Isaya 52 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 52 (Swahili) Isaiah 52 (English)

Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi. Isaya 52:1

Awake, awake, put on your strength, Zion; put on your beautiful garments, Jerusalem, the holy city: for henceforth there shall no more come into you the uncircumcised and the unclean.

Jikung'ute mavumbi; uondoke, Uketi, Ee Yerusalemu; Jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Sayuni uliyefungwa. Isaya 52:2

Shake yourself from the dust; arise, sit [on your throne], Jerusalem: loose yourself from the bonds of your neck, captive daughter of Zion.

Maana Bwana asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha. Isaya 52:3

For thus says Yahweh, You were sold for nothing; and you shall be redeemed without money.

Maana Bwana MUNGU asema hivi, Watu wangu hapo kwanza walishuka Misri ili wakae huko hali ya ugeni; na Mwashuri akawaonea bila sababu. Isaya 52:4

For thus says the Lord Yahweh, My people went down at the first into Egypt to sojourn there: and the Assyrian has oppressed them without cause.

Basi sasa, nafanya nini hapa, asema Bwana, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema Bwana, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa. Isaya 52:5

Now therefore, what do I here, says Yahweh, seeing that my people is taken away for nothing? those who rule over them do howl, says Yahweh, and my name continually all the day is blasphemed.

Kwa hiyo watu wangu watalijua jina langu kwa hiyo watajua siku ile ya kuwa mimi ndimi ninenaye; tazama ni mimi. Isaya 52:6

Therefore my people shall know my name: therefore [they shall know] in that day that I am he who does speak; behold, it is I.

Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki! Isaya 52:7

How beautiful on the mountains are the feet of him who brings good news, who publishes peace, who brings good news of good, who publishes salvation, who says to Zion, Your God reigns!

Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja; Maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi Bwana arejeavyo Sayuni. Isaya 52:8

The voice of your watchmen! they lift up the voice, together do they sing; for they shall see eye to eye, when Yahweh returns to Zion.

Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja, Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa; Kwa kuwa Bwana amewafariji watu wake, Ameukomboa Yerusalemu. Isaya 52:9

Break forth into joy, sing together, you waste places of Jerusalem; for Yahweh has comforted his people, he has redeemed Jerusalem.

Bwana ameweka wazi mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu. Isaya 52:10

Yahweh has made bare his holy arm in the eyes of all the nations; and all the ends of the earth have seen the salvation of our God.

Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana. Isaya 52:11

Depart you, depart you, go you out from there, touch no unclean thing; go you out of the midst of her; cleanse yourselves, you who bear the vessels of Yahweh.

Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu Bwana atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde. Isaya 52:12

For you shall not go out in haste, neither shall you go by flight: for Yahweh will go before you; and the God of Israel will be your rearward.

Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa, na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana. Isaya 52:13

Behold, my servant shall deal wisely, he shall be exalted and lifted up, and shall be very high.

Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu), Isaya 52:14

Like as many were astonished at you (his visage was so marred more than any man, and his form more than the sons of men),

ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu. Isaya 52:15

so shall he sprinkle many nations; kings shall shut their mouths at him: for that which had not been told them shall they see; and that which they had not heard shall they understand.