Isaya 41 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 41 (Swahili) Isaiah 41 (English)

Nyamazeni mbele zangu, enyi visiwa, na mataifa wajipatie nguvu mpya; na waje karibu wakanene; na tukaribiane pamoja kwa hukumu. Isaya 41:1

Keep silence before me, islands; and let the peoples renew their strength: let them come near; then let them speak; let us come near together to judgment.

Ni nani aliyemwinua mmoja atokaye mashariki, ambaye katika haki amemwita mguuni pake? Ampa mataifa mbele yake, na kumtawaza juu ya wafalme; awatoa wawe kama mavumbi kwa upanga wake, kama makapi yaliyopeperushwa kwa upinde wake. Isaya 41:2

Who has raised up one from the east, whom he calls in righteousness to his foot? he gives nations before him, and makes him rule over kings; he gives them as the dust to his sword, as the driven stubble to his bow.

Awafuatia, apita salama hata kwa njia asiyoikanyaga kamwe kwa miguu yake. Isaya 41:3

He pursues them, and passes on safely, even by a way that he had not gone with his feet.

Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, Bwana, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye. Isaya 41:4

Who has worked and done it, calling the generations from the beginning? I, Yahweh, the first, and with the last, I am he.

Visiwa vimeona, vikaogopa; ncha za dunia zilitetemeka; walikaribia, walikuja. Isaya 41:5

The isles have seen, and fear; the ends of the earth tremble; they draw near, and come.

Wakasaidiana, kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake; Uwe na moyo mkuu. Isaya 41:6

They help everyone his neighbor; and [every one] says to his brother, Be of good courage.

Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga, akisema, Ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isitikisike. Isaya 41:7

So the carpenter encourages the goldsmith, [and] he who smoothes with the hammer him who strikes the anvil, saying of the soldering, It is good; and he fastens it with nails, that is should not be moved.

Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu; Isaya 41:8

But you, Israel, my servant, Jacob whom I have chosen, the seed of Abraham my friend,

wewe niliyekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa; Isaya 41:9

you whom I have taken hold of from the ends of the earth, and called from the corners of it, and said to you, You are my servant, I have chosen you and not cast you away;

usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Isaya 41:10

Don't you be afraid, for I am with you; don't be dismayed, for I am your God; I will strengthen you; yes, I will help you; yes, I will uphold you with the right hand of my righteousness.

Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Isaya 41:11

Behold, all those who are incensed against you shall be disappointed and confounded: those who strive with you shall be as nothing, and shall perish.

Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako. Isaya 41:12

You shall seek them, and shall not find them, even those who contend with you: those who war against you shall be as nothing, and as a thing of nothing.

Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia. Isaya 41:13

For I, Yahweh your God, will hold your right hand, saying to you, Don't be afraid; I will help you.

Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema Bwana, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli. Isaya 41:14

Don't be afraid, you worm Jacob, and you men of Israel; I will help you, says Yahweh, and your Redeemer is the Holy One of Israel.

Tazama, nitakufanya kuwa chombo kikali kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha milima, na kuisaga; nawe utafanya vilima kuwa kama makapi. Isaya 41:15

Behold, I have made you [to be] a new sharp threshing instrument having teeth; you shall thresh the mountains, and beat them small, and shall make the hills as chaff.

Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia Bwana, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli. Isaya 41:16

You shall winnow them, and the wind shall carry them away, and the whirlwind shall scatter them; and you shall rejoice in Yahweh, you shall glory in the Holy One of Israel.

Maskini na wahitaji wanatafuta maji, wala hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu; mimi, Bwana, nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha. Isaya 41:17

The poor and needy seek water, and there is none, and their tongue fails for thirst; I, Yahweh, will answer them, I, the God of Israel, will not forsake them.

Nitafunua vijito vya maji juu ya vilima, na chemchemi katikati ya mabonde; nitageuza jangwa kuwa ziwa la maji, na mahali pakavu kuwa vijito vya maji. Isaya 41:18

I will open rivers on the bare heights, and springs in the midst of the valleys; I will make the wilderness a pool of water, and the dry land springs of water.

Nitapanda katika jangwa mwerezi, mshita, mhadasi, na mbono; nitatia katika nyika mberoshi, mtidhari, na mteashuri pamoja; Isaya 41:19

I will put in the wilderness the cedar, the acacia, and the myrtle, and the oil tree; I will set in the desert the fir tree, the pine, and the box tree together:

ili waone, na kujua, wakafikiri, na kufahamu pamoja, ya kuwa mkono wa Bwana ndio uliofanya jambo hilo. Mtakatifu wa Israeli ndiye aliyeliumba. Isaya 41:20

that they may see, and know, and consider, and understand together, that the hand of Yahweh has done this, and the Holy One of Israel has created it.

Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo. Isaya 41:21

Produce your cause, says Yahweh; bring forth your strong reasons, says the King of Jacob.

Wayatangaze na kutujulisha yatakayokuwa; watuonyeshe mambo ya zamani, ni mambo gani, tukapate kuyatia moyoni, tukajue mwisho wake; au wamdhihirishie yatakayotokea baadaye. Isaya 41:22

Let them bring forth, and declare to us what shall happen: declare you the former things, what they are, that we may consider them, and know the latter end of them; or show us things to come.

Tujulisheni yatakayokuwa baadaye, nasi tutakiri ya kuwa ninyi ni miungu; naam, tendeni mema au tendeni mabaya, ili tujipime, tukaone pamoja. Isaya 41:23

Declare the things that are to come hereafter, that we may know that you are gods: yes, do good, or do evil, that we may be dismayed, and see it together.

Tazameni, ninyi si kitu, tena kazi yenu si kitu; awachaguaye ninyi ni chukizo. Isaya 41:24

Behold, you are of nothing, and your work is of nothing; an abomination is he who chooses you.

Nimemwinua mtu toka kaskazini, naye amekuja; toka maawio ya jua amekuja anitajaye jina langu; naye atawajilia maliwali kama akanyagaye matope, na kama mfinyanzi afinyangaye udongo. Isaya 41:25

I have raised up one from the north, and he has come; from the rising of the sun one who calls on my name: and he shall come on rulers as on mortar, and as the potter treads clay.

Ni nani aliyeihubiri habari tokea mwanzo, tupate kuijua? Na tokea zamani, tupate kusema, Yeye ni mwenye haki? Naam, hapana hata mmoja aliyetujulisha; naam, hapana hata mmoja aliyetuonyesha; naam, hapana hata mmoja aliyesikia maneno yenu. Isaya 41:26

Who has declared it from the beginning, that we may know? and before, that we may say, [He is] right? yes, there is none who declares, yes, there is none who shows, yes, there is none who hears your words.

Mimi kwanza nitauambia Sayuni, Tazama; hawa ndio; nami nitampa Yerusalemu mletaji wa habari njema. Isaya 41:27

[I am the] first [who says] to Zion, Behold, behold them; and I will give to Jerusalem one who brings good news.

Na nitazamapo, hapana mtu, hata katika watu hao hapana mshauri mmoja, ambaye, nikimwuliza, aweza kunijibu neno. Isaya 41:28

When I look, there is no man: even among them there is no counselor who, when I ask of them, can answer a word.

Tazama, hao wote ni ubatili; kazi zao si kitu; sanamu zao ni upepo na fujo. Isaya 41:29

Behold, all of them, their works are vanity [and] nothing; their molten images are wind and confusion.