Isaya 65 Swahili & English

Listen/Download Audio
Isaya 65 (Swahili) Isaiah 65 (English)

Watu wasionitaka wanauliza habari zangu; nimeonekana na hao wasionitafuta; naliliambia taifa lisiloitwa kwa jina langu, Isaya 65:1

I am inquired of by those who didn't ask; I am found by those who didn't seek me: I said, See me, see me, to a nation that was not called by my name.

Nitazameni, nitazameni. Mchana kutwa nimewanyoshea mikono yangu watu walioasi, watu waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe; Isaya 65:2

I have spread out my hands all the day to a rebellious people, who walk in a way that is not good, after their own thoughts;

watu wanikasirishao mbele za uso wangu daima, wakitoa dhabihu katika bustani zao, na kufukiza uvumba juu ya matofali; Isaya 65:3

a people who provoke me to my face continually, sacrificing in gardens, and burning incense on bricks;

waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika vyombo vyao; Isaya 65:4

who sit among the graves, and lodge in the secret places; who eat pig's flesh, and broth of abominable things is in their vessels;

watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi, kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu, moto uwakao mchana kutwa. Isaya 65:5

who say, Stand by yourself, don't come near to me, for I am holier than you. These are a smoke in my nose, a fire that burns all the day.

Tazama, neno hili limeandikwa mbele zangu. Sitanyamaza, lakini nitalipa, naam, mimi nitawalipa ujira wao vifuani mwao; Isaya 65:6

Behold, it is written before me: I will not keep silence, but will recompense, yes, I will recompense into their bosom,

maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema Bwana, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao. Isaya 65:7

your own iniquities, and the iniquities of your fathers together, says Yahweh, who have burned incense on the mountains, and blasphemed me on the hills; therefore will I first measure their work into their bosom.

Bwana asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote. Isaya 65:8

Thus says Yahweh, As the new wine is found in the cluster, and one says, Don't destroy it, for a blessing is in it: so will I do for my servants' sake, that I may not destroy them all.

Nami nitaleta uzao toka Yakobo, na mrithi wa milima yangu toka Yuda, na mteule wangu atairithi, na watumishi wangu watakaa huko. Isaya 65:9

I will bring forth a seed out of Jacob, and out of Judah an inheritor of my mountains; and my chosen shall inherit it, and my servants shall dwell there.

Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng'ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. Isaya 65:10

Sharon shall be a fold of flocks, and the valley of Achor a place for herds to lie down in, for my people who have sought me.

Bali ninyi mmwachao Bwana, na kuusahau mlima wangu mtakatifu, na kuandika meza kwa ajili ya Bahati, na kuijazia Ajali vyombo vya divai iliyochanganyika; Isaya 65:11

But you who forsake Yahweh, who forget my holy mountain, who prepare a table for Fortune, and who fill up mixed wine to Destiny;

mimi nitawaandikia kuuawa kwa upanga, na ninyi nyote mtainama ili kuchinjwa; kwa sababu nilipoita hamkuitika; niliponena, hamkusikia; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambo nisiyoyafurahia. Isaya 65:12

I will destine you to the sword, and you shall all bow down to the slaughter; because when I called, you did not answer; when I spoke, you did not hear; but you did that which was evil in my eyes, and chose that in which I didn't delight.

Kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, watumishi wangu watakula, bali ninyi mtaona njaa; tazama, watumishi wangu watakunywa, bali ninyi mtaona kiu; tazama, watumishi wangu watafurahi, bali ninyi mtatahayarika; Isaya 65:13

Therefore thus says the Lord Yahweh, Behold, my servants shall eat, but you shall be hungry; behold, my servants shall drink, but you shall be thirsty; behold, my servants shall rejoice, but you shall be disappointed;

tazama, watumishi wangu wataimba kwa furaha ya moyo, bali ninyi mtalia kwa huzuni ya moyo; mtapiga kelele kwa sababu ya uchungu wa roho zenu. Isaya 65:14

behold, my servants shall sing for joy of heart, but you shall cry for sorrow of heart, and shall wail for vexation of spirit.

Nanyi mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa wateule wangu. Na Bwana MUNGU atakuua; naye atawaita watumishi wake kwa jina lingine. Isaya 65:15

You shall leave your name for a curse to my chosen; and the Lord Yahweh will kill you; and he will call his servants by another name:

Hata itakuwa yeye atakayejibariki duniani, atajibariki kwa Mungu wa kweli; naye atakayeapa duniani, ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za kwanza zimesahauliwa, na kwa kuwa zimefichwa machoni pangu. Isaya 65:16

so that he who blesses himself in the earth shall bless himself in the God of truth; and he who swears in the earth shall swear by the God of truth; because the former troubles are forgotten, and because they are hid from my eyes.

Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni. Isaya 65:17

For, behold, I create new heavens and a new earth; and the former things shall not be remembered, nor come into mind.

Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha. Isaya 65:18

But be you glad and rejoice forever in that which I create; for, behold, I create Jerusalem a rejoicing, and her people a joy.

Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza. Isaya 65:19

I will rejoice in Jerusalem, and joy in my people; and there shall be heard in her no more the voice of weeping and the voice of crying.

Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa. Isaya 65:20

There shall be no more there an infant of days, nor an old man who has not filled his days; for the child shall die one hundred years old, and the sinner being one hundred years old shall be accursed.

Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Isaya 65:21

They shall build houses, and inhabit them; and they shall plant vineyards, and eat the fruit of them.

Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine; maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi. Isaya 65:22

They shall not build, and another inhabit; they shall not plant, and another eat: for as the days of a tree shall be the days of my people, and my chosen shall long enjoy the work of their hands.

Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na Bwana, na watoto wao pamoja nao. Isaya 65:23

They shall not labor in vain, nor bring forth for calamity; for they are the seed of the blessed of Yahweh, and their offspring with them.

Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia. Isaya 65:24

It shall happen that, before they call, I will answer; and while they are yet speaking, I will hear.

Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema Bwana. Isaya 65:25

The wolf and the lamb shall feed together, and the lion shall eat straw like the ox; and dust shall be the serpent's food. They shall not hurt nor destroy in all my holy mountain, says Yahweh.