Isaya 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 13 (Swahili) Isaiah 13 (English)

Ufunuo juu ya Babeli; maono aliyoyaona Isaya, mwana wa Amozi. Isaya 13:1

The burden of Babylon, which Isaiah the son of Amoz did see.

Haya! Juu ya mlima usio na miti inueni bendera, wapazieni sauti zenu, wapungieni mkono, kwamba waingie katika malango ya wakuu. Isaya 13:2

Set up an ensign on the bare mountain, lift up the voice to them, wave the hand, that they may go into the gates of the nobles.

Mimi mwenyewe nimewaamuru watu wangu waliowekwa wakfu kwangu, naam, nimewaita watu wangu walio hodari kwa ajili ya hasira yangu, watu wangu wenye kutakabari. Isaya 13:3

I have commanded my consecrated ones, yes, I have called my mighty men for my anger, even my proudly exulting ones.

Kelele milimani kama kelele za watu wengi sana; kelele za falme za mataifa waliokutana pamoja; Bwana wa majeshi anapanga jeshi kwa vita; Isaya 13:4

The noise of a multitude in the mountains, as of a great people! the noise of a tumult of the kingdoms of the nations gathered together! Yahweh of Hosts is mustering the host for the battle.

watu waliotoka katika nchi iliyo mbali, tokea upande wa mwisho wa mbingu; naam, Bwana na silaha za ghadhabu yake, ili aiangamize nchi yote. Isaya 13:5

They come from a far country, from the uttermost part of heaven, even Yahweh, and the weapons of his indignation, to destroy the whole land.

Pigeni kelele za hofu; maana siku ya Bwana i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu. Isaya 13:6

Wail; for the day of Yahweh is at hand; as destruction from the Almighty shall it come.

Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka. Isaya 13:7

Therefore shall all hands be feeble, and every heart of man shall melt:

Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto. Isaya 13:8

and they shall be dismayed; pangs and sorrows shall take hold [of them]; they shall be in pain as a woman in travail: they shall look in amazement one at another; their faces [shall be] faces of flame.

Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake. Isaya 13:9

Behold, the day of Yahweh comes, cruel, with wrath and fierce anger; to make the land a desolation, and to destroy the sinners of it out of it.

Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. Isaya 13:10

For the stars of the sky and the constellations of it shall not give their light; the sun shall be darkened in its going forth, and the moon shall not cause its light to shine.

Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali; Isaya 13:11

I will punish the world for [their] evil, and the wicked for their iniquity: and I will cause the arrogance of the proud to cease, and will lay low the haughtiness of the terrible.

nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri. Isaya 13:12

I will make a man more rare than fine gold, even a man than the pure gold of Ophir.

Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali. Isaya 13:13

Therefore I will make the heavens to tremble, and the earth shall be shaken out of its place, in the wrath of Yahweh of hosts, and in the day of his fierce anger.

Basi, itakuwa kama vile paa aliyetishwa, na kama kondoo wasio na mtu wa kuwakusanya; kila mtu atageukia watu wake; nao watakimbia, kila mtu aende nchi yake mwenyewe. Isaya 13:14

It shall happen, that as the chased roe, and as sheep that no man gathers, they shall turn every man to his own people, and shall flee every man to his own land.

Kila mtu atakayeonekana atatumbuliwa, na kila mtu atakayepatikana ataanguka kwa upanga. Isaya 13:15

Everyone who is found shall be thrust through; and everyone who is taken shall fall by the sword.

Na watoto wao wachanga watavunjwa-vunjwa mbele ya macho yao, nyumba zao zitatekwa nyara, na wake zao watatendwa jeuri. Isaya 13:16

Their infants also shall be dashed in pieces before their eyes; their houses shall be rifled, and their wives ravished.

Tazama, nitawaamsha Wamedi juu yao, ambao hawaoni fedha kuwa kitu, wala hawafurahii dhahabu. Isaya 13:17

Behold, I will stir up the Medes against them, who shall not regard silver, and as for gold, they shall not delight in it.

Na nyuta zao zitawaangusha vijana; wala hawatahurumia mazao ya tumbo; jicho lao halitawahurumia watoto. Isaya 13:18

[Their] bows shall dash the young men in pieces; and they shall have no pity on the fruit of the womb; their eye shall not spare children.

Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza. Isaya 13:19

Babylon, the glory of kingdoms, the beauty of the Chaldeans' pride, shall be as when God overthrew Sodom and Gomorrah.

Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko. Isaya 13:20

It shall never be inhabited, neither shall it be lived in from generation to generation: neither shall the Arabian pitch tent there; neither shall shepherds make their flocks to lie down there.

Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko. Isaya 13:21

But wild animals of the desert shall lie there; and their houses shall be full of doleful creatures; and ostriches shall dwell there, and wild goats shall dance there.

Na mbwa-mwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka. Isaya 13:22

Wolves shall cry in their castles, and jackals in the pleasant palaces: and her time is near to come, and her days shall not be prolonged.