Isaya 30 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 30 (Swahili) Isaiah 30 (English)

Ole wa watoto waasi; asema Bwana; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi; Isaya 30:1

Woe to the rebellious children, says Yahweh, who take counsel, but not of me; and who make a league, but not of my Spirit, that they may add sin to sin,

waendao kutelemkia Misri wala hawakuuliza kinywani mwangu; ili wajitie nguvu kwa nguvu za Farao, na kutumainia kivuli cha Misri. Isaya 30:2

that set out to go down into Egypt, and have not asked at my mouth; to strengthen themselves in the strength of Pharaoh, and to take refuge in the shadow of Egypt!

Basi, nguvu za Farao zitakuwa aibu yenu, na kutumainia kivuli cha Misri kutakuwa kufadhaika kwenu. Isaya 30:3

Therefore shall the strength of Pharaoh be your shame, and the refuge in the shadow of Egypt your confusion.

Kwa maana wakuu wake wako Soani, na wajumbe wake wamefika Hanesi. Isaya 30:4

For their princes are at Zoan, and their ambassadors are come to Hanes.

Wote watawaonea haya watu wasioweza kuwafaidia, wasio na msaada wala faida, bali ni aibu na sababu ya kushutumiwa. Isaya 30:5

They shall all be ashamed because of a people that can't profit them, that are not a help nor profit, but a shame, and also a reproach.

Ufunuo juu ya hayawani wa Negebu. Katikati ya nchi ya taabu na dhiki, Ambayo hutoka huko simba jike na simba, Nyoka na joka la moto arukaye, Huchukua mali zao mabegani mwa punda wachanga, Na hazina zao juu ya nundu za ngamia Waende kwa watu ambao hawatawafaa kitu. Isaya 30:6

The burden of the animals of the South. Through the land of trouble and anguish, from whence come the lioness and the lion, the viper and fiery flying serpent, they carry their riches on the shoulders of young donkeys, and their treasures on the humps of camels, to a people that shall not profit [them].

Kwa maana Misri huwasaidia bure, bila faida; Kwa hiyo nimemwita, Rahabu aketiye kimya. Isaya 30:7

For Egypt helps in vain, and to no purpose: therefore have I called her Rahab who sits still.

Haya, enenda sasa, andika neno hili katika kibao mbele ya macho yao, lichore katika kitabu ili liwe kwa ajili ya majira yatakayokuja, kwa ushuhuda hata milele. Isaya 30:8

Now go, write it before them on a tablet, and inscribe it in a book, that it may be for the time to come forever and ever.

Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana; Isaya 30:9

For it is a rebellious people, lying children, children who will not hear the law of Yahweh;

wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo; Isaya 30:10

who tell the seers, "Don't see;" and to the prophets, "Don't prophesy to us right things, speak to us smooth things, prophesy deceits,

tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; mkomesheni Mtakatifu wa Israeli mbele yetu. Isaya 30:11

get out of the way, turn aside out of the path, cause the Holy One of Israel to cease from before us."

Basi kwa ajili ya hayo Mtakatifu wa Israeli asema hivi, Kwa sababu mwalidharau neno hili, na kutumainia jeuri na ukaidi, na kuyategemea hayo; Isaya 30:12

Therefore thus says the Holy One of Israel, "Because you despise this word, and trust in oppression and perverseness, and rely thereon;

basi, uovu huu utakuwa kwenu kama mahali palipobomoka, palipo tayari kuanguka patokezapo katika ukuta mrefu, ambapo kuvunjika kwake huja ghafula kwa mara moja. Isaya 30:13

therefore this iniquity shall be to you as a breach ready to fall, swelling out in a high wall, whose breaking comes suddenly in an instant.

Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, akikivunja-vunja asiache kukivunja, hata hakipatikani katika vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani. Isaya 30:14

He shall break it as a potter's vessel is broken, breaking it in pieces without sparing; so that there shall not be found among the pieces of it a broken piece with which to take fire from the hearth, or to dip up water out of the cistern."

Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali. Isaya 30:15

For thus said the Lord Yahweh, the Holy One of Israel, In returning and rest shall you be saved; in quietness and in confidence shall be your strength. You would not:

Bali ninyi mlisema, La! Maana tutakimbia juu ya farasi; basi, ni kweli, mtakimbia; tena, Sisi tutakimbia juu ya wanyama waendao upesi; basi, wale watakaowafuatia watakuwa wepesi. Isaya 30:16

but you said, No, for we will flee on horses; therefore shall you flee: and, We will ride on the swift; therefore shall those who pursue you be swift.

Elfu moja watakimbia kwa kukemewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima. Isaya 30:17

One thousand [shall flee] at the threat of one; at the threat of five shall you flee: until you be left as a beacon on the top of a mountain, and as an ensign on a hill.

Kwa ajili ya hayo Bwana atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana Bwana ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao. Isaya 30:18

Therefore will Yahweh wait, that he may be gracious to you; and therefore will he be exalted, that he may have mercy on you: for Yahweh is a God of justice; blessed are all those who wait for him.

Kwa maana watu watakaa katika Sayuni huko Yerusalemu; wewe hutalia tena; hakika yake atakuonea rehema nyingi kwa sauti ya kilio chako; asikiapo ndipo atakapokujibu. Isaya 30:19

For the people shall dwell in Zion at Jerusalem; you shall weep no more; he will surely be gracious to you at the voice of your cry; when he shall hear, he will answer you.

Na ingawa Bwana atawapeni chakula cha shida na maji ya msiba, lakini waalimu wako hawatafichwa tena, ila macho yako yatawaona waalimu wako; Isaya 30:20

Though the Lord give you the bread of adversity and the water of affliction, yet shall not your teachers be hidden anymore, but your eyes shall see your teachers;

na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto. Isaya 30:21

and your ears shall hear a word behind you, saying, This is the way, walk you in it; when you turn to the right hand, and when you turn to the left.

Nanyi mtakitia najisi kifuniko cha sanamu zenu za fedha zilizochongwa, na mabamba ya sanamu zenu za dhahabu zilizoyeyushwa; utazitupilia mbali kama kitu kilicho najisi; utasema, Haya, toka hapa. Isaya 30:22

You shall defile the overlaying of your engraved images of silver, and the plating of your molten images of gold: you shall cast them away as an unclean thing; you shall tell it, Get you hence.

Naye atatoa mvua juu ya mbegu zako, upate kuipanda nchi hii; na mkate wa mazao ya nchi, nayo itasitawi na kuzaa tele; katika siku hiyo ng'ombe zako watakula katika malisho mapana. Isaya 30:23

He will give the rain for your seed, with which you shall sow the ground; and bread of the increase of the ground, and it shall be fat and plenteous. In that day shall your cattle feed in large pastures;

Ng'ombe pia na wana-punda wailimao nchi watakula chakula kilichokolea, kilichopepetwa kwa ungo na kwa pepeo. Isaya 30:24

the oxen likewise and the young donkeys that till the ground shall eat savory provender, which has been winnowed with the shovel and with the fork.

Na juu ya kila mlima mrefu, na juu ya kila kilima kilichoinuka, itakuwapo mito na vijito vya maji, katika siku ya machinjo makuu itakapoanguka minara. Isaya 30:25

There shall be on every lofty mountain, and on every high hill, brooks [and] streams of waters, in the day of the great slaughter, when the towers fall.

Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile Bwana atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha yao. Isaya 30:26

Moreover the light of the moon shall be as the light of the sun, and the light of the sun shall be sevenfold, as the light of seven days, in the day that Yahweh binds up the hurt of his people, and heals the stroke of their wound.

Tazama, jina la Bwana linakuja kutoka mbali sana, linawaka kwa hasira yake, kwa moshi mwingi sana unaopaa juu; midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni moto ulao; Isaya 30:27

Behold, the name of Yahweh comes from far, burning with his anger, and in thick rising smoke: his lips are full of indignation, and his tongue is as a devouring fire;

na pumzi yake ni kijito kifurikacho, kifikacho hata shingoni, kupepeta mataifa kwa ungo wa ubatili; na lijamu ikoseshayo itakuwa katika taya za watu. Isaya 30:28

and his breath is as an overflowing stream, that reaches even to the neck, to sift the nations with the sieve of destruction: and a bridle that causes to err [shall be] in the jaws of the peoples.

Mtakuwa na wimbo kama vile wakati wa usiku, ishikwapo sikukuu takatifu, mtakuwa na furaha ya moyo kama vile mtu aendapo na filimbi katika mlima wa Bwana, aliye Mwamba wa Israeli. Isaya 30:29

You shall have a song as in the night when a holy feast is kept; and gladness of heart, as when one goes with a pipe to come to the mountain of Yahweh, to the Rock of Israel.

Naye Bwana atawasikizisha watu sauti yake ya utukufu, naye atawaonyesha jinsi mkono wake ushukavyo, na ghadhabu ya hasira yake, na mwako wa moto ulao, pamoja na dhoruba, na tufani, na mvua ya mawe ya barafu. Isaya 30:30

Yahweh will cause his glorious voice to be heard, and will show the lighting down of his arm, with the indignation of [his] anger, and the flame of a devouring fire, with a blast, and tempest, and hailstones.

Maana kwa sauti ya Bwana, Mwashuri atavunjika-vunjika, yeye apigaye kwa bakora. Isaya 30:31

For through the voice of Yahweh shall the Assyrian be dismayed; with his rod will he strike [him].

Na kila pigo la fimbo iliyoamriwa, ambayo Bwana ataliweka juu yake, litakuwa pamoja na matari na vinanda, na kwa mapigano yenye kutikisa atapigana nao. Isaya 30:32

Every stroke of the appointed staff, which Yahweh shall lay on him, shall be with [the sound of] tambourines and harps; and in battles with the brandishing [of his arm] will he fight with them.

Maana Tofethi imewekwa tayari tokea zamani, naam, imewekwa tayari kwa mfalme huyo; ameifanya kubwa, inakwenda chini sana; tanuru yake ni moto na kuni nyingi; pumzi ya Bwana, kama mto wa kiberiti, huiwasha. Isaya 30:33

For a Topheth is prepared of old; yes, for the king it is made ready; he has made it deep and large; the pile of it is fire and much wood; the breath of Yahweh, like a stream of sulfur, does kindle it.