Isaya 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 10 (Swahili) Isaiah 10 (English)

Ole wao wawekao amri zisizo za haki, na waandishi waandikao maneno ya ushupavu; Isaya 10:1

Woe to those who decree unrighteous decrees, and to the writers who write perverseness;

ili kumpotosha mhitaji asipate haki yake, na kuwanyang'anya maskini wa watu wangu haki yao; ili wajane wawe mateka yao, na kuwafanya yatima waliofiwa na baba zao kuwa mawindo yao! Isaya 10:2

to turn aside the needy from justice, and to rob the poor of my people of their right, that widows may be their spoil, and that they may make the fatherless their prey!

Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi? Isaya 10:3

What will you do in the day of visitation, and in the desolation which shall come from far? to whom will you flee for help? and where will you leave your glory?

Watainama chini ya wafungwa tu, wataanguka chini yao waliouawa. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa. Isaya 10:4

They shall only bow down under the prisoners, and shall fall under the slain. For all this his anger is not turned away, but his hand is stretched out still.

Ole wake Ashuru! Fimbo ya hasira yangu, ambaye gongo lililo mkononi mwake ni ghadhabu yangu! Isaya 10:5

Ho Assyrian, the rod of my anger, the staff in whose hand is my indignation!

Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani. Isaya 10:6

I will send him against a profane nation, and against the people of my wrath will I give him a charge, to take the spoil, and to take the prey, and to tread them down like the mire of the streets.

Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache. Isaya 10:7

However he doesn't mean so, neither does his heart think so; but it is in his heart to destroy, and to cut off not a few nations.

Maana asema, Je! Wakuu wangu si wote wafalme? Isaya 10:8

For he says, Aren't my princes all of them kings?

Je! Kalno si kama Karkemishi? Hamathi si kama Arpadi? Samaria si kama Dameski? Isaya 10:9

Isn't Calno as Carchemish? Isn't Hamath as Arpad? Isn't Samaria as Damascus?

Kama vile mkono wangu ulivyofikilia falme za sanamu, ambazo sanamu zao za kuchongwa zilikuwa bora kuliko sanamu za Yerusalemu na za Samaria; Isaya 10:10

As my hand has found the kingdoms of the idols, whose engraved images did excel them of Jerusalem and of Samaria;

je! Sitautenda Yerusalemu na sanamu zake vile vile kama nilivyoutenda Samaria na sanamu zake? Isaya 10:11

shall I not, as I have done to Samaria and her idols, so do to Jerusalem and her idols?

Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitayaadhibu matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake. Isaya 10:12

Therefore it shall happen that, when the Lord has performed his whole work on Mount Zion and on Jerusalem, I will punish the fruit of the stout heart of the king of Assyria, and the glory of his high looks.

Kwa maana amesema, Kwa nguvu za mkono wangu nimetenda jambo hili, na kwa hekima yangu; maana mimi nina busara; nami nimeiondoa mipaka ya watu, nikaziteka akiba zao, nikawaangusha waketio juu ya viti vya enzi kama afanyavyo shujaa. Isaya 10:13

For he has said, By the strength of my hand I have done it, and by my wisdom; for I have understanding: and I have removed the bounds of the peoples, and have robbed their treasures, and like a valiant man I have brought down those who sit [on thrones]:

Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama katika kioto cha ndege; na kama vile watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya dunia yote; wala hapana aliyetikisa bawa, wala kufumbua kinywa, wala kulia. Isaya 10:14

and my hand has found as a nest the riches of the peoples; and as one gathers eggs that are forsaken, have I gathered all the earth: and there was none that moved the wing, or that opened the mouth, or chirped.

Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti. Isaya 10:15

Shall the axe boast itself against him who hews therewith? Shall the saw magnify itself against him who wields it? as if a rod should wield those who lift it up, [or] as if a staff should lift up [him who is] not wood.

Kwa hiyo Bwana, Bwana wa majeshi, atawapelekea kukonda watu wake walionona; na badala ya utukufu wake kutawashwa kuteketea kama kuteketea kwa moto. Isaya 10:16

Therefore will the Lord, Yahweh of Hosts, send among his fat ones leanness; and under his glory there shall be kindled a burning like the burning of fire.

Na mwanga wa Israeli utakuwa ni moto, na Mtakatifu wake atakuwa mwali wa moto; nao utateketeza na kula mbigili zake na miiba yake katika siku moja. Isaya 10:17

The light of Israel will be for a fire, and his Holy One for a flame; and it will burn and devour his thorns and his briers in one day.

Naye atauteketeza utukufu wa msitu wake, na wa shamba lake linalositawi, tangu nafsi hata nyama ya mwili, itakuwa kama vile afapo mtu aliye mgonjwa. Isaya 10:18

He will consume the glory of his forest, and of his fruitful field, both soul and body: and it shall be as when a standard-bearer faints.

Na miti ya msitu wake itakayosalia itakuwa michache, hata mtoto ataweza kuihesabu. Isaya 10:19

The remnant of the trees of his forest shall be few, so that a child may write them.

Tena itakuwa katika siku hiyo mabaki ya Israeli, na hao waliopona wa nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga, bali watamtegemea Bwana, Mtakatifu wa Israeli, kwa kweli. Isaya 10:20

It shall come to pass in that day, that the remnant of Israel, and those who are escaped of the house of Jacob, shall no more again lean on him who struck them, but shall lean on Yahweh, the Holy One of Israel, in truth.

Mabaki, nao ni mabaki ya Yakobo, watamrudia Mungu, aliye mwenye nguvu. Isaya 10:21

A remnant shall return, [even] the remnant of Jacob, to the mighty God.

Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki. Isaya 10:22

For though your people, Israel, be as the sand of the sea, [only] a remnant of them shall return: a destruction [is] determined, overflowing with righteousness.

Kwa maana Bwana, Bwana wa majeshi, atayatimiza maangamizo yaliyokusudiwa katika nchi yote. Isaya 10:23

For a full end, and that determined, will the Lord, Yahweh of Hosts, make in the midst of all the earth.

Kwa hiyo Bwana, Bwana wa majeshi, asema hivi, Enyi watu wangu mkaao katika Sayuni, msiogope Ashuru, ingawa akupiga kwa fimbo, na kuliinua gongo lake juu yako, kwa namna ya Kimisri. Isaya 10:24

Therefore thus says the Lord, Yahweh of Hosts, my people who dwell in Zion, don't be afraid of the Assyrian, though he strike you with the rod, and lift up his staff against you, after the manner of Egypt.

Maana bado kitambo kidogo tu ghadhabu itakoma, na hasira yangu itageukia kuwaangamiza. Isaya 10:25

For yet a very little while, and the indignation [against you] shall be accomplished, and my anger [shall be directed] to his destruction.

Na Bwana wa majeshi ataamsha mjeledi juu yake, kama vile alivyopiga Midiani karibu na jabali la Orebu; na fimbo yake itakuwa juu ya bahari, naye ataiinua kwa namna ya Kimisri. Isaya 10:26

Yahweh of Hosts will stir up against him a scourge, as in the slaughter of Midian at the rock of Oreb: and his rod will be over the sea, and he will lift it up after the manner of Egypt.

Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta. Isaya 10:27

It shall happen in that day, that his burden shall depart from off your shoulder, and his yoke from off your neck, and the yoke shall be destroyed by reason of fatness.

Amefika Ayathi; amepita kati ya Migroni; ameweka mizigo yake huko Mikmashi; Isaya 10:28

He is come to Aiath, he is passed through Migron; at Michmash he lays up his baggage;

wamevuka kivuko; wamekwenda kulala katika Geba; Rama unatetemeka; Gibea wa Sauli umekimbia. Isaya 10:29

they are gone over the pass; they have taken up their lodging at Geba; Ramah trembles; Gibeah of Saul is fled.

Piga kelele sana, Ee binti Galimu; sikiliza, Ee Laisha; ole wako, maskini Anathothi! Isaya 10:30

Cry aloud with your voice, daughter of Gallim! listen, Laishah! You poor Anathoth!

Madmena ni mkimbizi; wenyeji wa Gebimu wamejikusanya wakimbie; Isaya 10:31

Madmenah is a fugitive; the inhabitants of Gebim flee for safety.

siku hii ya leo atasimama huko Nobu; anatikisa mkono wake juu ya mlima wa binti Sayuni, mlima wa Yerusalemu. Isaya 10:32

This very day shall he halt at Nob: he shakes his hand at the mountain of the daughter of Zion, the hill of Jerusalem.

Angalia, Bwana, Bwana wa majeshi, atayakata matawi kwa nguvu za kutisha; nao walio warefu wa kimo watakatwa; na hao walioinuka wataangushwa chini; Isaya 10:33

Behold, the Lord, Yahweh of Hosts, will lop the boughs with terror: and the high of stature shall be hewn down, and the lofty shall be brought low.

naye atavikata vichaka vya msitu kwa chuma; na Lebanoni utaanguka kwa mkono wake aliye mwenye uweza. Isaya 10:34

He will cut down the thickets of the forest with iron, and Lebanon shall fall by a mighty one.