1
Hili ni neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi katika habari za Yuda na Yerusalemu.
This is the message that was revealed to Isaiah son of Amoz concerning Judah and Jerusalem:
2
Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.
In the last days the mountain of the house of the LORD will be established as the chief of the mountains; it will be raised above the hills, and all nations will stream to it.
3
Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.
And many peoples will come and say: “Come, let us go up to the mountain of the LORD, to the house of the God of Jacob. He will teach us His ways so that we may walk in His paths.” For the law will go forth from Zion, and the word of the LORD from Jerusalem.
4
Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.
Then He will judge between the nations and arbitrate for many peoples. They will beat their swords into plowshares and their spears into pruning hooks. Nation will no longer take up the sword against nation, nor train anymore for war.
5
Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.
Come, O house of Jacob, let us walk in the light of the LORD.
6
Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapana mikono na wana wa wageni.
For You have abandoned Your people, the house of Jacob, because they are filled with influences from the east; they are soothsayers like the Philistines; they strike hands with the children of foreigners.
7
Tena nchi yao imejaa fedha na dhahabu, wala hapana mwisho wa hazina zao; tena nchi yao imejaa farasi, wala hapana mwisho wa magari yao.
Their land is full of silver and gold, with no limit to their treasures; their land is full of horses, with no limit to their chariots.
8
Tena nchi yao imejaa sanamu; huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyofanywa kwa vidole vyao wenyewe.
Their land is full of idols; they bow down to the work of their hands, to what their fingers have made.
9
Mtu mnyonge huinama, na mtu mkubwa hujidhili; kwa hiyo usiwasamehe.
So mankind is brought low, and man is humbled—do not forgive them!
10
Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa Bwana, mbele za utukufu wa enzi yake.
Go into the rocks and hide in the dust from the terror of the LORD and the splendor of His majesty.
11
Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
The proud look of man will be humbled, and the loftiness of men brought low; the LORD alone will be exalted in that day.
12
Kwa maana kutakuwa siku ya Bwana wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.
For the Day of the LORD of Hosts will come against all the proud and lofty, against all that is exalted—it will be humbled—
13
Na juu ya mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani;
against all the cedars of Lebanon, lofty and lifted up, against all the oaks of Bashan,
14
na juu ya milima mirefu yote, na juu ya vilima vyote vilivyoinuka;
against all the tall mountains, against all the high hills,
15
na juu ya kila mnara mrefu, na juu ya kila ukuta ulio na boma;
against every high tower, against every fortified wall,
16
na juu ya merikebu zote za Tarshishi, na juu ya kila taswira ipendezayo.
against every ship of Tarshish, and against every stately vessel.
17
Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
So the pride of man will be brought low, and the loftiness of men will be humbled; the LORD alone will be exalted in that day,
18
Nazo sanamu zitatoweka kabisa.
and the idols will vanish completely.
19
Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.
Men will flee to caves in the rocks and holes in the ground, away from the terror of the LORD and from the splendor of His majesty, when He rises to shake the earth.
20
Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojifanyia ili kuziabudu, kwa fuko na popo;
In that day men will cast away to the moles and bats their idols of silver and gold—the idols they made to worship.
21
ili aingie ndani ya pango za majabali, na ndani ya tundu za miamba iliyopasuka, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.
They will flee to caverns in the rocks and crevices in the cliffs, away from the terror of the LORD and from the splendor of His majesty, when He rises to shake the earth.
22
Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake; kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?
Put no more trust in man, who has only the breath in his nostrils. Of what account is he?