Isaya 49 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 49 (Swahili) Isaiah 49 (English)

Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi kabila za watu mlio mbali sana; Bwana ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu. Isaya 49:1

Listen, isles, to me; and listen, you peoples, from far: Yahweh has called me from the womb; from the bowels of my mother has he made mention of my name:

Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake amenificha; Isaya 49:2

and he has made my mouth like a sharp sword; in the shadow of his hand has he hid me: and he has made me a polished shaft; in his quiver has he kept me close:

akaniambia; Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika wewe nitatukuzwa. Isaya 49:3

and he said to me, You are my servant; Israel, in whom I will be glorified.

Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina Bwana, na thawabu yangu ina Mungu wangu. Isaya 49:4

But I said, I have labored in vain, I have spent my strength for nothing and vanity; yet surely the justice [due] to me is with Yahweh, and my recompense with my God.

Na sasa Bwana asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena, na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya Bwana, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu); Isaya 49:5

Now says Yahweh who formed me from the womb to be his servant, to bring Jacob again to him, and that Israel be gathered to him (for I am honorable in the eyes of Yahweh, and my God is become my strength);

naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia. Isaya 49:6

yes, he says, It is too light a thing that you should be my servant to raise up the tribes of Jacob, and to restore the preserved of Israel: I will also give you for a light to the Gentiles, that you may be my salvation to the end of the earth.

Bwana, mkombozi wa Israeli, Mtakatifu wake, amwambia hivi yeye anayedharauliwa na wanadamu; yeye anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye mtumishi wao watawalao; Wafalme wataona, watasimama; wakuu nao watasujudu; kwa sababu ya Bwana aliye mwaminifu, Mtakatifu wa Israeli aliyekuchagua Isaya 49:7

Thus says Yahweh, the Redeemer of Israel, [and] his Holy One, to him whom man despises, to him whom the nation abhors, to a servant of rulers: Kings shall see and arise; princes, and they shall worship; because of Yahweh who is faithful, [even] the Holy One of Israel, who has chosen you.

Bwana asema hivi, Wakati uliokubalika nimekujibu, na siku ya wokovu nimekusaidia; nami nitakuhifadhi, nitakutoa uwe agano la watu hawa, ili kuiinua nchi hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa ukiwa; Isaya 49:8

Thus says Yahweh, In an acceptable time have I answered you, and in a day of salvation have I helped you; and I will preserve you, and give you for a covenant of the people, to raise up the land, to make them inherit the desolate heritage:

kuwaambia waliofungwa, Haya, tokeni; na hao walio katika giza, Jionyesheni. Watajilisha katika njia, na juu ya majabali watapata malisho. Isaya 49:9

saying to those who are bound, Go forth; to those who are in darkness, Show yourselves. They shall feed in the ways, and on all bare heights shall be their pasture.

Hawataona njaa, wala hawataona kiu; hari haitawapiga, wala jua; kwa maana yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza. Isaya 49:10

They shall not hunger nor thirst; neither shall the heat nor sun strike them: for he who has mercy on them will lead them, even by springs of water will he guide them.

Nami nitafanya milima yangu yote kuwa njia, na njia kuu zangu zitatukuzwa zote. Isaya 49:11

I will make all my mountains a way, and my highways shall be exalted.

Tazama, hawa watakuja kutoka mbali; na tazama, hawa kutoka kaskazini, na kutoka magharibi, na hawa kutoka nchi ya Sinimu. Isaya 49:12

Behold, these shall come from far; and, behold, these from the north and from the west; and these from the land of Sinim.

Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa kuwa Bwana amewafariji watu wake, Naye atawahurumia watu wake walioteswa. Isaya 49:13

Sing, heavens; and be joyful, earth; and break forth into singing, mountains: for Yahweh has comforted his people, and will have compassion on his afflicted.

Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau. Isaya 49:14

But Zion said, Yahweh has forsaken me, and the Lord has forgotten me.

Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. Isaya 49:15

Can a woman forget her sucking child, that she should not have compassion on the son of her womb? yes, these may forget, yet I will not forget you.

Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima. Isaya 49:16

Behold, I have engraved you on the palms of my hands; your walls are continually before me.

Watoto wako wafanya haraka, hao wakuharibuo, nao waliokufanya ukiwa, watatoka kwako. Isaya 49:17

Your children make haste; your destroyers and those who made you waste shall go forth from you.

Inua macho yako, ukatazame pande zote; hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama niishivyo, asema Bwana, hakika utajivika na hao wote, kama kwa uzuri, nawe utajifungia hao, kama bibi arusi. Isaya 49:18

Lift up your eyes round about, and see: all these gather themselves together, and come to you. As I live, says Yahweh, you shall surely clothe you with them all as with an ornament, and gird yourself with them, like a bride.

Maana katika habari za mahali pako palipokuwa ukiwa, pasipokaliwa na watu, na nchi yako iliyoharibika hakika sasa utakuwa mwembamba usiwatoshe wenyeji wako, nao waliokumeza watakuwa mbali. Isaya 49:19

For, as for your waste and your desolate places, and your land that has been destroyed, surely now shall you be too small for the inhabitants, and those who swallowed you up shall be far away.

Watoto ulionyang'anywa watasema masikioni mwako, Mahali hapa ni pembamba, hapanitoshi; nipe nafasi nipate kukaa. Isaya 49:20

The children of your bereavement shall yet say in your ears, The place is too small for me; give place to me that I may dwell.

Ndipo utasema moyoni mwako, Ni nani aliyenizalia watoto hawa, na mimi nimefiwa na watoto wangu, nami ni peke yangu, nimehamishwa, ninatanga-tanga huko na huku? Tena ni nani aliyewalea hawa? Tazama, naliachwa peke yangu; hawa je! Walikuwa wapi? Isaya 49:21

Then shall you say in your heart, Who has conceived these for me, seeing I have been bereaved of my children, and am solitary, an exile, and wandering back and forth? and who has brought up these? Behold, I was left alone; these, where were they?

Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwatwekea kabila za watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao. Isaya 49:22

Thus says the Lord Yahweh, Behold, I will lift up my hand to the nations, and set up my ensign to the peoples; and they shall bring your sons in their bosom, and your daughters shall be carried on their shoulders.

Na wafalme watakuwa baba zako za kulea, na malkia zao mama zako za kulea; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni Bwana, tena waningojeao hawatatahayarika. Isaya 49:23

Kings shall be your nursing fathers, and their queens your nursing mothers: they shall bow down to you with their faces to the earth, and lick the dust of your feet; and you shall know that I am Yahweh; and those who wait for me shall not be disappointed.

Je! Aliye hodari aweza kunyang'anywa mateka yake, au jeshi lao waliofungwa halali wataokoka? Isaya 49:24

Shall the prey be taken from the mighty, or the lawful captives be delivered?

Naam, Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye jabari wataokoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu. Isaya 49:25

But thus says Yahweh, Even the captives of the mighty shall be taken away, and the prey of the terrible shall be delivered; for I will contend with him who contends with you, and I will save your children.

Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na wote wenye mwili watajua ya kuwa mimi, Bwana, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo. Isaya 49:26

I will feed those who oppress you with their own flesh; and they shall be drunken with their own blood, as with sweet wine: and all flesh shall know that I, Yahweh, am your Savior, and your Redeemer, the Mighty One of Jacob.