they chased them [from] before the gate even to Shebarim, and struck them at the descent; and the hearts of the people melted, and became as water.

Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Bwana hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao. Yoshua 7:6

Joshua tore his clothes, and fell to the earth on his face before the ark of Yahweh until the evening, he and the elders of Israel; and they put dust on their heads.

Yoshua akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili kututia katika mikono ya Waamori, na kutuangamiza? Laiti tungelikuwa radhi kukaa ng'ambo ya Yordani Yoshua 7:7

Joshua said, Alas, Lord Yahweh, why have you at all brought this people over the Jordan, to deliver us into the hand of the Amorites, to cause us to perish? would that we had been content and lived beyond the Jordan!

Ee Bwana, niseme nini baada ya Israeli kuwapa visogo adui zao? Yoshua 7:8

Oh, Lord, what shall I say, after that Israel has turned their backs before their enemies!

Maana Wakanaani na wenyeji wote wa nchi hii watasikia habari hii, nao watatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu? Yoshua 7:9

For the Canaanites and all the inhabitants of the land will hear of it, and will compass us round, and cut off our name from the earth: and what will you do for your great name?

Bwana akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi? Yoshua 7:10

Yahweh said to Joshua, Get you up; why are you thus fallen on your face?

Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe. Yoshua 7:11

Israel has sinned; yes, they have even transgressed my covenant which I commanded them: yes, they have even taken of the devoted thing, and have also stolen, and dissembled also; and they have even put it among their own stuff.

Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu. Yoshua 7:12

Therefore the children of Israel can't stand before their enemies; they turn their backs before their enemies, because they are become accursed: I will not be with you any more, except you destroy the devoted thing from among you.

Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, mwe tayari kesho; maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu. Yoshua 7:13

Up, sanctify the people, and say, Sanctify yourselves against tomorrow: for thus says Yahweh, the God of Israel, There is a devoted thing in the midst of you, Israel; you can not stand before your enemies, until you take away the devoted thing from among you.

Basi asubuhi mtaletwa karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya kwamba kabila ile atakayoitwaa Bwana itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile atakayoitwaa Bwana itakaribia nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa Bwana itakaribia mtu kwa mtu. Yoshua 7:14

In the morning therefore you shall be brought near by your tribes: and it shall be, that the tribe which Yahweh takes shall come near by families; and the family which Yahweh shall take shall come near by households; and the household which Yahweh shall take shall come near man by man.

Tena itakuwa ya kwamba yeye atakayetwaliwa, naye anacho kitu kile kilichowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, yeye na vitu vyote alivyo navyo; kwa sababu amelivunja agano la Bwana, na kwa sababu ametenda upumbavu katika Israeli. Yoshua 7:15

It shall be, that he who is taken with the devoted thing shall be burnt with fire, he and all that he has; because he has transgressed the covenant of Yahweh, and because he has done folly in Israel.

Basi Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, akawasogeza Israeli kabila kwa kabila; kabila ya Yuda ikatwaliwa. Yoshua 7:16

So Joshua rose up early in the morning, and brought Israel near by their tribes; and the tribe of Judah was taken:

Akazisogeza jamaa za Yuda, akaitwaa jamaa ya Wazera; akaisogeza jamaa ya Wazera mtu kwa mtu; Zabdi akatwaliwa. Yoshua 7:17

and he brought near the family of Judah; and he took the family of the Zerahites: and he brought near the family of the Zerahites man by man; and Zabdi was taken:

Akawasogeza watu wa nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda akatwaliwa. Yoshua 7:18

and he brought near his household man by man; and Achan, the son of Carmi, the son of Zabdi, the son of Zerah, of the tribe of Judah, was taken.

Yoshua akamwambia Akani, Mwanangu, nakusihi, umtukuze Bwana, Mungu wa Israeli, ukaungame kwake; uniambie sasa ulilolitenda; usinifiche. Yoshua 7:19

Joshua said to Achan, My son, please give glory to Yahweh, the God of Israel, and make confession to him; and tell me now what you have done; don't hide it from me.

Akani akamjibu Yoshua, akasema, Kweli nimefanya dhambi juu ya Bwana, Mungu wa Israeli, nami nimefanya mambo haya na haya. Yoshua 7:20

Achan answered Joshua, and said, Of a truth I have sinned against Yahweh, the God of Israel, and thus and thus have I done:

Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake. Yoshua 7:21

when I saw among the spoil a goodly Babylonian mantle, and two hundred shekels of silver, and a wedge of gold of fifty shekels weight, then I coveted them, and took them; and, behold, they are hid in the earth in the midst of my tent, and the silver under it.

Basi Yoshua akatuma wajumbe wakapiga mbio mpaka hemani; na tazama, vile vitu vilikuwa vimefichwa hemani mwake, na ile fedha chini yake. Yoshua 7:22

So Joshua sent messengers, and they ran to the tent; and, behold, it was hid in his tent, and the silver under it.

Wakavitoa kutoka hapo katikati ya hema, wakavileta kwa Yoshua, na kwa wana wa Israeli wote, nao wakaviweka chini mbele za Bwana. Yoshua 7:23

They took them from the midst of the tent, and brought them to Joshua, and to all the children of Israel; and they laid them down before Yahweh.

Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng'ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori. Yoshua 7:24

Joshua, and all Israel with him, took Achan the son of Zerah, and the silver, and the mantle, and the wedge of gold, and his sons, and his daughters, and his oxen, and his donkeys, and his sheep, and his tent, and all that he had: and they brought them up to the valley of Achor.

Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? Bwana atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe. Yoshua 7:25

Joshua said, Why have you troubled us? Yahweh shall trouble you this day. All Israel stoned him with stones; and they burned them with fire, and stoned them with stones.

Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa ya mawe hata leo; naye Bwana akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata hivi leo.

Yoshua 7:26

They raised over him a great heap of stones, to this day; and Yahweh turned from the fierceness of his anger. Therefore the name of that place was called "The valley of Achor" to this day.