Isaya 40 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 40 (Swahili) Isaiah 40 (English)

Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu. Isaya 40:1

Comfort you, comfort you my people, says your God.

Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa Bwana adhabu maradufu kwa dhambi zake zote. Isaya 40:2

Speak comfortably to Jerusalem; and cry to her, that her warfare is accomplished, that her iniquity is pardoned, that she has received of Yahweh's hand double for all her sins.

Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Isaya 40:3

The voice of one who cries, Prepare you in the wilderness the way of Yahweh; make level in the desert a highway for our God.

Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa; Isaya 40:4

Every valley shall be exalted, and every mountain and hill shall be made low; and the uneven shall be made level, and the rough places a plain:

Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya. Isaya 40:5

and the glory of Yahweh shall be revealed, and all flesh shall see it together; for the mouth of Yahweh has spoken it.

Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la kondeni; Isaya 40:6

The voice of one saying, Cry. One said, What shall I cry? All flesh is grass, and all the glory of it is as the flower of the field.

Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya Bwana yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani. Isaya 40:7

The grass withers, the flower fades, because the breath of Yahweh blows on it; surely the people is grass.

Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele. Isaya 40:8

The grass withers, the flower fades; but the word of our God shall stand forever.

Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, Panda juu ya mlima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu. Isaya 40:9

You who tell good news to Zion, go up on a high mountain; you who tell good news to Jerusalem, lift up your voice with strength; lift it up, don't be afraid; say to the cities of Judah, Behold, your God!

Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake. Isaya 40:10

Behold, the Lord Yahweh will come as a mighty one, and his arm will rule for him: Behold, his reward is with him, and his recompense before him.

Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole. Isaya 40:11

He will feed his flock like a shepherd, he will gather the lambs in his arm, and carry them in his bosom, [and] will gently lead those who have their young.

Ni nani aliyeyapima maji kwa konzi ya mkono wake, na kuzikadiri mbingu kwa shubiri, na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi, na kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani? Isaya 40:12

Who has measured the waters in the hollow of his hand, and meted out the sky with the span, and comprehended the dust of the earth in a measure, and weighed the mountains in scales, and the hills in a balance?

Ni nani aliyemwongoza roho ya Bwana, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake? Isaya 40:13

Who has directed the Spirit of Yahweh, or being his counselor has taught him?

Alifanya shauri na nani, ni nani aliyemwelimisha na kumfunza njia ya hukumu, na kumfunza maarifa, na kumwonyesha njia ya fahamu? Isaya 40:14

With whom took he counsel, and who instructed him, and taught him in the path of justice, and taught him knowledge, and shown to him the way of understanding?

Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana. Isaya 40:15

Behold, the nations are as a drop of a bucket, and are accounted as the small dust of the balance: Behold, he takes up the isles as a very little thing.

Lebanoni nayo hautoshi kwa kuni, wala wanyama wake hawatoshi kwa kafara. Isaya 40:16

Lebanon is not sufficient to burn, nor the animals of it sufficient for a burnt offering.

Mataifa yote huwa kama si kitu mbele zake; huhesabiwa kwake kuwa duni ya si kitu, na ubatili. Isaya 40:17

All the nations are as nothing before him; they are accounted by him as less than nothing, and vanity.

Basi, mtamlinganisha Mungu na nani? Au mtamfananisha na mfano wa namna gani? Isaya 40:18

To whom then will you liken God? or what likeness will you compare to him?

Sanamu fundi mmoja huiyeyusha, na mfua dhahabu huifunika dhahabu, huifulia mikufu ya fedha. Isaya 40:19

The image, a workman has cast [it], and the goldsmith overlays it with gold, and casts [for it] silver chains.

Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi mstadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika. Isaya 40:20

He who is too impoverished for [such] an offering chooses a tree that will not rot; he seeks to him a skillful workman to set up an engraved image, that shall not be moved.

Je! Hamkujua? Hamkusikia? Hamkuambiwa tokea mwanzo? Hamkufahamu tangu kuwekwa misingi ya dunia? Isaya 40:21

Have you not known? have yet not heard? has it not been told you from the beginning? have you not understood from the foundations of the earth?

Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa; Isaya 40:22

[It is] he who sits above the circle of the earth, and the inhabitants of it are as grasshoppers; who stretches out the heavens as a curtain, and spreads them out as a tent to dwell in;

ndiye awatanguaye wakuu, na kuwabatilisha waamuzi wa dunia. Isaya 40:23

who brings princes to nothing; who makes the judges of the earth as vanity.

Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu. Isaya 40:24

Yes, they have not been planted; yes, they have not been sown; yes, their stock has not taken root in the earth: moreover he blows on them, and they wither, and the whirlwind takes them away as stubble.

Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? Asema yeye aliye Mtakatifu. Isaya 40:25

To whom then will you liken me, that I should be equal [to him]? says the Holy One.

Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake. Isaya 40:26

Lift up your eyes on high, and see who has created these, who brings out their host by number; he calls them all by name; by the greatness of his might, and because he is strong in power, not one is lacking.

Mbona unasema, Ee Yakobo, mbona unanena, Ee Israeli, Njia yangu imefichwa, Bwana asiione, na hukumu yangu imempita Mungu wangu asiiangalie? Isaya 40:27

Why say you, Jacob, and speak, Israel, My way is hid from Yahweh, and the justice [due] to me is passed away from my God?

Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki. Isaya 40:28

Have you not known? have you not heard? The everlasting God, Yahweh, the Creator of the ends of the earth, doesn't faint, neither is weary; there is no searching of his understanding.

Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Isaya 40:29

He gives power to the faint; and to him who has no might he increases strength.

Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; Isaya 40:30

Even the youths shall faint and be weary, and the young men shall utterly fall:

bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. Isaya 40:31

but those who wait for Yahweh shall renew their strength; they shall mount up with wings as eagles; they shall run, and not be weary; they shall walk, and not faint.