Isaya 36 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 36 (Swahili) Isaiah 36 (English)

Ikawa, katika mwaka wa kumi na nne wa kumiliki kwake mfalme Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akapanda ili kupigana na miji yote ya Yuda yenye boma, akaitwaa. Isaya 36:1

Now it happened in the fourteenth year of king Hezekiah, that Sennacherib king of Assyria came up against all the fortified cities of Judah, and took them.

Mfalme wa Ashuru akamtuma amiri toka Lakishi hata Yerusalemu,kwa mfalme Hezekia,pamoja na jeshi kubwa. Naye akasimama karibu na mfereji wa birika ya juu,iliyo katika njia kuu ya kuuendea uwanda wa dobi. Isaya 36:2

The king of Assyria sent Rabshakeh from Lachish to Jerusalem to king Hezekiah with a great army. He stood by the conduit of the upper pool in the highway of the fuller's field.

Wakamtokea Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika tarehe. Isaya 36:3

Then came forth to him Eliakim the son of Hilkiah, who was over the household, and Shebna the scribe, and Joah, the son of Asaph, the recorder.

Yule amiri akawaambia, Haya, mwambieni Hezekia, kwamba mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, asema hivi, Ni tumaini gani hili unalolitumainia? Isaya 36:4

Rabshakeh said to them, Say you now to Hezekiah, Thus says the great king, the king of Assyria, What confidence is this in which you trust?

Nasema, mashauri yako, na nguvu zako kwa vita, ni maneno yasiyo na maana; basi, unamtumaini nani hata ukaniasi mimi? Isaya 36:5

I say, [your] counsel and strength for the war are but vain words: now on whom do you trust, that you have rebelled against me?

Tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliopondeka, yaani, Misri, ambayo, mtu akitegemea juu yake, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio. Isaya 36:6

Behold, you trust on the staff of this bruised reed, even on Egypt, whereon if a man lean, it will go into his hand, and pierce it: so is Pharaoh king of Egypt to all who trust on him.

Lakini ukiniambia, Tunamtumaini Bwana, Mungu wetu, je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake mlimoinuka, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii? Isaya 36:7

But if you tell me, We trust in Yahweh our God: isn't that he, whose high places and whose altars Hezekiah has taken away, and has said to Judah and to Jerusalem, You shall worship before this altar?

Basi sasa, tafadhali mpe bwana wangu, mfalme wa Ashuru, dhamana, nami nitakupa farasi elfu mbili, ikiwa wewe kwa upande wako waweza kupandisha watu juu yao. Isaya 36:8

Now therefore, please give pledges to my master the king of Assyria, and I will give you two thousand horses, if you are able on your part to set riders on them.

Wawezaje, basi, kurudisha nyuma uso wa akida mmoja wa watumishi walio wadogo wa bwana wangu, na kuitumainia Misri upewe magari na farasi? Isaya 36:9

How then can you turn away the face of one captain of the least of my master's servants, and put your trust on Egypt for chariots and for horsemen?

Je! Nimepanda mimi, ili kupigana na mahali hapa na kupaangamiza, bila shauri la Bwana? Bwana ndiye aliyeniambia, Panda upigane na nchi hii na kuiangamiza. Isaya 36:10

Am I now come up without Yahweh against this land to destroy it? Yahweh said to me, Go up against this land, and destroy it.

Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Shebna, na Yoa, wakamwambia yule amiri, Tafadhali, sema na watumishi wako kwa lugha ya Kiashuri; maana tunaifahamu; wala usiseme nasi kwa lugha ya Kiyahudi, masikioni mwa watu wote walio ukutani. Isaya 36:11

Then said Eliakim and Shebna and Joah to Rabshakeh, Please speak, to your servants in the Syrian language; for we understand it: and don't speak to us in the Jews' language, in the ears of the people who are on the wall.

Lakini yule amiri akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma kwa bwana wako, na kwako wewe, niseme maneno haya? Hakunituma kwa watu hawa walio ukutani, ili wale mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi? Isaya 36:12

But Rabshakeh said, Has my master sent me to your master, and to you, to speak these words? [has he] not [sent me] to the men who sit on the wall, to eat their own dung, and to drink their own water with you?

Kisha yule amiri akasimama akalia kwa sauti kuu kwa lugha ya Kiyahudi, akisema, Lisikieni neno la mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru. Isaya 36:13

Then Rabshakeh stood, and cried with a loud voice in the Jews' language, and said, Hear you the words of the great king, the king of Assyria.

Mfalme asema hivi; Hezekia asiwadanganye, kwa maana hataweza kuwaokoa; Isaya 36:14

Thus says the king, Don't let Hezekiah deceive you; for he will not be able to deliver you:

wala msimwache Hezekia kuwatia moyo wa kumtumaini Bwana; akisema, Bwana bila shaka atatuokoa, mji huu hautatiwa katika mkono wa mfalme wa Ashuru. Isaya 36:15

neither let Hezekiah make you trust in Yahweh, saying, Yahweh will surely deliver us; this city shall not be given into the hand of the king of Assyria.

Msimsikilize Hezekia; maana mfalme wa Ashuru asema hivi, Fanyeni suluhu na mimi, mkatoke mnijie, mkale kila mtu matunda ya mzabibu wake na matunda ya mtini wake, mkanywe kila mmoja maji ya birika yake mwenyewe; Isaya 36:16

Don't listen to Hezekiah: for thus says the king of Assyria, Make your peace with me, and come out to me; and eat you everyone of his vine, and everyone of his fig tree, and drink you everyone the waters of his own cistern;

hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu. Isaya 36:17

until I come and take you away to a land like your own land, a land of grain and new wine, a land of bread and vineyards.

Jihadharini, asije Hezekia akawadanganya, akisema, Bwana atatuokoa. Je! Yuko mungu mmoja wa mataifa aliyewaokoa watu wake na mkono wa mfalme wa Ashuru? Isaya 36:18

Beware lest Hezekiah persuade you, saying, Yahweh will deliver us. Has any of the gods of the nations delivered his land out of the hand of the king of Assyria?

Wako wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Wako wapi miungu ya Sefarvaimu? Je! Wameiokoa Samaria na mkono wangu? Isaya 36:19

Where are the gods of Hamath and Arpad? where are the gods of Sepharvaim? and have they delivered Samaria out of my hand?

Katika miungu yote ya nchi hizi ni nani waliookoa nchi yao na mkono wangu, hata Bwana auokoe Yerusalemu na mkono wangu? Isaya 36:20

Who are they among all the gods of these countries, that have delivered their country out of my hand, that Yahweh should deliver Jerusalem out of my hand?

Lakini watu wakanyamaza kimya; wala hawakumjibu hata neno moja; maana ilikuwa amri ya mfalme, kwamba, Msimjibu neno. Isaya 36:21

But they held their peace, and answered him not a word; for the king's commandment was, saying, Don't answer him.

Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu mwenye kuandika tarehe, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zimeraruliwa, wakamwambia Hezekia maneno ya yule amiri. Isaya 36:22

Then came Eliakim the son of Hilkiah, who was over the household, and Shebna the scribe, and Joah, the son of Asaph, the recorder, to Hezekiah with their clothes torn, and told him the words of Rabshakeh.